Asante sana Kikwete kwa kutupatia Rais Magufuli, Watanzania tuna raha sana

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
Kiukweli nimeshindwa kujizuia kutoa shukrani za dhati kwa Jakaya Kikwete kwa uzalendo wake katika hii nchi. Kikwete wewe ni jabali, mwanajeshi wa ukweli bila magwanda.Watu wanasema huna akili na wanasahau wewe umelamba digrii UDSM kipindi hakuna google wala wikipedia.

Tena digrii ya nguvu ya uchumi sio ya sociology wala PSPA, huku wao wanaokuponda wamesoma miaka ya google ila UDSM tu wameshindwa kusoma kwa kukosa vigezo wameishia vyuo ulivyowaletea vya msaada.

Mtu amesoma Sauti au Jordan tena digrii ya ualimu, sociology au development studies. Halafu linaponda eti JK hana akili.Lenyewe UDSM tu limeshindwa kufika hii internet era.

Umefanya mengi sana makubwa hii nchi. Shule za kata leo house girl tu kumpata shida. Kila mtoto anafika sekondari.

UDOM ambayo ni jengo la CCM chimwaga ndio lililoanzisha chuo leo watu walioshindwa kufika UDSM wanapata nafasi ya kusoma nao chuo kikuu ila kwa kukosa shukrani wanakutukana.

Mabasi ya mwendokasi ni uroda. Asante sana Kikwete kuna mijinga inakuponda hujafanya kitu huku inapanga foleni kila siku na kadi zao za malipo kusubiri mabasi ya mwendo kasi. Kikwete unawacheka tu ukiwa Msoga na majuu kwenye trip zako zile.

Muhimbili heart institute, barabara leo Mwanza tunaenda siku moja tu full lami na bus luxury kama Dar lux, Green star, na mengineyo kiyoyozi from Dar to Mwanza kisa uzuri wa bara bara ulizojenga. Kuna wajinga wanasema hujafanya kitu huku inacharge simu zao kwenye hizo bus ikiwa safarini ( wanafikiri bila uzuri wa bara bara ni mtu gani angeweka ma bus mazuri kama hayo?)

Daraja la Kigamboni, Terminal 3 new airport DSM. Kitu JK Nyerere kama Dubai vile.

Mwisho kabisa kumpa nchi Rais Magufuli jembe ni bonge la zawadi kwa watanzania wote wapenda maendeleo ya nchi yao.

Mafisadi wanahaha kila siku wanadata kwa kasi ya Rais Magufuli na nina amini Tanzania mpya imeshazaliwa.

Ila Kikwete umetisha sana hasa style yako ya majina mfukoni na kumtanguliza Membe kama fake choice na kuweza kuwafool wana CCM 3000.

Barcelona walitawala mpira kwa style ya fake no 9 na Kikwete umeweza mpitisha Rais Magufuli wa style ya fake no 9 pia kwenye siasa.

Yaani unaudanganya uma kwa kumtanguliza mtu asiyefaa ili mabeki wamkabe asiwafunge kumbe mfungaji yupo nyuma. Anawafunga kiulaini tu.

CCM Oyeee..
====

Mdau chige yeye ameandika > Ahsante JK kwa kutuachia Nyapara;

Moja ya mambo ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakimlaani sana Mjomba, yaani Mzee wa Msoga ni kutuachia "Huyu Jamaa!" Kwamba, eti Huyu Jamaa ameshafeli pamoja na tambo zao zote!

Hata hivyo, Waswahili husema "Mnyonge Mnyongeni Haki Yake Mpeni!"

Tuwe wakweli! Hivi ukiangalia timu ya JK kwa muda wote aliokuwa mjengoni; ni nani alistahili kuwa Nyapara Bora kuliko wenzake kama sio Sizonje?!

Kama yupo, nitajieni!

Inaonekana Mjomba hakuwa na shida ya kutuachia Rais! Alichotaka yeye ni kutuachia Nyapara... Nyapara Hodari! Nyapara asiyechoka kusimamia wafungwa tangia majogoo hadi Machweo!

