Askari anapotumia silaha ovyo mtaani, anawakomaza na kuwapa ujasiri wananchi

Wapo wanaosema huyo kamanda apandishwe cheo kwa kupiga risasi hadharani. Wewe unawapinga hao?
 
Huyu ni Waziri mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe Adam Malima Kighoma akisukumwa na kutishiwa bunduki na mmoja wa askari polisi. Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika.

#My_take
Vitendo hivi vya kioonevu vilianza kwa wananchi wa kawaida ikaonekana ni sawa na hakuna aliyepiga kelele. Vikahamia kwa viongozi wa upinzani ikaonekana pia ni sawa. Sasa vimehamia kwa viongozi wastaafu na wale wanaokinzana na serikali katika baadhi ya mambo.

Haya mambo sio ya bahati mbaya. Ni mambo ambayo yanalelewa na kubarikiwa na viongozi wa serikali hii ya awamu ya tano. Ingekuwa mawazo yangu ni tofauti, tungeona serikali hii ikichukuwa hatua dhidi ya wale askari au maafisa usalama wanaofanya vitendo hivi. Hii peke yake inaonekana dhahiri serikali na watawala bado hawajawa na utayari wa kukataa vitendo hivi vinavyofanywa na baadhi ya watu kutoka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Watu hawa wanafanya vitendo hivi wakijua kabisa Serikali au viongozi wao wa juu hawezi kuwachukulia hatua.

Nimeona video husika. Ukisikiliza maneno ya askari aliyekuwa anafanya upuuzi ule ikiwa ni pamoja na kupiga risasi hewani, utaskia akisema kwa kurudia rudia "kwanini hamheshimu serikali?''. Hii ilikuwa ni defensive mechanism dhidi ya kile alichokuwa anakifanya kwa Malima. Anaamini kabisa kwa kusema maneno hayo, atabaki salama. Hii ni akili ya ajabu sana. Jeshi la polisi moja ya wajibu wake ni kutekeleza sheria (to enforce laws), hivyo kama Malima alikuwa na kosa, alipaswa kukamatwa na kupelekwa polisi ili afunguliwe mashitaka na sio kusukumwa, kutishwa kwa maneno na risasi za moto.

Ikiwa vigogo hawa wanafanyiwa hivyo hadharani mbele ya watu mchana kweupe, vipi kwa raia wa kawaida, walala hoi wala wasiofahamika? Wanafanyiwa nini wawapo huko gizani au uchochoroni? Bila shaka ni ngumu sana kuamini kama raia wa taifa hili wako salama.

Wito wangu kwa viongozi wa nchi yetu hasa mawaziri msijisahau sana. Hakikisheni katika kutekeleza majukumu yenu hambariki uovu. Kataeni na pigeni kelele pale inapobidi. Hizo nafasi zenu sio za kudumu kama utanzania wenu. Hii ifanywe pia na sisi wananchi wote wa Tanzania. Tusikubali vitendo hivi kutamalaki katika taifa letu. Tuvikatae bila kujali anayevifanya au kuvibariki ni nani?. Tukifanya hivyo tutakuwa salama na tutajenga taifa la haki na usawa.

____________
Sumu
 
Mimi nimeipenda hiyo kwa kuwa inadhihirisha unabii wa yule dogo lema kule bungeni. Toka sasa nitaanza kumwita the dogo prophet. Maana alisema walianza kwao lakini mwisho watawaingilia na wale wa upande wa pili. Ama kweli kama jinsi wema unavyoumba na ubaya Nao unaumba
 
Huyu Malima mjinga Sana risasi zinapigwa ndio anazidi kusogea anafikri kuwa risasi inamjua kuwa alishawahi kuwa waziri,kwanza ashukuru askari aliyeshika silaha ni askari mwenye busara,askari anapo piga risasi hewani maana yake anakutishia ukimbiye au usalimu amri ukamatwe kwa Amani.

Lakini Kama utajifanya nunda wa kuto kuogopa risasi,askari anapiga risasi hewani wewe unazidi kumsogelea hiyo ni sababu tosha yakumfanya askari akugonge za kichwa kwa kuwa hiyo ni sababu ya msingi ya kuonekana kuwa ulikuwa unatishia maisha ya askari.

