Athari za Uchaguzi Mkuu, Azam TV wapandisha bei za vifurushi?

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,418
Wakati wanazindua mzigo mpya 'Bazzika' walijifanya wanapunguza bei za vifurushi lakini kiukweli WAMEPANDISHA BEI.

Hawa ni wapigaji kama wapigaji wengine. Wangebakiza channel za vifurushi husika kama zamani, kwa mfano: Vifurushi vilivyokuwa vinapatikana ndani ya Azam Lite ya Sh. 10,000/= vingebakizwa ndani ya Azam Lite ya Sh. 8,000/= lakini cha kushangaza vimepelekwa kwenye kifurushi cha Sh. 13,000/=.

Kifurushi cha Sh. 18,000/= kimepunguzwa hadi Sh. 13,000/= lakini cha kushangaza ni kwamba channel za Azam Sports 1 na 2 ambazo zilipelekea wateja wanunue kifurushi hiki hazipatikani kwa hiyo bei mpya ya Sh. 13,000/= bali wamezihamishia kwenye kifurushi kingine cha Sh. 20,000/=

Channel zilizokuwa zinapatikana kwenye kifurushi cha Sh. 23,000/= ambacho kimepunguzwa hadi Sh. 20,000/= zimehamishiwa kwenye kifurushi cha Sh. 28,000/=.

AZAM TV, hamjapunguza bei bali mmepandisha. SIJUI MNATUCHUKULIAJE SISI AKINA YAKHE!

Simenti imepanda bei, Azam TV wamepandisha bei, tutegemee bei kupanda zaidi kwenye bidhaa na huduma nyingine.
 
Wakati wanazindua mzigo mpya 'Bazzika' walijifanya wanapunguza bei za vifurushi lakini kiukweli WAMEPANDISHA BEI...
Sio kweli fatilia vizuri mkuu, channel baadhi za 23000 zimeletwa kwenye kifurushi Cha 20000 mfano MBC 2, MBC ACTION na MBC MAX
 
Wamepandisha bei ya ving'amuzi zao lakini wamepunguza bei ya juice zao! Wanajali wanyonge. Hongera Azam.
 
Startimes wanatakiwa kuonesha ligi ya nyumbani ili tuhame Azam maana hata app ni ya hovyo sijawahi kuona
 
Back
Top Bottom