Aneth Msuya ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya auawa kinyama Dar

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,271
1,119
Nimepata taarifa hii ya mauaji ya kinyama ambayo imekuwa ikizunguka kwenye makundi ya WhatsApp....

Anathe Msuya mdogo wa Erasto Msuya bilionea wa Arusha aliyeuawa, amechinjwa usiku kuamkia leo nyumbani kwake eneo la Kibada block 16. Katika tukio lenye mazingira ya ujambazi lakini hakuna kilichoibiwa..


Inasomeka...

Anaitwa Annate, ni mdogo wake marehemu Erasto Msuya aliyepigwa risasi 22 Kia. Nimepigiwa simu asubuhi majirani walikuwa wanatafuta ndugu zake. Sidhani kama ni majambazi kwa sababu inasemekana hakuna kilichoibiwa. She was found lying naked on a pool of blood huku amechinjwa. Alikuwa anaishi na mtoto wake mwenye miaka mitano na dada wa kazi. Mtoto amekutwa akiwa amevaa sare za shule bado ikimaanisha hakuwa amebadili toka jana alivyotoka shule.

Yaani Aneth hata siamini, jana tulikua nae kazini, kaondoka kufika home kakuta housegirl katoroka, akapiga simu kwa mwenzetu akamueleza kwamba leo hatokuja ili angalie logistics. Ndio asubuhi Himalaya hizo taarifa. Mtoto wake ana miaka minne ndio anahojiwa anasema hiyo jana walikuja watu watano weusi, wakavunja mlango ni majira ya saa tatu usiku, akakimbia chumbani, walipoingia wakamkuta mtoto wakauliza mama yuko wapi akasema chumbani, wakamfuata huko mtoto hajui kilichoendelea hadi saa 1 asubuhi school bus imekuja anajaribu kutoka kashindwa ikamwacha, ndo akafanikiwa kutoka kaenda kwa jirani kawaambia school bus imemuacha, mama kalala haamki na mimi nasikia njaa. Ndio jurani kwenda wakakuta kachinjwa yuko uchi (seems walimbaka) kisu kipo hapohapo na hawajaiba kitu.

=======================

Dada wa bilionea Msuya auawa kinyama Dar

DADA wa marehemu Erasto Msuya aliyetambuka kwa jina la Anathe Msuya, ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana Dar es Salaam.

Anathe aliuawa nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni, ambako inaelezwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuahidi kutoa taarifa kamili leo.

“Ni kweli kuna tukio hilo la kifo, lakini taarifa kamili kwa undani nitazitoa kesho (leo), ninaomba muwe na subira,” alisema Kamanda Sirro.

Anathe ni dada wa marehemu Erasto Msuya ambaye alikuwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyeuawa kwa kufyatuliwa risasi.

Msuya aliuawa Julai 7, mwaka 2013 katika eneo la Mijohoroni, kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akiwa ameitika wito wa kwenda kununua madini ya Tanzanite baada ya kupigiwa simu na vijana wawili waliomtaka wakutane maeneo hayo.

Inaelezwa kuwa alifika katika eneo hilo akiwa na gari lake aina ya Range Rover T 800 CKF na kuwakuta vijana hao wakimsubiri.

Baada ya kuteremka, Msuya aliekea kumsalimia mmoja wa vijana hao, hata hivyo kabla hajamfikia kijana huyo aliitoa bunduki ya SMG namba KJ 10520 aliyokuwa ameificha kwenye koti na kumfyatulia risasi takribani 22 mwilini.

Bilionea huyo aliyekuwa akimilika vitega uchumi mbalimbali jijini hapa na maeneo mengine nchini aliuawa saa 6:30 mchana.

Taarifa za polisi zilisema katika eneo la tukio ilikutwa bastola namba GLS 417T2 CAR 83271, mali ya Msuya na vitu vingine, ambavyo ni simu ya Samsung S5, iPhone na koti la mmoja wa watuhumiwa likiwa limetelekezwa mita chache kutoka eneo la tukio.

Polisi waliweza kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo na kuwafikisha mahakamani mjini Moshi ambako kesi hiyo inaendelea kusikilizwa.

