Askari Polisi (FFU) aliyebaka mwanafunzi Jela miaka 30

sisemi na kubaliana na mhali,fulakini mazingira na maelezo ya mbakwaji yanachanganya sana
Hakuna cha mazingira hapa!! sharti akabakwe humo lupango tutaagiza vibaka ishirini wamwoe kwa zamu. Kati yao watano ni waathirika. Hadi awashwe na maji washawasha kama yale aliyokuwa akimwagia raia
 
mimi mtu akinitumia ujumbe wa hivyo namdharau moja kwa moja .......hata kama ni jambo la maana nampuuzia by the way baba watoto wangu alikuwa anatabu hii ila nimemfunza mpaka akaelewa mambo ya kuniambia husinipikie badala ya usinipikie siyataki
Kwa hivyo mumeo ulikuwa unamdharau wakati anachanganya lugha!!?
 
Mkuu siku hizi imeshakua ni kama kawaida tu kwa mtu kutokutumia herufi "h" jaribu kuchunguza utaona maajabu aisee!! Kuna hii "Alafu" kama imeshakua ndio mbadala wa "Halafu" tena mijitu mingine mizima!! Inasikitisha sana aiseee,Kaazi kweli kweli..!!
Humu wengi villaza wanachanganya herufi kwenye r anaweka L panapohitaji l anaweka r, sijui tunaipeleka wapi elimu yetu.
 
Kwa hiyo mumeo ulikuwa unamdharau wakati anachanganya lugha!!?
pyee nilimkomalia mpaka kajia of course alikuwa ananitongoza

hutakuja mpenz hahahaha badala ya utakuja mpenzi ila baada ya kukubaliana ikabidi nigeuk mwalimu wake tukimaliza ku du tunafunzana..................................
 
Humu wengi villaza wanachanganya herufi kwenye r anaweka L panapohitaji l anaweka r, sijui tunaipeleka wapi elimu yetu.
Kuna comment moja niliona humu kama sikosei, mtu badala ya kuandika alilala yy kaandika 'arirara' duh maajabu humu
 
pyee nilimkomalia mpaka kajia of course alikuwa ananitongoza

hutakuja mpenz hahahaha badala ya utakuja mpenzi ila baada ya kukubaliana ikabidi nigeuk mwalimu wake tukimaliza ku du tunafunzana..................................
That interesting.......thamani ya mtu inaweza kushushwa kwa sababu ya uandishi mbovu
 
Humu wengi villaza wanachanganya herufi kwenye r anaweka L panapohitaji l anaweka r, sijui tunaipeleka wapi elimu yetu.
Mkuu mimi naona tuwakosoe na kuwarekebisha wote wanao iharibu hii lugha ya kiswahili na hasa kwenye matumizi sahihi ya herufi,unapoona kosa rekebisha,tusifumbie macho kabisa ama sivyo lugha fasaha ya Kiswahili itabaki kua ni historia tu,

Ninachojiuliza ni kua hivi hata huko mashuleni hua wana andika hivi hivi kama wanavyo andika humu?
 
FFU Jela Miaka 30 kwa Kubaka Mwanafunzi, Pia Atalipa Faini ya Milioni 15 na Viboko 12 Seebait.com 2016



ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Raphael Makongojo (25) aliyembaka aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Pia Makongojo amepewa adhabu kali, ikiwemo viboko 12 pamoja na kuamriwa kutoa faini ya Sh milioni 15 mara atakapomaliza kifungo chake.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Arusha ndani ya chumba cha faragha (chemba) ambako waandishi hawakuruhusiwa kusikiliza hukumu, lakini baadaye waliambiwa kwa sharti la hakimu wala waendesha mashtaka kutajwa majina yao kwa sababu kesi hiyo iliendeshwa faragha.

Awali kesi hiyo ilianza kwa mshitakiwa kusomewa maelezo yake ya awali akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Korogwe ambaye hivi sasa amemaliza masomo.

Awali askari huyo alishushwa pamoja na mahabusu wenzake mahakamani hapo, lakini kwa kuwa kesi inayomkabili ni ya ubakaji hivyo inasikilizwa ndani ya chumba cha faragha (chemba) ambako hakuna ruhusa kwa wanahabari kuandika habari hiyo hadi hapo hukumu itakapotolewa.

Kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria Namba 186 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 ya Mwenendo wa Makosa ya Kujamiiana ya Mwaka (1998) inayosema kuwa bila kujali masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusisha makosa ya kujamiiana, ushahidi au mashahidi watakaohusika hawaruhusiwi kutolewa kwenye chombo chochote cha habari.

Awali, mshitakiwa huyo kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka lake kwa hakimu (jina linahifadhiwa) ambako Wakili wa Serikali (jina linahifadhiwa) alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 16, mwaka huu katika eneo la Kwa Mrombo, FFU jijini Arusha.

Alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha Kifungu cha 130(1 na 2 a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 16.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mama mzazi wa mtoto huyo ambaye hakupenda kutaja jina lake, aliiomba serikali kuingilia kwa makini sheria inayohusu makosa ya ubakaji ili adhabu itakayotolewa kwa mbakaji iwe kifungo cha maisha badala ya hakimu au mahakama kutoa kifungo cha miaka 30.
 
Back
Top Bottom