JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,661
- 6,395
Baada ya uchunguzi kukamilika ilibainika kuwa, askari hao walikuwa wamefuta picha kutoka kwenye camera za Jeshi la Polisi walizokuwa wanatumia kupima mwendo kasi (speed rader) wa madereva waliokuwa wamekiuka sheria za usalama barabarani kwa maslahi yao binafsi.
Walishtakiwa kijeshi na wakapaatikana na hatia na Julai 8,2024 walifukuzwa kazi na kufutwa Jeshini.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Tanzania
Pia soma:Jeshi la Polisi latoa ufafanuzi juu ya tuhuma za baadhi ya Trafiki kuhusika na uchepushaji wa fedha