Mchukie utakavyo lakini Huyu Jamaa ni Nyapara Hodari! Mzee wa Msoga alitaka kutuachia Nyapara na sio Rais! Alitaka kutuachia Nyapara wa kusimamia yale ambayo aliyaanzisha!

Aliacha lile daraja la kuvuka bahari! Mjomba alitaka Nyapara Hodari wa kuhakikisha daraja linakamilika!

Mzee wa Msoga aliacha ule mradi wa mabasi yaendayo fujo haujakamilika vizuri!

Aliacha ule mradi wa hospitali Dada wa hospitali kuu nchini! Aliacha ule mradi pale Njia Panda ya kwenda Ulaya! Aliacha ule mradi wa barabara ya tukutuku inayoishia Kigoma!

Niendelee?! Kuna ule mradi wa stendi ya meli pale njia panda iliyokuwa inatumika kupitishia watumwa kwenda kwa Seyyid Said!

Hiyo ni baadhi tu! Daktari wa Bwagamoyo alifahamu kabisa hiyo miradi ni mikubwa! Ni miradi inayohitaji Nyapara mahiri, machachari, jasiri na jeuri!

Kama kubuni mradi kunahitaji akili basi akili ilishatumika! Ambacho kilibaki ni kuhakikisha anapatikana Nyapara Hodari wa kusimamia hiyo miradi! Nyapara anayeogopeka! Nyapara mpiga mikwara! Nyapara mwenye silika ya kufokafoka!

Mzee wa Msoga kapiiiga hesaàabu; kaona hapa hakuna cha shemeji wala nini bali huyu huyu!!

But all in all, hivi Mzee wa Msoga ni kwanini ulimdanganya Huyu Jamaa kwamba unamwachia urais wakati ulifahamu kabisa unamwachia unyapara? Unyapara wa kusimamia yale uliyoanzisha?!

Matokeo yake, mwenzako kila akijaribu kujilisha shavu, wabaya wake oh, "Hakuna jipya hapo, hilo shavu ni la shemeji yake na Joka la Mdimu"... aaaaaaargh; Mungu anakuona Mzee wa Msoga! Unaona sasa, hadi anafikia kuzinduwa vilivyozinduliwa manake kila anapogusa; anakuta ulishapita zamani!

Lazima uambiwe ukweli bhana; it's not fair! Mambo ya kukabidhiana unyapara badala ya urais sio kabisa!
 
Naona baada ya kusikia msako wa wasio na kazi umeamua kujiajiri kwa kupost sifa kwa JK jiandae kuondoka hamna namna
 
ha ha ha nawe endelea kumsifia kingunge, sumaye, lowassa na dj mbowe...

stooo ya mabadiliko imeajiri walinzi vibaka.. muda utaongea tu


Naona baada ya kusikia msako wa wasio na kazi umeamua kujiajiri kwa kupost sifa kwa JK jiandae kuondoka hamna namna
 
Ni sahihi kabisa, Baba yetu Kikwete kafanya mambo mengi mazuri katika kipindi chake cha uongozi(urais). Ni dhambi kubwa kusema rais Kikwete hajafanya lolote. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Baba
Ni sahihi kabisa, Baba yetu Kikwete kafanya mambo mengi mazuri katika kipindi chake cha uongozi(urais). Ni dhambi kubwa kusema rais Kikwete hajafanya lolote. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Ni baba yako na sio yetu.
 
Nami nampongeza sana JK kwa kutupatia Magufuli. Nimemkubali Ngosha kwa jinsi anavyotunyoosha bila hata kututazama usoni
 
Baba
Ni baba yako na sio yetu.

ni baba yetu watanzania wote wazalendo tunaochukia mafisadi kwa vitendo..

hata kama ukiwa rafiki yangu au ndugu yangu ukiwa fisadi nakukata tu... huyo ndio jk
 
hakuna rais aliyeijenga hii nchi kuliko kikwete

Ni sahihi kabisa, Baba yetu Kikwete kafanya mambo mengi mazuri katika kipindi chake cha uongozi(urais). Ni dhambi kubwa kusema rais Kikwete hajafanya lolote. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…