ATC vs KQ: Management Ndio Dawa

Akilimtindi,
Mimi naamini kabisa kuwa Balali asingeshindwa kuiendesha benki kuu ipaswavyo yaani Kiutaalam. Tatizo wajomba ni hizo SIASA kuingilia kati. Maswala ya EPA na mikopo yote ambayo imewahi kutangulia inajulikana kabisa kwamba ni mpango ule ule toka UJAMAA ambapo hata scholarship tu ilikuwa lazima ipitiwe na wanansiasa acha mbali kupata Passport ya kusafiria..Ni mpango huo huo unaendelea hadi leo, tazama form za Passport ni lazima uwe na barua toka kwa kiongozi wa kata yako!.. I mean sasa hivi uraia umekuwa ni mahala unapoishi sio tena kuzaliwa. Mtanzania mzawa ambaye anaishi nje ni second class citizen, hana haki sawa na Mhindi aliyehamia Tanzania... this is how we do it!

Kwa hiyo huo msemo.. una maana moja tu Ujamaa bado upo, siasa zinatangulia kila kitu ndio maana hata wasomi wetu wanakimbilia viti vya Uheshimiwa hata iwe Udiwani tu unatosha kuitafuta POWER!.
 
Ndugu zangu wana JF, yanayotokea Kenya Airways ni matayarisho ya siku nyingi baada ya kazi ngumu na kubwa ya kulijenga Shirika hilo.

Nina weza kufananisha Kenya Airways na Air Tanzania kama hivi:

Kenya airways ni sawasawa na Jengo jipya ambalo tayari linatumika kikamilifu na linaeleweka.

Air Tanzania ni kiwanja ambacho bado hakijajengwa kabisa labda pana safishwa tu kila wakati baada ya majani kuota.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, serikali haina budi kuleta wataalam watakaoweza kuijenga Air Tanzania kutoka katika hali mbaya iliyonayo sasa hivi.

Kuwekeza Fedha pekee haitoshi, kunahitajika utaalam maalum unaoendana na hali ya sasa ya biashara ya usafiri wa anga. Nina imani kuwa wapo vijana wengi tu wa kitanzania ambao tayari wana-exposure na experience inayolingana na Mbughua au hata zaidi. Kinachotakiwa ni kuwatafuta halafu unawachanganya na wataalam waliobobea katika fani ya uongozi wa masuala ya anga nina hakika ATC tunayoiona sasa hivi itabadilika na kuchukua mwelekeo chanya.
 
ajay

aliingizwa na bodi iliyopita nikiwa pale kabla sijaenda nje akiongozwa na alhaji mwizi mfuruki
akafayna kazi bila kibali tukajitahidi kuwaeleza serikali wakampiga ...@##$$$ haraka sana akaarudishwa dubai baya zaidi nikiwa najitayarisha kukimbia mfuruki akaapa atarudi na na kuwa director mwenye uwezo amguse...kweli akaingia akapewa dir ....kabla ya kurudi baada ya kufukuzwa mfuruki alijitahidi kumkimbizaawe managrer s.africa wakamchomea akakimbilia nairobi then akaahadiwa manager walipoona hakuna uwezekano wakampatia kuja dar!!!!

wasifu mmoja wapo sijui kama bado yupo maana alikuwa mwoga sana akiwa anaaanza kazi!!!
 
Kubwajinga,
Mimi sina tatizo na ELIMU ya viongozi wa mashirika yetu ati ni lazima iwe na kiwango fulani isipokuwa ni pamoja na Exposure na Experience ya mtu huyo ktk uendeshaji wa mashirika ya biashara hasa ktk dunia hii ya Utandawazi.

Dunia hii, mbali na elimu ya darasa inatakiwa sana Experience na Exposure, ..

Mkuu Mkandara,
Nakubaliana kabisa na mawazo yako. Hili hata Mwalimu alilitamani tatizo ni kuwa hakulielewa vizuri. Nakumbuka enzi zake wale wote waliosomeshwa nje ya nchi walipata upendeleo katika ajira. Kwa mfano ukisomea urusi, UK n.k., unakuwa na thamani kuliko wa UDSM, lakini walisahau kuwa exposure waliyopata ilikuwa ni ya darasani tu yenye limitation maana haihusiani na utendaji, i.e. hawakuwa na uzoefu wa kazi hasa kama zinavyofanywa huko walikosomea.

Matokeo yake ikawa, tukapata wasomi wazuri na wakapewa madaraka makubwa lakini wengi wao walivurunda kwa kutokuwa na uzoefu wa kazi.

Tulisahau kuwa hawa wote walitakiwa wamu-understudy mtu na sio wao kuvumbua jinsi ya kufanya kazi.

Nafikiri Kikwete naye ana mtazamo wake ulio mbaya zaidi, kwani yeye anaangalia tu kama una degree na una ushoga naye. Hiyo inatosha kukupa kazi ya majukumu makubwa licha ya kuwa dunia imebadilika zaidi ya wakati wa Mwalimu. Kikwet wala haangalii degree yenyewe umeipatia wapi ndio maana watu kama akina Nchimbi wamepewa madaraka ya juu licha ya kuwa na vyeti nyanya.
 
Pointi ambayo nitaiunga mkono ni hiyo ya kutenganisha siasa na biasara,sasa hivi mtu anapewa kuwa CEO kama zawadi baada ya kufanya jambo flani au sababu ya kufahamiana na mtu fulani au anatoka familia fulani.Mtu huyu naye anajua ni kwa vp amepata hiyo nafasi naye anaitumia kuchuma hadi anakata tawi alilokalia au waswahili wanasema anakula akishiba anakunya kwenye unga bila kujua kesho tena yeye au mtoto wake au mjomba wake atahitaji kula.

Mtu Mzima,
Maneno ya kiutu uzima hayo na yanaligusa karibu baraza zima la mawaziri la JK na wengineo wote aliowateua katika kila idara na mashirika ya serikali. Sasa kazi anayo maana wakivurunda mahali na ikihitajika awabadilishe, bado itabidi awatafutie ulaji sehemu nyingine, sasa sijui atawaundia mashirika au wizara nyingine maana si unajua tena si ni washikaji zake?
 
Back
Top Bottom