MLAU
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 4,726
- 3,358
Sidhani kama taarifa hii ni kweli Polisi hawawezi kuingia mitaani na kuanza kupiga watu viboko.Habari za jioni,
Baada ya tukio la kuuliwa askari wetu, jana nilishuhudia kwa macho yangu mwenyewe baadhi ya vijana wakiwa wamelazwa chini huku wakichapwa bakora. Leo hii watu hapa bungu wanachapwa ovyo mtaani. Hii sio haki kabisa.
Ili kupata suluhisho la tatizo hili polisi na vyombo vyetu vya usalama vitumie ueledi wa hali ya juu kabisa.
Kwanza Jeshi la Polisi hawana viboko kama kifaa cha kazi nadhani mtoa mada anataka kuleta uhasama zaidi kati ya Polisi na raia.
Naona na wachangiaji tunachangia tu bila kuangalia mtoa mada dhamira yake ni nini hasa.
Huko Bungu Viongozi wa jamii watasema kama ni kweli kuwa wanainchi wanapigwa ovyo na Polisi mitaani.