Andrew Chenge sasa aage na kuondoka...

Ndugu zangu,

Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.

Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.

Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.

Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.

Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge atajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.

Maggid Mjengwa.

Picha: Gazeti Mtanzania.

Nyie watu wa ajabu kweli kweli

Kwamba ndio mmejua leo kuwa Chenge hafai?

Mlivyomchagua kuwa mwenyekiti wa Bunge kwa kura nyingi za wabunge wa CCM hamkujua?

Hebu msituchoshe na msitufanye wajinga kwa makosa yenu mnayofanya kila siku.

Waingereza walirudisha chenji ya Rada Bil 40 na ushee na SFO ikasema kabisa Chenge amehongwa...Mlifanya nini?

Msituchoshe wezi nyie CCM
 
Nyie watu wa ajabu kweli kweli

Kwamba ndio mmejua leo kuwa Chenge hafai?

Mlivyomchagua kuwa mwenyekiti wa Bunge kwa kura nyingi za wabunge wa CCM hamkujua?

Hebu msituchoshe na msitufanye wajinga kwa makosa yenu mnayofanya kila siku.

Waingereza walirudisha chenji ya Rada Bil 40 na ushee na SFO ikasema kabisa Chenge amehongwa...Mlifanya nini?

Msituchoshe wezi nyie CCM
PCCB ya Tanzania ilimsafisha
 
Yaani huyu Mzee anarukaga vihunzi kweli, ila safari hii amenasa kwenye kamtego kadogo, chini ya magu hachomoki mtu

Hayo ndio maombi ya kila mmoja wetu mkuu ila, Hata chembe ya hofu hana. Nakuambia, ka si kwa vile utamaduni ni mtu kuongoza miaka 10, 2020 Mtemi Chenge angelikalia kiti kitukufu. Hatokufa kabla hajakikalia kile kiti na kusafisha mashaka yoote mliyo muwekea. Just mark ma words,
 
Jamaa hana mshipa wa aibu any way Ccm ndy walivyo

OvA
Na bado anasimama na kusema kwamba yeye ni msafi kama pamba ilivyo nyeupe...
Na eti Rais amedanganywa na watu wasio na nia njema na Tanzania..
 
Kama MACK ZUCKERBERG na BILL GATES wao Wali DROPOUT pale HAVARD UNIVERSITY..
ANDREW CHENGE yeye alikaza mpaka aka GRADUATE pale ..
Mnategemea WABONGO mtaenda nae sawa.?
 
wewe acha tu, yaani ni mchafu hakuna...labda JPM alivyouliza sasa atang'atuka..
 
Na bado anasimama na kusema kwamba yeye ni msafi kama pamba ilivyo nyeupe...
Na eti Rais amedanganywa na watu wasio na nia njema na Tanzania..
Anastahili Kutolewa kwa kipigooo tu kama vp

OvA
 
Anastahili Kutolewa kwa kipigooo tu kama vp

OvA
Ukweli ni kwamba hadi sasa chenge alipaswa awe tayari amehukumiwa na adhabu yake ingependeza ifanane na zile zinazo tolewa hadharani huko Saudi Arabia
 
Ajaribu mtu kumnyang'anya cheo chake kama hajakuta kiti chake hapo bungeni kimemwagiwa"unga mweupe mweupe" hivi.
 
yani hawa wezi wakubwa huwa hawalali segerea, kule wanaenda maskini na wengine wenye kesi za kubambikiwa, duniani hakuna haki kabisa
 
Sometime namuonea Chenge wivu. Mnaweza kumsema wee na baadaye mkashangaa anagombea urais na ikulu akaenda. Nape alizunguka na jina lake mikoa yote Tanzania na akafanikiwa kuwatingisha Lowassa na Rostam ila Chenge hata hakujigusa. Yule ndiye mtemi bwana. Nyie mnatema mate kushoto yeye anafukia kulia na biashara zinasonga.

