Arusha: Rais Samia ashiriki Misa Maalum ya Miaka 40 ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine. Atoa pole kwa familia za wanafunzi waliofariki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,540
13,214
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Misa Maalum ya miaka 40 ya Kumbukumbu ya Miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Juu, Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.

PAUL MAKONDA
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais Samia kumteua mkuu wa mkoa wa Arusha kuongoza wananchi wenye akili nyingi na wapambanaji wasiokata tamaa na wanaojua hatma ya nchi.

Makonda amesema mji huo ni wa wajanja wanaoweza kutoka na kwenda popote kupambana na kujenga uchumi. Makonda amesema watu wa mkoa huo wametambulisha umahiri wao katika utafutaji ilhali kuna baadhi ya mikoa waganga wa kienyeji ni wengi lakini si kwa mkoa wa Arusha.

Kwenye hatua nyingine, Makonda amesema jiji la Arusha litafungwa camera na kuhakikisha taa zinawaka na kuwa na polisi wa kitalii watakaokuwa wanaendesha baiskeli kuhakikisha ulinzi umeimarika.

Makonda: Ifike hatua watu wakija jiji la Arusha wajisikie raha na kupiga picha na polisi wao ambao ndio wanaimarisha ulinzi katika jiji la Arusha.

Pia tumekubaliana kuondoa mabango yote yanayochafua sura ya jiji la Arusha na kuhakikisha tunakuwa na muonekano mzuri ili watalii watakapokuja wasione kama watu tusioweza kujipanga, tunatembelea miji yao tunaona namna ilivyo.

Pia Makonda amemuomba Rais Samia kilomita 20 za barabara za lami kwani katika ya mji wa Arusha kuna barabaraba mbovu, amedai kuwa wananchi wa mkoa huo wamemtuma akamuombe 'mama yake' barabara na wanampima kama ni mama yake kweli.

RAIS SAMIA SULUHU
Rais Samia Suluhu ameongelea hali ya mafuriko nchini. Ametoa pole waliokumbwa na mafuriko ikiwemo Rufiji, Morogoro na Arusha. Pia ametoa pole kwa ajali ya wanafunzi iliyotokea leo jijini Arusha.

“Baada ya mvua hizi na hali ya kawaida kurejea, serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi za mafuriko kwenye maeneo hayo ili tuweze kuchukua hatua zitakazoondoa tatizo hili kwa muda mrefu. Niwaombe wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na watendaji wa serikali kwenye maeneo yao. Pia niwaase wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wanapofika sehemu zenye maji yanayotembea iwe wanapita kwa miguu au kwenye magari ili kuepusha athari zozote zinazoweza kusababisha vifo kwa wananchi wetu,” Alisema Dk. Samia.

Rais amesema tangu mvua zianze tangu kuanza kwa mvua ambapo Rufiji Serikali imepeleka chakula na dawa, pia kujenga tents za kuwahifadhi ikiwemo kutumia miundombinu ya shule kama madarasa.

Rais Samia amesema wameelekeza nguvu kukabiliana na mahitaji ya haraka na amewataka viongozi wote kuwajibika ipasavyo. Rais Samia amesema pamoja na maeneo kukumbwa na mafuriko kila mara kutokana na asili yake ya mabonde Serikali itaendelea kuchukua hatua na kuimarisha jitihada za kupambana na mafuriko.

Rais samia amesema baada ya mvua hizi na hali ya kawaida kurejea, Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi za mafuriko hayo na kuweza kuchukua hatua zitakazoondoa tatizo hilo kwa muda mrefu.
PIA, SOMA:
 
Sidhani kama ni sahihi Mwislamu kujumuika na wakristo wakati kila Ijumaa anaenda msikitini
 
Ikiwa hao mawaziri na vigogo mbalimbali, hawaogopi kutumia fedha zao na kutuma watu ili kumchafua Rais,

Yaani, Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania hawamuogopi, yeye ndo mwenye ukali wa namna yoyote,

Halafu wewe Mkuu wa mkoa Paul Makonda, kijana mchapa kazi na jasiri ambaye huna makali kama ya Rais, Je wewe huwaogopi hao wasiomwogopa Rais hadi ukawasemelee kwa mkuu wa nchi

Ni vema tu Mh Rais akakuongezea ulinzi ili uwe salama zaidi na muendelee kuwatumikia wanyonge

Mungu ibariki TANZANIA
 
Halafu wewe Mkuu wa mkoa Paul Makonda, kijana mchapa kazi na jasiri ambaye huna makali kama ya Rais, Je wewe huwaogopi hao wasiomwogopa Rais hadi ukawasemelee kwa mkuu wa nchi
Kwamba Makonda ana intelijensia ya kuwabaini hao wahalifu ila rais hana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…