Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 126,599
- 241,419
Tungali tunaendelea na nyuzi za mwezi wa 3 ambao ni Mwezi wa Mungu
Kwenye awamu hii utajiri ulikuwa sawa na Uhaini , ukiwa na hela nyingi hata kama zimetokana na Mahindi uliyolima mwenyewe utakiona cha moto , kama hujaitwa kuhojiwa ama hujakamatwa na kupewa kesi ya Uhujumu uchumi , basi ukiamka asubuhi utakuta hela zako zimesombwa .
Kulikuwa na wivu wa kijinga sana ambao haufahamiki ulitoka wapi , Maduka ya halali ya kubadilishia fedha za kigeni yakavamiwa na vikosi maalum , yakasachiwa na kuporwa kila kilichomo na kufungwa , wenye mali wakakamatwa na kuhojiwa huku wakitishwa .
Wafanyabiashara wenye mafanikio waliopata tenda za serikali kwa halali wakadakwa na kuswekwa rumande , huku wengine wakipewa kesi za kutisha za Uhujumu uchumi na madawa ya kulevya , Mfano wa karibu alikuwa Yusufu Manji , Mfadhili na kiongozi wa Yanga na Diwani wa Mbagala Kuu
Huyu alipewa kihalali kazi za kutengeneza sare zaJeshi , magari ya Polisi na Majengo ya serikali na akapata pesa akawa Tajiri , hapa kosa lake lilikuwa nini ? kuhusu namna alivyoshinda tenda waulizwe viongozi wa awali .
Mwingine katika wengi walioonewa ni Mzee Rugemalira , huyu Mzee kwanza namshukuru kwa ujasiri wake wa kugoma kuomba radhi na kukubali ule ujinga wa Plea Bargain , huyu alimiliki kihalali kampuni yake iliyoingia ubia na IPTL , kalipwa hela zake halali za Escrow akaunti akadhalilishwa na kurundikwa jela
Ikumbukwe kwamba Rugemalira hana uhusiano wowote na huyo Harbinder , Wamekutana Jela tu , Harbinder aliletwa na watu wa serikali ili ainunue IPTL na kumdhulumu Rugemalira , kama Harbinder alikuwa na Makosa hayo hayakumhusu Rugemalira , Tunamshukuru Mama yule Tibaijuka aliyemstua Ruge kwamba kulikuwa na njama za kumdhulumu hela zake , yaani mpango ulikuwa ni kumpa hisa zote za IPTL Harbinder ili kumpiga Ruge (Hili ndio lilisababisha Tibaijuka kufutwa uwaziri , achaneni na zile porojo zingine)
Kwa wasioelewa hapa ni hivi , huyu Ruge alikuwa na hisa zake za IPTL kama vile Karamagi alivyokuwa TICS , hivi leo unaweza kuzuia hisa za Karamagi huko TICS ukaeleweka ? Kama Ruge angekuwa na Kiherehere kwa zile hisa za 30% kwenye IPTL ndiye angekuwa msemaji na kiongozi wa IPTL kama alivyokuwa Karamagi na hisa zake za 30% TICS , hapa naandika ili kuonyesha kwamba Ruge alionewa tu na ndio maana Ameachiwa huru bila masharti yoyote.
Ni kweli kwamba kulikuwa na wezi wa mali ya umma , lakini isingewezekana kila Tajiri awe mwizi , huyu Rugemalira ndiye aliyeingiza vinywaji vitamu kwenye nchi hii kutoka ulaya kwa miaka mingi mno , zikiwemo hizo bia tamu za Heineken , mtu mwenye juhudi kama hizo awezaje kukosa hela ? Utajiri haujawahi kuwa dhambi wala umasikini siyo utakatifu , bali ni laana kuu kwa Mungu .
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO