All is possible, angalau wana credit card, sisis huku jwe?Haya si maneno yangu. No maneno ya 👇👇👇
Sio kujipa faraja mkuu. Kuna ukweli ndani yake.Mada za kujipa faraja….
Unaishi Marekani. Kwenye akaunti yako ya benki hauna dola elfu tano.Kuwa na akaunti ya benki sio kipimo cha utajiri au umaskini. Utajiri au umaskini unapimwa kwa kutumia pato la taifa la mtu mmoja mmoja kwa mwaka." Hili ni jambo la msingi sana kuelewa katika mjadala wowote wa maendeleo ya kiuchumi. Katika ulimwengu wa leo, watu wengi wanaamini kuwa mtu kuwa na akaunti ya benki ni kiashiria cha kwamba yuko vizuri kiuchumi, lakini ukweli ni kwamba hiyo si sahihi. Akaunti ya benki ni tu njia ya kupata au kutumia fedha, lakini haina uhusiano wa moja kwa moja na kiasi cha kipato anachopata mtu kwa mwaka.
Pato la taifa la mtu mmoja mmoja (GDP per capita) ndilo kipimo rasmi kinachotumika kimataifa kupima kiwango cha maendeleo au hali ya kiuchumi ya mtu mmoja ndani ya taifa lake. Kwa mfano, nchini Marekani, pato la mtu mmoja ni takribani TZS milioni 222 kwa mwaka, nchini China ni TZS milioni 32, na nchini Tanzania ni takribani TZS milioni 3 kwa mwaka. Tofauti hii inaonesha kuwa hata kama Mtanzania ana akaunti ya benki, kipato chake kwa mwaka ni cha chini sana ukilinganisha na raia wa Marekani au China.
Akaunti ya benki inaashiria "financial inclusion" au ushirikishwaji wa kifedha, yaani mtu ameunganishwa na mfumo rasmi wa kifedha. Hii ni hatua muhimu kwa maendeleo ya taifa kwa sababu inaongeza fursa za upatikanaji wa huduma kama mikopo, bima, malipo ya kiserikali, na njia za kuhifadhi akiba kwa usalama. Lakini kuwa na akaunti hiyo hakumaanishi kuwa mtu huyo ana kipato kikubwa au ni tajiri – anaweza kuwa na akaunti isiyo na salio kwa muda mrefu, jambo ambalo halibadilishi hali yake halisi ya kiuchumi.
Kuhusu madai kwamba “asilimia 70 ya Wamarekani hawana dola 5,000 kwenye akaunti zao,” kuna ukweli fulani ndani yake lakini pia kuna hitaji la kulieleza kwa ufasaha zaidi. Tafiti mbalimbali, ikiwemo ya Federal Reserve, zinaonesha kuwa idadi kubwa ya Wamarekani (takribani 60% hadi 70%) hawana akiba ya dharura ya kiasi hicho cha fedha. Hii haimaanishi kuwa hawana kipato kabisa, bali huashiria jinsi mfumo wa maisha ya Kimarekani unavyoendeshwa kwa mikopo na malipo ya kila mwezi (credit cards, mortgages, loans). Watu hao wanaweza kulipa gharama zao za kila siku, lakini hawana akiba ya kutosha kwa ajili ya dharura au uwekezaji mkubwa.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Sensa ya Marekani (U.S. Census Bureau), watu wanaoishi rasmi chini ya kiwango cha umaskini ni asilimia 11.1 tu ya Wamarekani (sawa na watu milioni 36.8), na kwa kutumia kipimo cha ziada cha gharama za maisha (Supplemental Poverty Measure), kiwango hufikia asilimia 12.9. Hii ina maana kuwa madai ya kuwa asilimia 70 ya Wamarekani ni masikini si sahihi kwa mujibu wa takwimu rasmi.
Wazee wa kujirusha hao!Haya si maneno yangu. No maneno ya 👇👇👇
Kati ya watu milioni 340, ni wangapi kwenye hiyo video huko Maryland uliona wanaiba hayo matairi ya gari?Sio kujipa faraja mkuu. Kuna ukweli ndani yake.
Marekani mpaka wizi wa power window wapo.
Jana kuna video ime trend ya jamaa wanaiba matairi ya gari Maryland.
Video ime trend sana inakaribiana na na story ya Karmelo vs Austin Metcalf
Ni fedheha kuwa sana kwa taifa lililo endelea kiuchumi kama Marekani kuwa na raia ambao wanaweza kuiba power windows au matairi ya gari.Kati ya watu milioni 340, ni wangapi kwenye hiyo video huko Maryland uliona wanaiba hayo matairi ya gari?
Hao wezi wa power windows ni wangapi? Milioni 200?
Ila kweli lakini. Hata Tupac aliimba sana kuhusu ugumu wa maisha ya Marekani.Ni kweli kabisa Marekani Mambo magumu sana wenye HeLa ni wachache sana ndio maana Jay Z aliimba " Hard Knock Life"
Nguvu uitumiayo kujipa faraja dhidi ya Marekani, lazima kuna kitu nyuma yake!Ni fedheha kuwa sana kwa taifa lililo endelea kiuchumi kama Marekani kuwa na raia ambao wanaweza kuiba power windows au matairi ya gari.
Mambo kama hayo huwezi kuyaona kwenye nchi kama Sweden , Norway au Denmark.
Ni Mambo ambayo utategemea kuyakuta kwenye nchi masikini
Between me and you, the one who is obsessed with USA is you.Nguvu uitumiayo kujipa faraja dhidi ya Marekani, lazima kuna kitu nyuma yake!
Huenda ukawa mhanga wa kunyimwa viza, kurudishwa, au wivu flani…..