Na Mimi kama mwana Kagera nitoe mawazo yangu juu ya anguko la uchumi wa mkoa wa Kagera. Nimeona majadiriano ya kila aina ya sababu ya anguko la uchumi wa mkoa wa Kagera.
Ni kwa bahati mbaya kwa majadiriano hayo, wengi huchukulia picha ya mji wa Bukoba tu kuwa kiwakilishi cha mkoa wa Kagera. Siyo kweli mkoa huo ni pamoja na wiliya za asili za Karagwe, Biharamulo, Ngara na Bukoba yenyewe.
La pili, kama hujaanza kujadiri ni vizuri kuwa na picha ya eneo lote la mkoa, uwe na picha ya sehemu kama Kanyigo, Kamachumu, Nshamba, Kayanga, Nyaishozi, Bushangaro, Nkwenda, Kaisho, Ngara, Rulenge, Rusumo, .... Nasema haya kwa sababu wenyeji wa mkoa huwa na tabia ya kujenga na kuendeleza maeneo yao ya asiri kuliko kujikusanya sehemu Moja ndogo na kuijenga na ikatoa picha tofauti na sehemu iliyobaki.
Tatu. Maendeleo ya sehemu au uwekezaji uletwa na watu tofauti tofauti. Dar haijajengwa na Wazaramo tu, Mwanza haijajengwa na Wasukuma tu. Na hii inatokana na sababu nyingi, kama nitakavyo eleza hapa chini. Kwa hiyo nawabebesha lawama wazawa kwa asilimia 50 tu na 50 zilizobaki ni umma wote kwa jumla, hasa serikali.
Uwekezaji tunaoona unategemea na furusa, miundombinu, sera na miongozo ya serikali. Mwekezaji uwe mgeni au mwenyeji anatemegea kuwekeza atakapopata faida. Hakuna uzalendo katika uwekezaji huku unapata hasara. Mimi nimeiona Kagera miaka ya 80, 90, na 2000. Kikubwa kilichochangia kiangusha uchumi wa mkoa( pamoja na sababu zinazosemwa- sitazirudia ) ni:
1. Sera na miongozo ya serikali. Zao la kahawa. Mapato makubwa ya uchumi yalitokana na mauzo ya zao la kahawa. Bei ya kahawa imekuwa haimunufaishi mkulima kiasi kwamba wakulima wanakata tamaa ya kuwekeza katika kilimo cha kahawa. Kahawa chache zinanazolimwa zinanapelekwa Uganda kwa magendo. Uganda Sasa hivi inaongoza kwa nchi za Afrika mashariki kwa kilimo cha kahawa. Bei ya kahawa Uganda ni mara mbili ya Bei ya Tanzania. Wakati wa mavuno ya kahawa serikali inatumia nguvu nyingi kuzuia kahawa isivushwe kwenda Uganda.
Wape Bei mzuri wakulima. Wawekezaji watawekeza katika kilimo cha kahawa. Kahawa ya Uganda inauzwa kwenye soko la nje ambapo na sisi tunauza.
2. Miundo mbinu. Factor inayoangaliwa na mwekezaji ni pamoja na miundo mbinu, barabara, umeme, maji ....... Usafiri mkoa wa Kagera ni shida. Juzi juzi ndiyo tumeunganishwa na mtandao wa Barabara za rami. Usafiri majini, tangu Meri ya Bukoba izame na kiharibika kwa Mv Victoria ilipoharibika, ilichukua miaka mingi mkoa kuunganishwa na mikoa mingine kwa njia ya maji. Juzi tu ndiyo hali imeanza kurekebishwa.
Umeme: Mpaka Sasa mkoa haupo kwenye grid ya taifa. Tunategemea umeme kutoka nchi jirani. Jirani akijisikia anawasha na akijisikia anazima. Nani atawekeza katika wiwanda pasipokuwa na uhakika wa umeme na maji?
3. Natural resources: Maendeleo unayoona katika miji kama Arusha (mbuga za wanyama), Kilimanjaro (mlima Kilimanjaro), Geita (madini), Kahama (madini) na kwinginepo kumechangiwa na promotion ya natural resources. Mkoa wa Kagera ulijaa mali asili nyingi ambazo hazikuendelezwa. Kilikuwa na mbuga wa wanyama pori la kutoka Bukoba kwenda Karagwe. Zikaanzishwa runch na kilimo cha miwa. Pori la Kimisi likajifia na kuwekwa na ngo'mbe na wakimbizi wa Rwanda.
Kilikuwa na madini ya bati- Kyerwa. Kuna migodi ya Kabanga nickel. Mali asili zote hizo ni serikali tu yenye uwezo wa kuzisimamia na kuziendeleza.
4. Natural disasters ambazo healing yake ni concern ya serikali. -Vita ya Uganda ambayo iliacha watu na miundobinu hoi. Barabara, majengo, madaraja, wiwanda vilibomolewa.
- vita ya Rwanda na Burundi. Mapori yalivamiwa na waasi, barabara zilifungwa - hupiti barabarani mpaka uwe na escort. Shughuri za uchumi zilisimama.
-mbuga za wanyama za Kimisi, Rumanyika na nyingine hazikufanyiwa promotion.
Pamoja na mengine kama tetemeko la ardhi, ugonjwa wa ukimwa, munyauko wa migomba na Sasa hivi umeingia munyauko wa kahawa.
Kwa hiyo tunapojadiri anguko la uchumi wa mkoa wa Kagera, lazima tutilie maanani hayo yote. Tusilaumu wazawa tu.
Mchana mwema.