LGE2024 Askofu Dr Bagonza: Nendeni mkajiandikishe Kupiga Kura, atakayeiba kura Dhambi ni zake na Wasipoiba Kura Utapata Kiongozi unayempenda!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Askofu Dr Bagonza amewataka Wananchi wote wakajiandikishe kupiga Kura Ili wapate fursa ya kuchagua Viongozi wanaowapenda

" Nendeni mkajiandikishe Kupiga Kura Ili kama kuna Wezi wa Kura wapate cha kuiba" amesema baba Askofu

" Wakiiba kura Dhambi ni za kwao Lakini wewe utakuwa umetimiza wajibu wako mbele ya Mungu wa Mbinguni" amesisitiza Mtumishi huyu wa Mungu

" Wasipoiba Kura na Mgombea uliyemchagua akashinda basi utakuwa na Furaha ya Kuongozwa na Kiongozi halali mbele ya Mungu wa Mbinguni na mbele ya Wanadamu na Unayempenda" amemalizia Askofu Dr Bagonza wa KKKT

Ahsanteni sana 😄🌹
Hapo kwenye dhambi ni zake ameteleza, alitakiwa kusema atakayeiba kura, familia yake iwe matatani.
 
Hili swala kujiandikisha kupiga kura vijana tulichukulie serious, vijana wengi hatuja jiandikisha, na hatujali.

Vijana Tz wanatakiwa waamke, vijana ni wengi lakini hawapigi kura sasa upinzani utashinda vipi? Maana ma ccm humasisha vijana wao wajiandikishe ili wapige kura , mwisho wa siku yana shibda.

Tz vijana sijui kwa nini wavivu wavivu, hawajali as if maisha yao ni bora sana, vijana hawa ndo wana sababisha upinzani kuanguka, kwa hali hii ccm yata shinda sana na tutalsumu sana.
 
Back
Top Bottom