Asante sana Rais Samia kwa mabadiliko haya madogo ya uongozi katika Serikali Kuu, watanzania wote wamekupenda zaidi, wanakushukuru na kukuamini zaidi

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
20,482
22,419
Rais Samia Suluhu Hassan, Rais na kipenzi cha waTanzania uongozini.

Mwenyezi Mungu azidi kukujaalia afya njema, bidii, ubunifu na nguvu tele katika kuongoza nchi yetu Tanzania..

Hamasa na ushawishi wako kwa vitendo baada ya kufanya mageuzi na mabadiliko kidogo katika uongozi wa Serikali yako kuu, waTanzania kwa mamilioni yao, wamekupongeza sana, na kukushukuru mno, kwani dhamira na nia yako njema ya kuwaletea wanainchi maendeleo imedhihirika bayana...

Hamasa ya kukupenda na kukuamini imeongezea mara dufu matarajio yao kwao ni makubwa mno kisiasa kijamii na kiuchumi..

Inafahamika, inaaminika na inaonekana tena mchana kweupeee, kila pembe ya nchi Dr.Samia Suluhu Hassan una pendwa na unakubalika bila kificho kwa maneno na matendo yako, katika kazi za maendeleo..

Hakiwezekani mtu aje aseme hadharani, ati hata kama hamumpendi huyo ndio Rais wenu, hiyo ni dharau kubwa sana japo kwa hekima na busara ulichelewa kuchukua hatu.

Lakini pia, Mh. Rais usiku na mchana uko kazini kuhakikisha taasisi zetu mathalani zinazohusu kusimamia chaguzi zinakua imara na zina aminika kwa wananchi, na kwamba hata chaguzi zetu zote zinaaminika zinakua huru, wazi na za haki na waTanzania wanahamasika kupiga kura.

Halafu mtu mwingine anakuja kudhoofisha jitihada hizi kubwa kirahisi tu, za mh.Rais kurejesha imani za waTanzania kwenye taasisi zao.. eti bao la mkono πŸ’

Hapana, Hii si sawa na haipendezi. Kuna aina za matani tunapokua kazini ni hujuma. na dhamira yake ni kubomoa au kuidhoofisha kazi muhimu za Kuwaleta waTanzania pamoja na kuamininiana. madaraka ya kulevya ni ulevi mbaya sanaπŸ’

waTanzania wako pamoja nawe mh.Rais Dr.Samia Suluhu Hassan.
Mungu Ibariki Tanzania

Pia soma
- Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Mna roho ngumu kweli, leo mwenzio Lucas kaamua alale may be amekata tamaa, we mbona huchoki? Teuzi zimeisha mzee
 
Nyuzi kama hz ndizo hufanya nijihisi sikuhesabiwa kwenye sensa.

Watanzania "WOTE"
 
kwahiyo kila jukwaa na hoja yake umebeba mihemko na makasiriko 🀣

ndio observation yako imeisha hapo dah..

utumwa mwingine bana ni mzigo mzito wenye mateso sana πŸ’
Wewe hata huyo Boss wako afanye madudu ya aina gani! Aidha utanyamaza kimya ili yapite, au usifie! Ila haitakuja itokee ukamkosoa kwa chochote.
 
january kawa december
maraboti nape kakamilisha msemo wa kupanda na kushuka.
View attachment 3048625
hayo si maneno tu ya kwenye kanga πŸ’
nadhani nape na January ni miongoni mwa vijana wenye bahati sana na bilashaka wanajivunia kulitumikia taifa lao tena kwenye Serikali kuu wakiwa na umri wa ujana sana....

political upsidedown na mistakes katika ujana ni opportunity muhimu zaidi kwa wao kujisahihisha kama kuna dosari au kasori, kujiimarisha na hatimae kuja na comeback nzito sana kwenye siasa za kitaifa...


Ni matumaini yangu hivi sasa watakua backbencher makini lakini wakifanya kazi za chama vizuri sana kuelekea Uchaguzi mkuu ujaoπŸ’
 
Wananchi wana hasira ya 2019/2020 halafu waziri mmoja anakumbusha tena lwa kebehi anayoiita utani,hakumtendea haki Rais na 4R zake. Kilichotokea ni sahihi na wengine wemye mawazo ya wizi wa kura. awaonye,vyombo vya dola navyo vipewe maelezo,ili atakayeshinda ashinde atakayeshindwa ashindwe. Mungu yupo ni wa wote.
 
Mna roho ngumu kweli, leo mwenzio Lucas kaamua alale may be amekata tamaa, we mbona huchoki? Teuzi zimeisha mzee
Kwan kusema ukweli kuna chosha gentleman?πŸ’

mimi niteuliwe mara ngapi kwa mfano?
nilisimama kuvunja siku kama tatu zilizopita nilikua na ziara ya kamati ya siasa ya mkoa kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM,

asubuh hii nimerudi jimboni niko shambani navuna, alhamisi na ijumaa nina ziara katika kata kadha jimboni, nikimaliza narudi shamba...

sasa ni kukusanya chakula cha mifugo na kuhifadhi panapostahili,
halafu mang'ombe yamenenepeana hatari aise πŸ’
 
Umekuja Tena kivingine wewe chawa!! Juzi kati hapa ulikuwa unawapigia debe hao watenguliwa
 
Nyuzi kama hz ndizo hufanya nijihisi sikuhesabiwa kwenye sensa.

Watanzania "WOTE"
ulifuatilia koments za wangwana kwa umakini, ukiona kuna mihememko ndani yake ujue huyo hana hata kitambulisho cha kupigia kura na pia alipuuzia zoezi la kuhesabiwa wakati wa sensa πŸ’

hata hivyo,
kwa ujumla wake Dr.Samia Suluhu Hassan ana upiga mwingi halafu sasa ni right, left and center, Lazima utampenda tu πŸ’
 
Hivi kwa nini mnapenda kuwaongelea watu,talk on your own behalf bwana.Kama kakupa kula au hajali unapowaibia Watanania, usidhani sisi wote tunapenda uovu huo, we don't,ni kwamba tu hatuna la kufanya.Mimi on my part ningetamani mafisadi yote ya-face the firing squad,ili iwe fundisho kwa wengine.Nachukia sana watu wanaofanya mambo yanayofanya watu wengine wakose haki zao,and Samia is one of them.
 
Wewe hata huyo Boss wako afanye madudu ya aina gani! Aidha utanyamaza kimya ili yapite, au usifie! Ila haitakuja itokee ukamkosoa kwa chochote.
acha uposhaji gentleman,
hiyo ni uongo ya mchana kweupe aise...

mimi ni miongoni mwa wakosoaji wabishi mno kwa mh.Rais kipenzi cha waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan, pamoja na kwamba ni miongoni mwa waandamizi wake...

sema tu hunifuatilii sana, ni muhimu ukafolow account yangu ili upate elimu, uelewa na ufahamu zaidi juu ya namna rais anafaa kukosolewa na akayachukua yale muhimu tunayo mshauri na kuyafanyia kazi...

tummemkosoa sana namna ya kuongeza mapato ya nchi kwa kodi, ameskia ukosowaji wetu, amechukua hatua na kwa muda usiokua mrefu utabaini TRA itaongeza walipakodi kutoka million 2 hadi million 20 tutkapofanya Uchaguzi 2025....

so,
si kweli kwamba mimi simkosoi Rais na siwakosoi waandamizi wenzangu kwenye chama na Serikali, nafanya hivyo kwa bidii sana bila aibu wala haya kwa maslahi mapana ya waTanzania wote πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…