Anyimwa Mke sababu ya Msosi: Wanaume wa mjini Badilikeni sasa Habari zimefika Mikoani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,871
24,651
Jamaa yangu tupo naye kazini si tunapenda kumtania kwa jina la Ustaadh anasimulia kisa kilichotokea week iliyopit Mkoa mmoja Mkubwa Huko Nyanda za Juu Kusini.

Miaka ya nyuma vijana wengi wa sasa wasingeweza kupata wanawake wakalala nao. maana ilikuwa ngumu sana kumvua mwanamke chupi(jamaa mmoja ameelezea hili) ilikuwa inatakiwa uwe umeshiba hasa ikiwezekana umbebe kumpeleka kitandani. huko ukamvue ch**** ilikuwa issue. au ikibidi umpige ngwala.... sasa vijana wa sasa nguvu hamna hayo mambo mngeweza kweli?

Anasema ana jamaa yake x alienda kujitambulisha Jijin huko kwenye wanaume na wanawake wanene weusi tii. X alipangiwa siku ya kwenda kujitambulisha kwa wakwe wilayani huko mbali na jiji.akaenda ikafika wakati wa kula akipelekewa Kuku mkubwa sana, wali, ndizi, maparachichi na mazagazaga mengine yakatengwa mezani.

Mchumba mtarajiwa akawa amekaa na jamaa yake ili wapige ule msosi.jamaa akala kimjin mjini karibia robo tatu ya chakula ikarud.inasemekana jamaa alikula kuku paja moja tu na wali kias ndizi mbili mbalagha. Yule dada alimbembeleza sana na kumshawish jamaa aongeze x aligoma akidai ameshiba sana na kuwa siku ile amekula sana hajawah kula vile.

Bint aliporudisha vitu jikoni mama akamwuliza mbona umetoa vitu kabla mwenzio hajala? Bint akajibu jamaa kwa ile ratio amekula sana. Mama akaguna tu maana ikiiuwa ni chakula cha usiku na ndo jamaa ametoka mjini wakajua atakuwa ameshiba njiani.

Kesho asubuh likapelekwa birika lenye maziwa na viazi sinia zima. Jamaa akanywa maziwa kikombe kimoja na viazi viwili. Tena bint alivyorudisha mama akauliza kwa ukali kidogo "kwa nini unatoa vyombo wakati mwenzio hajamaliza kula?" Bint akajibu jamaa amekula ameshiba. Mama akauliza kama mkwe mtarajiwa ni mgonjwa.akajibiwa si mgonjwa kabisa mzima bukheri wa afya.

Mchana tena hali ikawa ile ile kuku tena hakuliwa ipavyo.baada ya siku mbili jamaa akaaga anarud mjini.basi akaagwa akaondoka. Jioni wazaz wakamwita bint yao na kumwambia wao kama wazaz hawaamini jamaa kama anaweza kuwa mkwe wao. Anashindwaje kula kama wanaume wanavyokula. Anyway hana mwili mkubwa basi angalau aonekane ana nguvu za kipiga msosi wa kutosha kama mwanaume.wakawa na wasiwas hata watoto watazaliwa weak. Na anaweza asiwe anamshughulikia kitandani mtoto wao ipasavyo.

Wakaenda mbali zaidi kuwa atawatesa watoto na ndugu wakienda mtembelea wakawa wanapiga msosi sana jamaa atamind kuona yeye anakula slice mbili halafu kuna mtu anapiga mkate mzima au nusu mkate na chai na ugali asubuh.

Wakaelezea kuwa watu wasiokula kiasi cha kutosha huwa wanakuwa wachoyo na wabahili sana. Hasa huumia wakiona wengine wanapiga sana msosi majumbani kwao.hivyo atawaua kwa njaa. Wakamwambia hawana ugomvi naye kama bint atalazimisha ila wao wametoa maoni yao. Bint ajitafakari kama akiona waliyosema ni sawa ajiuzulu nafasi ya kuwa mchumba na hatimaye mke.lakini je anawezaje kupambana na watu wakitishia usalama wa mke wake au watoto?maana hatakuwa na nguvu za kutosha

Bint aliwaza sana. Akakumbuka kweli jamaa siku zote anamkataza asile sana eti atanenepa so apunguze mwili.wakienda hotel jamaa ananunua kuku robo wale wote na chips kavu. Akakumbuka wakinunua pizza medium jamaa anasema they have to share.

Bint akatengua uteuzi wake. Akaamwambia jamaa waishie tu palepale yeye anaamua kuendelea na maisha mengine. Nasikia jamaa week ya pili hii analia tu room hatak kufanya lolote. Na ukichukulia yupo likizo. Basi jamaa ndo kakosa mke kwa sababu ya kula kibitozi mikoa yenye kuzalisha chakula kwa wing na yenye wanaume wa shoka.

