ARUSHA: Watu wawili wafariki kwa kuchomwa moto bila nyumba kuungua

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,015
4,982
Watu wawili wamefariki dunia Leo hii asubuhi katika nyumba ya marehemu bilionea Msuya baada ya moja ya chumba walichokuwa kuungua Moto huku mwanaume hiyo akiwa amefungwa kamba mikononi.

Tayari polisi wamechukua miili sasa hivi baada ya kuchukua maelezo kutoka kwa wapangaji wengine.

Hili tukio limetokea katika moja ya nyumba yake iliyopo Sakina Arusha.

----------
Eng Mose, said

Watu 2 wa jinsia ya kike na Kiume ambao bado majina yao hayajatambulika wamekutwa wamepoteza maisha katika Kitongoji cha Elkiurei Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru kwa kile kinachosemekana kuwa ni ajali ya moto.

Akithibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji hicho Bwana Enesphori Chami amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza kwasababu wamekuta marehemu hao katika mazingira ya ya kujiuliza maswali mengi kwa kuwa mwanaume alikuwa amefungwa kamba mikononi jambo lonaloleta utata kuelewa nini kilikuwa kinaendelea.

Bwana Chamia amesema marehemu hao walikuwa mwanaume na mwanamke wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kata ya 30 na 35 lakini kinachoshangaza wameungua wao pamoja na Godoro jambo ambalo linatia wasiwasi majirani waliokuwa eneo hilo.

Naye shuhuda aliyejionea tukio hilo amesema kuwa walilazimika kuvunja mlango kwa kuwa ulikuwa umefungwa kwa ndani lakini dirisha lilikuwa limefunguliwa jambo ambalo hawajaelewa kwasababu marehemu hao mwanaume alikuwa amefungwa kamba.

Shuhuda huyo amesema kuwa Mwanamke huyo anajulikana kwasababu wako naye siku zote lakini mwanaume anaonekana kuwa ni mgeni kwasababu hawajawahi kumuona na mwanamke alikuwa anaishi peke yake.

Naye Diwani wa kata ya Kiranyi Bwan John Seneu amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza kwasababu kama ni nyumba kuungua ingeteketea yote lakini kilichoungua ni godoro peke yake kitu kinachoendelea kuwafanya wananchi kuwa na maswali mengi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa makini Na matukio kama haya na kutambua wageni wanaowatembeleakatika maeneo yao

Pamoja na hayo jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzi cha tukio hilo la kusikitisha.
Marehemu Enzi za uhai wake
 
Binadamu tumekuwa wanyama sana. Hivi watu hawajiulizi maisha ya mtu kuishi duniani ni mafupi sana. Hakuna haja ya kumfanyia mwenzako visa kama vile utaishi milele.

Pili hakuna atakayeondoka na chochote hapa duniani. Tutaviacha vyote na kuondoka watupu kabisa.

Tuifanye dunia kuwa sehemu salama basi ya kuishi angalau kwa muda huu mfupi anaotujalia kukaa hapa duniani.
 
Hii kesi ya MSUYA kwa watu wa arusha hata mtaani ukienda utajua ni kiais gani nchi hii hakuna haki, Muhisika mkuu yupo mjini naranda randa na waliobakia kuuwana na kupambana ni vibaraka tu.

hakika WANAWAKE NI WATU HATARI SANA!
Usemayo n kwel yule maka anaendelea kuteketeza watu...yan mwanamke anaua familia ya mume na bado anadunda ....halafu unasema una utawala bora? Nnachojua rais wa nchi anajua ukweli ana uwezo kusisitiza haki itendeke
 
Hivi kuna nn juu ya matukio ya visa vya familia na wahusika wakuu wa haya mambo ya msuya... Anaejua vizuri atufahamishe huyo bilionea msuya aliuawa vipi na kwann mke wa marehem ahusishwe na tukio la kifo cha Dada wa marehem pia?
 
Hao wali
Hivi kuna nn juu ya matukio ya visa vya familia na wahusika wakuu wa haya mambo ya msuya... Anaejua vizuri atufahamishe huyo bilionea msuya aliuawa vipi na kwann mke wa marehem ahusishwe na tukio la kifo cha Dada wa marehem pia?
ofariki Ni wapangaji mkuu katika nyumba ya bilionea msuya
 
Unless uipinge habari yenyewe lakini kwa mujibu wa habari, mwanaume alikutwa amefungwa kamba mikononi!!

Sasa kama ni kweli amekutwa amefungwa kamba mikononi, unataka kusema hiyo kamba alijifunga mwenyewe?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…