Asante Mungu nimelishinda tena hili jaribu

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
592
2,216
Iko hivi, kuna siku kuna mteja kijana alikuja hapa ofisini kwangu nimtengenezee simu kama miezi mitano imepita hivi, ilikuwa ni smart ya kubadili kioo. Sasa nikamtengenea akarudi kuchukua kesho yake.

Akaondoka baada ya wiki moja akarudi na ile simu ikiwa imepoa battery hivo nikampa simu moja ya batani akaenda nayo ili asikose mawasiliano, aliporudi kuchukua simu yake akaniambia nimuuzie na hiyo ya batani, nikamwambia anipe 8000.

Akasema ana 4000 hivyo nimdai, kusema ukweli moyo ulisita maana simjui na ndio ilikuwa mara ya pili anakuja ofisini kwangu pia hata sijui anaishi wapi.

Kwa kawaida yangu nikaulazimisha moyo ukubali kuchukua hiyo hela nusu nikampatia simu Baada ya siku tatu hivi akaniletea ile 4000 nikaipokea.

Mimi huu mkoa ninaoishi kuna mtoto wa dada yangu wa kike anaishi huku huku ila wilaya tofauti, basi bhana huyo mtoto wa dada yangu amewahi kuja mara mbili kunisalimia na anarudi zake huko anakofanya kazi.

Basi kuna wakati akija kunisalimia aliniambia ana mchumba huku ninakoishi na kuna siku alikuja akakaa mpaka usiku ukaingia hivyo nilipotoka kazini akaniomba nimsindikize mpaka huko kwa mchumba wake kwani mchumba au bwana wake alikuwa amesafiri hivyo aliona akalale tu huko.

Nikamsindikiza mpaka nikamfikisha nikarudi zangu. Sasa jana amekuja akiwa na simu imekataa kuwaka battery imepoa, nikaichukua ili nikalibust ila likawa limelalaa zima.

Niliporudi nyumbani mchana wa leo nikamkuta hayupo ameenda kwa mchmba wake, jioni mida ya saa 11 akawa amekuja na huyo mchumba wake kumtambulisha kwangu.

Kumtazama ni yule jamaa niliyemuuzia simu na kunipa hela nusu! Nikabaki nashangaa, ila yeye hana hata wasiwasi maana kumbe alielekezwa siku nyingi tu na huyu mjomba wangu kwamba mimi ni fundi simu ndio maana akaniletea.

Na ile simu huyu mjomba wangu amempa tu mke wangu atengeneze atumie, na baada ya kuangalia ile simu nikagundua ni ile ile nimewahi itengeneza.

Sasa kilichonifanya niandike huu uzi ni;

Je, siku ile ningekataa kumpa simu kisa 4000 hii aibu ningepeleka wapi? Kiumri mimi na yeye tunalingana tu labda nimemzidi kidogo tu.

Nawasilisha.
 
Dah😂😂😂😂 hivi unayajua majaribu


Hebu pata picha wewe ni muhasibu wa kanisa

Una mkopo na nyumba yako ishapigwa machata Inauzwa!!
Kibaya zaidi wapendwa wenzio wanajua jambo hili

Afu kwa bahati mbayaa sadaka zikaibiwa

Ungetumia namna gani kuwaaminisha watu kua wew hujaiba!

Hayo ndio majaribu
Hayo yako ni majawabu
 
Back
Top Bottom