Kwanza uliona jana akitajwa sehemu yoyote na Magufuli? Hujiulizi kwa nini? Yeye kwake hivi vituhuma ni kama maji anavioga na kuvinywa vilevile.
Upo sahihi Chenge huyo huishia kutajwa tu
 
Kuna 'shortcut' ambayo ndiyo njia rahisi kuliko zote i.e. kumvua uwanachama wa CCM kutakopelekea kukosa sifa za Ubunge au kuwa Mbunge wa Mahakama, swali la kujiuliza ni: Je, Mwenyekiti ana nia, uwezo na sababu ya kulivua 'gamba' hilo sasa?
Hapo ndipo ninaposhangaa. Wale wanaonekana kuwa upande wa EL wanavuliwa uanachama mara moja,lakini wale ambao ni key players kwenye maufisadi tunawakumbatia.
Made in Tanzania!!
 
Chenge alijiu
Ndugu zangu,

Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.

Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.

Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.

Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.

Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge atajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.

Maggid Mjengwa.

Picha: Gazeti Mtanzania.
Chenge alijiuzulu wakati wa sakata la Escrow. Lakini CCM mkamrudisha tena hata kabla ya wino haujakauka. Nawashangaa sana!
 
Ndege wafananao huruka pamoja! Hilo ndilo joka la mdimu! Hakuna anayethubutu hata kulitaja kwa jina!
 
Nyie watu wa ajabu kweli kweli

Kwamba ndio mmejua leo kuwa Chenge hafai?

Mlivyomchagua kuwa mwenyekiti wa Bunge kwa kura nyingi za wabunge wa CCM hamkujua?

Hebu msituchoshe na msitufanye wajinga kwa makosa yenu mnayofanya kila siku.

Waingereza walirudisha chenji ya Rada Bil 40 na ushee na SFO ikasema kabisa Chenge amehongwa...Mlifanya nini?

Msituchoshe wezi nyie CCM
Haya Ya Akina Chenge Tumeyapigia Kelele Imepita Miaka 16 Sasa...!
- Mfupa huu ukimshinda na Magufuli, basi, hicho Chama Tawala kitakuwa kweli kimeoza, na nchi itakuwa kweli imelaaniwa.

Ndugu zangu,

Hapo chini ni makala niliyoandika na kuchapwa na jarida Raia Mwema mwaka 2009.

"Sakata la rada: Chenge ametajwa,hatushtuki!

Na Maggid Mjengwa,

ZIMETUFIKIA habari za Makachero wa Uingereza kitengo cha Makosa
Makubwa ya Jinai ( SFO) kubaini maovu zaidi ya kifisadi anayotuhumiwa
kuyafanya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Miundo
Mbinu Bw. Andrew Chenge. Kwamba Chenge ameongopa chini ya kiapo juu ya
fedha,dola za Kimarekani miloni moja na nusu alizoweka kwenye akaunti
yake Kisiwani New Jersey.

Katika hali ya kawaida tulitarajia idara zinazohusika zishtuke. Na
mshtuko wake ndio utakaopelekea pia jamii kushtuka. Ni kashfa kubwa.
Ni aibu kwa nchi, kwa Serikali na kwa chama tawala,CCM. Maana, Chenge
amekuwa kiongozi mwandamizi Serikalini na hadi sasa anakalia kiti cha
ubunge.

Habari hizi zimetufikia wakati Bunge likiendelea na kikao chake mjini
Dodoma. Watanzania hatuwaombi wawakilishi wetu,bali tunawataka
wawaulize na kuwahoji wenye kuhusika na kutoa ufafanuzi juu ya kashfa
hii. Hili halihusu itikadi za vyama, lina maslahi mapana ya nchi yetu.
Kazi hii tusiache ifanywe na wabunge wa Uingereza.