Wito wangu. Akina kaka mliopo mijini fanyeni kazi, kuleni vizuri msishindie na kulalia pombe tu na kutengeneza vitambi vya kizembe.pigeni kazi watu wanawaona mjue. Na pia msiwaharibie wenzenu walioko mjini reputation ikaonekana wote wako hivyo. Mjini wenyewe mnasema wanaume hawasifiwi kula?upuuzi huo. Mwanaume mzima unajiita kiroboto,nyigu n.k? Sasa mtakutana na simba,nyati,tembo,faru n.k
 
Mkuu mimi nipo Dar na ndo nilipozaliwa sema nimefanikiwa kusoma mikoani lakini pia wazazi wangu walikuwa wananisisitiza sana suala la kula. na nninyi wengine ndo mnaotuangusha sisi watu wa mitulinga
Mmerudi tenaeeee!!! Ninyi wamikoani mnamatatizo sana.ngoja tuwaandalie mabomu mengine
 
Du noma sana. Kula msosi bwana, unavunga nini? Menyuka aisee, unaona! Unaonaa? Mwenzio Mke hana tena! Kabaki kulia, eti mwanaume kabisa analia. Wanatuaibisha sana watu wa Daslam
 
huwa nikiendaga kwenye harusi huwa naulizwagwa "unakula na nani" ??

Sikupatii picha na hilo domo lako mkuu hahaaa

Ila mwanaume kula aisee. Unapaswa kula sio kujivunga. Mimi huwa hakitupwi kitu hadi bebi akibakisha hata tuwe hoteli gani anajuaga lazima asogeze kwangu.

Huwa sipendi kwakweli sahani itoke mezani irudi jikoni na chakula. Kwanza ni dhambi
 
Kwenye msosi wala sijivungi, natupia mikono mdomoni mpaka mkanda nihakikishe naufungua..!!
 
Mwanaume anayeringa kwenye msosi anakera, mi mwenyewe sivungi, unakuta mkaka eti chipsi mayai hamalizi, Mimi chipsi mayai moja sishibi labda ninywe na Pepsi na maji liter moja
Wewe unanifaa sn kw kampan, napenda mwanamke anaekula km mm.....halafu nakula sana natural food, mlenda, mgagani, majani ya kunde, kisamvu, ugali natumia dona, vitafunwa napendelea mihogo, au magimbi.....mm ni wa mkoani km mnavyotuita, nikija huko kwenu sa cjui nipaiteje huwa napenda kupata lunch kw mama ntilie flan mitaa ya mwenge anapika dona la maana sn, roast dagaa na mamboga mboga, nikija ntakutafuta Senee, km upo mjini!
 
Mi kiukwel nikiletewa hawa kuku wa humu town ambao now ni legelege huwa sibakizi kitu.natafuna mpaka mifupa.kuku laini utadhan waliumbwa kwa nyama tupu.na siku hizi nmezila kula kabisa hawa kuku mabitoz na masister du.

Nlishangaa nmeishi na jamaa mmoja hostel miaka ya nyuma anaimba wimbo eti mwanaume hasifiwi kula. Nlishangaa sana. Sili ili nisifiwe nakula sababu mwil unahitaj. Hawa jinsia me ya siku hizi zaman wasingeoa au kupata madem kabisa. Maana miaka yetu ilitaka ukakamavu hasa
 
Soseji moja, yai moja,kikombe cha chai.... Asubuhi
Kiepe yai, mshkaki mmoja... Mchana
Kipande cha muhindi chenye pilipili na ndimu.. jioni
Kiepe yai na Fanta... Usiku
Siku imeisha!!!!
Sasa msosi gani huo.
Kwa asubuhi huo msosi ni pale unapoamka kisha baada ya saa moja ndio inagongwa breakfast yenyewe.
 
Umenikumbusha miaka ya 1985 a tukiwa kama washenga tumeenda kutoa mahari tulifika mida ya saa nne asubuhi hatujakaa sawa msosi ukaja ugali na nyama ya kuku wali na makande pembeni tuko watu sita tukala kikaisha kwa mbinde mida ya lunch tena wali ugali na nyama ya mbuzi na maziwa mgando tulikula mpaka nikaona hapa tunakomoana si kwa msosi huo tukamuita shemeji mtu tukamwambia shemu sikia chakula kimebaki na hapa tumeshiba fanya utaratibu kisirudi jikon kitunze badae mtawapa mbwa ila watu wa jikoni wasijue shemeji mtu acha acheke akafanya yake na usiku mwendo ule ule kesho yake tunarudi muoaji anasema nitakuwa nakuja ukweni kwa kushitukiza tu
 
Mwanaume anayeringa kwenye msosi anakera, mi mwenyewe sivungi, unakuta mkaka eti chipsi mayai hamalizi, Mimi chipsi mayai moja sishibi labda ninywe na Pepsi na maji liter moja
Chipsi mayai nacho chakula??
 
Huku Darisalam changamoto sana Mkuu.
Wale tunaopenda misosi ya kutufanya tuwe strong huwa tunateseka sana.

Maana utakuta mtaa mzima wanauza chips tu basi, madukani sasa ni sembe kwa kwenda mbele.inakera sana.
 
Mimi unaweza ukajua mwanaume mwenzio ati hahahahaaa. . Napenda kula sanaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…