Aveva na "genge" lako.. Jipimeni Mapema

Hata Mimi nasikia kua "Mfanyabiashara" Mo anaitaka Simba.. Tunatakiwa tutafakari sana kabla ya kumkabidhi timu huyu "Mfanyabiashara".
Alishindwa kuihudumia Mbagala Market ataiweza Simba?
 
...hebu nielekezeni,kuna ubaya gani wa MO kupewa timu?,km atajenga facilities kwa ajili ya timu kufanyia mazoezi,atasajili wachezaji wa viwango toka pande zote za dunia (sio mafundi wa mtibwa!),alipe mishahara ya wachezaji kwa wakati...hatimaye Mungu akijalia,timu ianze kufanya vizuri kitaifa na kimataifa,hata km jamaa atapata "faida" ambayo siijui ni faida gani!,hivi sisi mashabiki wa Simba tutapungukiwa na nini?!
....Hawa jamaa wamekataa bilioni 10 za MO kwa kudai ni ndogo,halafu timu ikaendelea kufanya vibaya mpk mwisho wa ligi,hivi kwanini basi wao wasingeweka bilioni 30 km wanazo!,na wala sio kutudanganya timu ina thamani halafu inaendelea kudidimia kimpira!,tusileweshwe na propaganda za hawa matapeli mpeni timu "MO".
Furaha yetu siku zote ni Ushindi/Ubingwa!,nothing else!

Mbagala market aliitelekezea wapi huyu Mo?
 
Mbagala market aliitelekezea wapi huyu Mo?
Hili ndilo hata Mimi linanipa ukakasi.. Kama alishindwa vidogo.. Ataweza vikubwa kweli?
Tunatakiwa tuwe makini sana katika hili.
 
Mbagala market aliitelekezea wapi huyu Mo?
.....acheni kushadadia mambo yaliyopita wakati sasa hivi Simba inafanya vibaya,hao mbagala market huwezi kuwaweka kundi moja na Simba,muacheni mwenye pesa achukue timu awekeze hadhi ya Simba irudi,habari ya kuhukumu kabla hajafanya chochote ni ujinga tu!,vinginevyo endeleeni kuuliza maswali yenu ya kitoto Simba iendelee kugeuzwa paka!
 
Kumbe tupo wengi tulioshtukia huu mchezo wa viongozi wa simba kucheza na akili zetu kutumia magazeti. Kwanza walishatudanganya sana kuanzia miaka hiyo mara aucho halid, mavugo, mshambuliaji na kipa wa gor mahia (majina yamenitoka) n.k. tukaishia kuona wakina nserekuma na papa ndaw. Kamati ya ufundi inasema ina listi wachezaji 33 wanataka kuwasajili hivi kila mwaka simba inaundwa upya? Kamati makini ya ufundi ingekuwa na listi ya wachezaji wasiozidi 10 saba wa ndani na 3 wa nje kwani timu inaanza kuundwa na wachezaji waliopo unaendelea kuwapunguza taratibu kila mwaka then ndani ya miaka 3 unapata timu imara. Inaelekea hata hawajui mapungufu ya simba nini? Halafu unaanza kuajiri kocha au unaanza kusajili wachezaji? Je wachezaji unaosajili wasipoendana na mfumo wa kocha alumiwe nani mbele ya safari?
 
Back
Top Bottom