Gazeti Mtanzania



aneth 2.jpg
aneth.jpg

Hizi ni Picha za Marehemu enzi za Uhai wake

---
VIDEO: Mauaji ya Erasto Msuya, Aneth Msuya na hukumu ya Miriam Mrita
Soma Sakata la Kifo cha Bilionea Msuya

MAUJI YA ANETH MSUYA NA MWENENDO WA KESI YA MAUAJI YAKE

AUG 23, 2016 Mirima Mrita alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauji ya Aneth Msuya

Soma Mjane wa Erasto Msuya apandishwa Kizimbani Kisutu

SEPT 18, 2023 Mahakama ilimkuta Miriam Mrita na kesi ya kujibu Mauji ya Aneth Msuya
Soma Dar: Mke wa Bilionea Msuya akutwa na Kesi ya Kujibu mauaji ya wifi yake

FEB 23, 2024 Mahakama Kuu ilimuachia huru Miriam Mrita
Soma Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia mauaji ya Aneth Msuya


MWENENDO WA KESI MAUAJI YA BILIONEA ERASTO MSUYA

Septemba 17, 2013 watuhumiwa wakiwa kwa mganga wakijizindika wasikamatwe

Soma Waliomua Bilionea Erasto Msuya wakutwa kwa sangoma

Juni 12, 2014, Mahakama yaelezwa jinsi Erasto Msuya alivyouawa
Soma Mahakama yaelezwa bilionea wa madini Erasto Msuya alivyouawa

Oktoba 27, 2017, Shahidi adai kuahidiwa Tsh 17m kutekeleza mauaji
Soma Shahidi aelezea walivyoahidiwa kulipwa Sh 17 milioni kila mmoja kumuua bilionea Msuya

Mei 11, 2018, Shahidi alidai kuwa Mfanyabiasha wa Madini, Chusa ndiye alipanga mauaji
Soma SHAHIDI: Chusa alipanga mauaji ya Bilionea Msuya

Mei 14, 2018 Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu washtakiwa 6
- Kesi ya bilionea Msuya: Sita wana kesi ya kujibu huku mmoja akiachiwa huru

Julai 23, 2018 washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa
soma Washtakiwa watano mauaji ya bilionea Msuya wahukumiwa na Mahakama Kuu adhabu ya kunyongwa hadi kufa

Agosti 18, 2018 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa wakata rufani
Soma Waliohukumiwa kwa mauaji ya Bilionea Msuya wapinga kunyongwa

Jaji aliyetoa hukumu atishiwa kifo
Soma Jaji aliyesikiliza kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya na kutoa hukumu ya kifo atishiwa kuuawa

Pia soma Aliyeachiwa kesi ya mauaji ya Bilionea Msuya aeleza mazito


UGOMVI WA MALI ZILIZOACHA NA ERASTO MSUYA
Familia ilishindwa kuelewana suala la mirathi na kupelekea Serikali kuingilia kati
Soma Mali za Marehemu Bilionea Erasto Msuya, ndugu ngumi mkononi

Mama Mzazi wa Erasto Msuya adai kuwa mjane alikomba mali kabla ya mazishi
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Wadau wahoji uhalali wa ndugu wa Miriam Mrita kusimamia mali za Erasto Msuya
Soma Mama wa Bilionea Msuya: Mke alikomba mali kabla ya kumzika mwanangu

Mama Mzazi wa Msuya akubali kuondoa shauri Mahakamani ili kulimaliza kifamilia
soma Mama wa Bilionea Msuya akubali kuondoa kesi kwa Muda Mahakamani

Mahakama yataka pande mbili za familia kukaa meza moja na kuondoa tofauti
Soma Ugomvi wa Mali za Marehemu Bilionea Msuya, Mahakama yanena

2021, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumuondoa Miriam Mrita kuwa msimamizi wa Mali
Soma Mahakama yamuengua mjane wa Bilionea Erasto Msuya kusimamia Mirathi ya Mumewe
 
Duh huko arusha vitu hivi vimeota mizizi lakini polisi watawakamata wauaji hao...hata wakijificha wapi watakamatwa
 
Dunia bila mnyama mwanadamu inaweza kuwa Aden mara ya pili. May the almighty rest her soul in peace. Kijana atabaki na bad memory for good,Mwenyezi Mungu amjaze ujasiri na hekima
 
Arachuga hiyo.erasto alikuwa bilionea wa kununua tanzanite huko mererani.
 
Back
Top Bottom