Askofu Dkt. Fredrick Shoo asema Kanisa la Kilutheri lina imani na Rais Samia

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
913
2,521
MHESHIMIWA RAIS KANISA LIPO PAMOJA NAWE

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo amesema Kanisa hilo lina imani na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba litaendelea kusimama naye katika maombi na kumuunga mkono katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Dkt. Shoo ametoa kauli hiyo mkoani Arusha yanapofanyika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Amesema amelazimika kuzungumza hayo kufuatia kinaoendelea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu suala la uwekezaji wa bandari na kampuni ya DP World.

“Tuna imani na wewe Mheshimiwa Rais, tunakuamini Mheshimiwa Rais na tunaamini kwamba ukisema taasisi zako na vyombo vyako vitafanyia kazi jambo hili unamaanisha hivyo,"

"Sasa najua katika jambo hili tumeelekea mahali ambapo tunataka kugawanyika kabisa na wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na maslahi ya kiuchumi. Namshukuru Mungu amekujaalia hekima katika hili kama Mama na kiongozi umekaa kimya.

Kimya chako hiki Mheshimiwa Rais sio kwamba hulifanyii kazi, na mimi nasema jambo hili linahitaji hekima kubwa ya kuliendea na sisi kama tulivyosema tunaendelea kukuombea kwa Mungi ili hekima yote itumike katika kuweza kuleta muafaka wa jambo hili pasipo kugawanya au Wananchi kugawanyika na kutumika kama kitu cha kuchochea Wananchi kwa watu wenye maelengo yao mengine. Amesema Dkt.Shoo.

FB_IMG_1692636489081.jpg
 
Bila shaka kuwa Dr Frederick Shoo ana imani na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa atachukua uamuzi ulio sahihi...

Hata mimi nina imani naye na ninajua ni mwanamke mwenye hekima na busara nyingi tu na Kwa hiyo atachukua uamuzi wenye busara bila shaka. Akifanya kinyume kwenye hili, Tanganyika itamshangaa!!!

Dr Frederick Shoo amempa ujumbe Rais Kwa njia ya hekima sana..

Na hapa kwa serikali ina maana kuwa, uamuzi sahihi anaomaanisha Dr Shoo ni kufanya kile ambacho umma/wananchi wanasema na kutaka...

Kwa mkataba wa bandari, wananchi wanasema na tumeshasema HAPANA Kwa harufi kubwa kabisa...

Mwenye hekima hufanya kilicho sahihi. Mpumbavu hushupaza shingo hata kujikwaa na kuangukia shimoni..

Ni juu yake Rais Samia Suluhu Hassan kuchagua awe upande wa kiongozi/Rais WENYE HEKIMA au UPUMBAVU aendelee kushupaza shingo yake hadi ivunjike kwa kufanya maamuzi yenye makosa tena na tena na tena.....
 
Askofu ametumia diplomatic way of saying "MHESHIMIWA SUALA HILI ACHANA NALO,TUMIA HEKIMA KWASABAB WEW TU TU NDIO UNAWEZA KUAMURU VYOMBO VINGINE KULIFANYIA KAZI"..
Ahsante Askofu atakuwa amekuelewa
Exactly..

Lakini, robots za upande ule wa kijani, kama mazuzu zinadhani Dr Shoo na KKKT kwa ujumla wake wanakubaliana na mkataba huu mbovu na hovyo kwa vipimo vyote..
 
Hakuna kanisa ambalo lipo kinyume na Rais ila zinapotokea sintofaham lazima wahoji. Na bado askofu huyo kasema kanisa linapo onya na kukemea wasiambiwe neno kuchanganya dini na siasa
Askofu Shoo kasema Viongozi wote waliomba wamuone Rais kuhusu Mkataba wa Bandari na Rais akawapokea na kuwasikiliza na kubwa zaid akaahidi kuyashughulikia maombi yao na hoja yao kuu ilikuwa ni kuboresha Mkataba kwa kuondoa au kuongeza mambo yenye manufaa kwa Nchi, na mchakato na mjadala unaendelea kwa makundi mengine

Ghafla linatokea Kundi linajiona kubwa kuliko Serikali na kuanza kuja na vitisho sijui wanasomea wafuasi wao Waraka sijui usomwe kwny Ibada, sijui hawataki kabisa uwekezaji n.k so what?

