Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,181
- 5,553
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia Mtumishi (Mhasibu) wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu huku likimsaka mwingine kwa tuhuma kuhujumu mapato ya Serikali kwa kutoa risiti bandia za EFD.
Kulingana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Juma Hokororo amesema watumishi hao wanatuhumiwa kuunda mfumo mwingine unaotoa risiti ambazo zinafanana na za Halmashauri ambazo huchepusha mapato.
Aidha ameongeza kuwa Licha ya Halmashuri kufikia asilimia zaidi ya mia moja ya makadirio ya mapato wanayopaswa kukusanywa, huenda wangekusanya zaidi kama mapungufu hayo yasingekuwepo.