Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 357
- 798
Rais naskia ametangaza majengo yote ya eneo la Kariakoo yafanyiwe uhakiki. Japo sijaithibitisha hii habari niliisikia tu juu juu kwenye mitandao.
Uhakiki wa majengo ni jambo zuri mno kwasababu itatuhakikishia kupungua kwa majanga ya aina hii - majengo kuporomoka.
Kwahiyo kama hili zoezi litakuwepo, mimi sitalipinga. Lakini kulingana na aina ya utendaji kazi wa watumishi wa serikali, naona kabisa kwamba kutatokea rushwa kubwa mnoo.
Kwanini nasema hivi - kwamba kutakuwa na rushwa kubwa?
Mimi nina uhakika kabisa, ukitumia mbinu zote za uhakiki wa majengo ukafanya mpaka zile 'stress testing za ki engineer' kama inavyotakiwa, kuna uwezekano ukakuta kwamba asilimia 30 ya majengo ya Kariakoo yanakosa sifa.
Sasa hapo ngoma inakuja kwamba, jengo lisilokuwa na viwango may be mmiliki ametumia zaidi ya 5 billion, maana yake hapo hata yule anayehakiki tayari anajua kwamba kwa vyovyote vile huyu mmiliki wa jengo anaweza hata kutoa hongo ya Milioni 100 ili tu aandikiwe kwamba jengo lake linavigezo vyote.
Na ni rahisi kwa afisa kuaccept huo mlungula, kwasababu ki uhalisia hata kama jengo lingine litaanguka kariakoo, inaweza kuwa ni baada ya miaka 10, ambao tayari ni mda mrefu sana.
Rai yangu kwa serikali ni kwamba hili jambo kama wanania kweli wa kulifanya ki ueledi, basi lifanyike kwa levels zaidi ya 3. Yaani kuwe na 3 teams ya independent assessors (2 wawe watanzania, 1 awe foreign company) unamtafuta hata kampuni ya kichina kwa kazi hiyo.
Hiyo itapunguza mwanya wa rushwa ambao tayari naanza kuunusa. Lasivo, nacho kiona hapa ni 'Kufa kufaana'