This time watapata lesson kuwa Nchi ni kubwa kuliko vikundi vya kidini, kisiasa na kijamii

Lengo la kwanza kum frustrate Rais na Serikali tayari wameshindwa na nini kusomewa waraka hata kama wakitaka kuwasaidia kusambaza nakala za Waraka tutafanya hivyo cha msingi kila mtu kila kikundi kijue Tanzania ni kubwa zaid yao
 
Askofu Shoo kasema Viongozi wote waliomba wamuone Rais kuhusu Mkataba wa Bandari na Rais akawapokea na kuwasikiliza na kubwa zaid akaahidi kuyashughulikia...
Unajidanganya bwana Pohamba, penda usipende RC wapo mbali sana...wanajua wanachofanya.

Najua ule waraka umekuumiza sana.

Vumilia hii ni National interest
 
Unajidanganya bwana Pohamba......penda usipende RC wapo mbali sana...wanajua wanachofanya.....
Najua ule waraka umekuumiza sana..
Vumilia hii ni National interest
Uniumize kwani huu Waraka wa kwanza kutolewa ?

RC wako mbali sana wala si uongo, ila pia nawe usitudanganye kuwa ni wanasimamia Maslahi ya Nchi, Bank yao ya Ukombozi ndio ilikuwa uchochoro wa kupitisha Miamala ya Escrow na Maaskofu waliochonga huo Mchongo walilipwa na majina yakatoka

kwny Miradi ya Fedha wanazopokea toka Serikalini kuna Ufissdi wa kutisha hadi wahusika wamejirusha kwny maghorofa na kupoteza maisha kukimbia Scandle

kwmy Siasa za Kimataifa nakukumbusha tu wao ndio waliokuwa wakandarasi wa mauaji ya Kimbari Rwanda 1994

kwny Second World war sitaki kukuumiza roho kukutajia role yao kwny mauaji ya Wayahudi wakisaidiana na Wanazi

hapo sitaki kuhesabika nadhalilisha Taasisi yako pendwa nikikutajia kashfa zao kwny Unyanyasaji wa kingono kwa Watoto

Wewe una haki ya kuwaheshimu kwa kadri unavyowaheshimu nami nina wajibu wa kuwaheshimu kwa kuwa wanaheshimiwa na wale ninao waheshimu sana lakini msivuke mipaka mkawapa Uadilifu sijui uzalendo ambao hawana kwa historia yao na matendo yao.
 
Askofu Shoo kasema Viongozi wote waliomba wamuone Rais kuhusu Mkataba wa Bandari na Rais akawapokea na kuwasikiliza na kubwa zaid akaahidi kuyashughulikia maombi yao na hoja yao kuu ilikuwa ni kuboresha Mkataba kwa kuondoa au kuongeza mambo yenye manufaa kwa Nchi, na mchakato na mjadala unaendelea kwa makundi mengine

Ghafla linatokea Kundi linajiona kubwa kuliko Serikali na kuanza kuja na vitisho sijui wanasomea wafuasi wao Waraka sijui usomwe kwny Ibada, sijui hawataki kabisa uwekezaji n.k so what?

This time watapata lesson kuwa Nchi ni kubwa kuliko vikundi vya kidini, kisiasa na kijamii

Lengo la kwanza kum frustrate Rais na Serikali tayari wameshindwa na nini kusomewa waraka hata kama wakitaka kuwasaidia kusambaza nakala za Waraka tutafanya hivyo cha msingi kila mtu kila kikundi kijue Tanzania ni kubwa zaid yao

mimi sio rc ila rais atumie busara hao watu hawawezi hata kidogo. asijifanye kufurukuta.
 
