ANIMALS INTELLIGENCE: Nani mwenye busara zaidi hapa?

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258


Kwa muda mrefu nimeendelea kushangaa intelijensia ya wanyama. Kwa muono huu wa picha hapa, kwamba kuna viumbe hutanguliza watoto na wengine hukaaa sambamba na wengine hukaa nyuma ya watoto wao.. Je uongozi upi ni bora hapa?

Ukiangalia kwa makini pia utagundua hata watoto wako na mpangilio fulani hivi. Mfano bata kuna watatu wako sambamba na kuku kuna mtoto mmoja yuko mbele na hawa wengine wamesambaa kiaina.
 
Bata hutangulia mbele vifaranga huja nyuma,

Kuku hutanguliza watoto mbele yeye huja nyuma.

Kuna mazingatio makubwa sana ya ulezi kati ya hawa ndege wawili.
 

tanguliza watoto mbele, unawaona na hata adui akija unamuona na ni rahisi kujihami na kuwaokoa watoto. adui akija kwa nyuma anaanza na wewe hivyo unaweza kujihami na kujinasua hivyo watoto wanakua salama, kuku ni mlezi mzuri zaidi sababau hakubali kumuacha mtoto nyuma
 
uchambuzi mzuri na hawa wanaoacha kama bata falsafa yao ni ipi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…