Sababu za kuanza kujadili uhalali wa askari kukupa za kichwa zitakuja baadae wakati ukiwa umefunikwa sanda.

We jamaa inabidi wakuchunguze akili haupo timamu
 
Kwanza huyo dogo keshadharauliwa na wenzake kwa kuitwa poti wakati lafudhi yake ni ya kimeru, kilichomtoa kukukakara kwenye gari ni nini?

Halafu kafyatua risasi bust inamaana risasi alishamaliza hakujua malima ni mzoefu ndio maana alijua ameshamaliza risasi ndio kwanza akazidi kumsogelea.

Huyu dogo achunguzwe myenendo yake huko jeshini inawezekana haziko sawa kichwani.
 
Ndg zangu,

Hii tabia ya wananchi kutishiwa silaha ovyoovyo,haikubaliki kabisa. Siku hizi askari wanatoa silaha ovyo na kutishia watu mtaani bila uwepo wa hali ya hatari.Jeuri hiyo nani anawapa? Wananchi wakishazizoea bunduki nn kitakachofuata?

Mh Nape alitishiwa bastola bila sababu ya msingi.Jana Adam Malima nae hivyohivyo Askari amemfyatulia risasi mbili za SMG.Hii siyo sawa kabisa.

Sasaiv mara Panya road,mara Kibiti, mara Mkuranga.
Jana nimeshuhudia ukomavu wa watu kuhusu silaha. SMG ilipigwa,watu wakasogea kidogo na kurudi tena,na Adam Malima hakustuka kabisa.Nn maana yake?View attachment 509813View attachment 509815View attachment 509817
Ndio watakubari sheria zibadilishwe wote tutafute haki cortini sio kuonewa na police,
 
Jamaa mmoja alisikika akisema ah ah huna mamlaka hiyo huna mamlaka hiyo!!! Ina maana askari anapewa silaha kwa ajili yakuuzia nayo sura tu
 
Ndg zangu,

Hii tabia ya wananchi kutishiwa silaha ovyoovyo,haikubaliki kabisa. Siku hizi askari wanatoa silaha ovyo na kutishia watu mtaani bila uwepo wa hali ya hatari.Jeuri hiyo nani anawapa? Wananchi wakishazizoea bunduki nn kitakachofuata?

Mh Nape alitishiwa bastola bila sababu ya msingi.Jana Adam Malima nae hivyohivyo Askari amemfyatulia risasi mbili za SMG.Hii siyo sawa kabisa.

Sasaiv mara Panya road,mara Kibiti, mara Mkuranga.
Jana nimeshuhudia ukomavu wa watu kuhusu silaha. SMG ilipigwa,watu wakasogea kidogo na kurudi tena,na Adam Malima hakustuka kabisa.Nn maana yake?View attachment 509813View attachment 509815View attachment 509817
Yaani hapo unajidanganya na pia unadanganya umma! Kimsingi Risasi haizoweleki ndg. Kwani haina macho! We wapotoshe wasijua ila siku watajua.
 
Yaani hapo unajidanganya na pia unadanganya umma! Kimsingi Risasi haizoweleki ndg. Kwani haina macho! We wapotoshe wasijua ila siku watajua.
Wewe ndo unadanganya umma upo nchi ya Amani ndomana unasema risasi haizoeleki ila waulize wasomali ambao hata bomu likipigwa anaendelea na shughuli zake
 
Mungu tunaomba amani na utulivu vitawale katika nchi uliyotupa ya Tanzania
 
Wiki iliyopita nilikuwa sehemu karibu na uwanja wa mpira,,,kuna washkaji huwa wanachezaga pool table hapo,,, basi bwana walikuja police hata walipotokea, ,,, wakapiga risasi hewani utadhani wameona jambazi,,,,ikasababisha hadi mtafaruku mkubwa, ,,,,,yaan sasaivi izo risasi na mabomu ya machozi imekuwa kama mazoea,,,hata bar ikifika saa sita tu mnaondolewa na mabomu ya machozi sehemu zingine,,,,,kuna bar moja ipo karibu na kambi ya Jeshi kule bahari beach sikuizi ndio hawaendi nasikia, baada yakupewa dicpline na wazee wa kazi,,,,,sisahau siku moja kulizuka mtafaruku mkubwa pale
 
Back
Top Bottom