MHESHIMIWA RAIS KANISA LIPO PAMOJA NAWE

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo amesema Kanisa hilo lina imani na Rais Samia Suluhu Hassan na kwamba litaendelea kusimama naye katika maombi na kumuunga mkono katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Dkt. Shoo ametoa kauli hiyo mkoani Arusha yanapofanyika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Amesema amelazimika kuzungumza hayo kufuatia kinaoendelea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu suala la uwekezaji wa bandari na kampuni ya DP World.

“Tuna imani na wewe Mheshimiwa Rais, tunakuamini Mheshimiwa Rais na tunaamini kwamba ukisema taasisi zako na vyombo vyako vitafanyia kazi jambo hili unamaanisha hivyo,"

"Sasa najua katika jambo hili tumeelekea mahali ambapo tunataka kugawanyika kabisa na wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na maslahi ya kiuchumi. Namshukuru Mungu amekujaalia hekima katika hili kama Mama na kiongozi umekaa kimya.

Kimya chako hiki Mheshimiwa Rais sio kwamba hulifanyii kazi, na mimi nasema jambo hili linahitaji hekima kubwa ya kuliendea na sisi kama tulivyosema tunaendelea kukuombea kwa Mungi ili hekima yote itumike katika kuweza kuleta muafaka wa jambo hili pasipo kugawanya au Wananchi kugawanyika na kutumika kama kitu cha kuchochea Wananchi kwa watu wenye maelengo yao mengine. Amesema Dkt.Shoo.

View attachment 2724358
Hii inaitwa setting the scores!.
Masikini TEC!.
P
 
mimi sio rc ila rais atumie busara hao watu hawawezi hata kidogo. asijifanye kufurukuta.
Hawawezi mara ngapi …acha kukariri

Hakuna mwenye hatimiliki wala kura ya veto …acheni kujikuza sana kuliko uhalisia

Kama mna nguvu hiyo mnayojifaragua Jakaya asingemaliza miaka 10

Hata Wafuasi wenu wanajua sometime mnatumika kupitishia agenda binafsi na ndio sababu kila kukicha Makanisa binafsi yamachipuka kila Mtaa

Mwisho kabisa nakujulisha maeneo mengi Nchini hivi sasa kuna Mgogoro wa Ardhi kati ya ya kanisa na wakazi wa maeneo hayo na wengi ni Waumini wa kanisa hilo hilo

sasa hivi hakuna kujificha kwny kanisa, Msikiti, Chama au sinagogi kupitisha agenda binafsi
 
Hawa KKKT wanachekew kisa hawajatoa waraka wakitoa nao mtaanza kuwaponda ila nijuavyo Mimi Ni kuwa hakuna kundi ambalo halina imani na samia kinacho pingwa ni baadhi ya vifungu ndani ya mkataba
 
Askofu Shoo kasema Viongozi wote waliomba wamuone Rais kuhusu Mkataba wa Bandari na Rais akawapokea na kuwasikiliza na kubwa zaid akaahidi kuyashughulikia maombi yao na hoja yao kuu ilikuwa ni kuboresha Mkataba kwa kuondoa au kuongeza mambo yenye manufaa kwa Nchi, na mchakato na mjadala unaendelea kwa makundi mengine

Ghafla linatokea Kundi linajiona kubwa kuliko Serikali na kuanza kuja na vitisho sijui wanasomea wafuasi wao Waraka sijui usomwe kwny Ibada, sijui hawataki kabisa uwekezaji n.k so what?

This time watapata lesson kuwa Nchi ni kubwa kuliko vikundi vya kidini, kisiasa na kijamii

Lengo la kwanza kum frustrate Rais na Serikali tayari wameshindwa na nini kusomewa waraka hata kama wakitaka kuwasaidia kusambaza nakala za Waraka tutafanya hivyo cha msingi kila mtu kila kikundi kijue Tanzania ni kubwa zaid yao

Hii nchi kweli safari bado ndefu sana. Kwahiyo ndugu wewe unaridhika kabisa na mkataba wa DPW Vs Tz?
Hakuna anayepinga uwekezaji TPA,watu wanapinga mkataba uliopo. Watu wengine mnawezaje kuuona uko sawa lakini?
 
Back
Top Bottom