Itakumbukwa huko nyuma wabunge wa Uingereza wakiongozwa na mbunge wa
kujitegemea mwanamama Clare Short, walipata kuichachafya serikali
iliyopita ya Bw. Tony Blair juu ya sakata la nchi yetu kuuziwa rada ya
bei juu na pia rushwa kutumika katika ununuzi huo.
Wakati huo Bi. Clare Short alikuwa Waziri mwandamizi wa Masuala ya
Maendeleo na Misaada katika Baraza la Mawaziri la Bw. Tony Blair.
Yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Fedha kansela Gordon Brown
walipinga ununuzi huo. Leo tunaona,kuwa Clare na Brown walikuwa
sahihi. Gordon Brown ndiye Waziri Mkuu wa sasa wa Uingereza. Huku
kwetu tulihoji na kudadisi tuliitwa kwa majina mengi; " wavivu wa
kufikiri", " wenye wivu wa kike" na mengineyo.

Nilipata kuandika, kuwa aibu hii kamwe haiwezi kuwa yua Uingereza tu,
ni aibu yetu pia. Ni aibu yetu kwa vile kuna baadhi ya Watanzania
wenzetu wenye kutuhumiwa kuhusika na uhalifu huu. Wakati mjadala wa
ununuzi wa rada hiyo ulipofukuta mwaka ule wa 2001, sio tu tulionekana
wajinga tuliokuwa tukihoji ununuzi ule bali hata wale waliokuwa nasi
katika kupigania kufutiwa ama kupunguzwa kwa madeni yetu tuliwageuka;
mfano mzuri ni Shirika la Oxfam. Tuliwaacha wakiduwaa , wakati wao
walisisitiza, kuwa Serikali ya Uingereza isitoe leseni kwa kampuni ya
BAE, kwa vile mkataba huo haukuwa na manufaa kwa Watanzania walio
wengi. Serikali yetu ilitangaza kuupokea uamuzi wa serikali ya
Uingereza "Kwa mikoni miwili".

Tangu awali, sakata hili la ununuzi wa rada liliamsha maswali mengi
yenye kuhitaji majibu, mwaka 2001 kupitia safu ya " Gumzo la Ijumaa"
kwenye gazeti la Majira nilipata kuuliza yafuatayo; Je, ni nani hasa
wahusika wakuu wa manunuzi ya rada hiyo? Ni akina nani waliopitisha
uamuzi wa manunuzi ya rada hiyo? Je, bunge letu lilipata kufikishiwa
muswaada wa manunuzi ya rada hiyo, kuujadili na kutoa mapendekezo yao
kwa niaba ya wananchi? Je, kulikuwepo na hali ya kushindanisha
makampuni ya utengenezaji wa rada hizo duniani? Hivi tukiwa tumezama
ndani ya lindi la umasikini, je, ni rada ya kisasa na ghali mno
ndiyo tuliyohitaji ? Je, kuna mianya ya rushwa ya kimataifa katika
manunuzi ya rada hii? Leo tunapata majibu ya baadhi ya maswali yale.
Wakati ule Serikali ya Uingereza ililazimika kuahirisha
kutoa uamuzi wake wa kuuza au kutoiuzia Tanzania, rada yenye thamani
ya Dola za Kimarekani milioni 40 baada ya kubainika kwamba tayari
kiwanda cha BAE ambacho ndicho chenye tenda hiyo kilishatengeneza na
kuiweka tayari kwa kuisafirisha.
Ikaelezwa, kuwa rada hiyo ilitengenezwa baada ya maafisa
wa BAE kupewa uthibitisho na wizara ya ulinzi ya Uingereza kwamba
itapita na suala la leseni lingekuwa ni suala la kupitisha tu
(formality). Kwamba kusingekuwa na ugumu katika hilo.
Ikasemekana, kuwa hata Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Tony
Blair akiungwa mkono na aliyekuwa waziri wake wa ulinzi Geoff Hoon
alishinikiza leseni itolewe kwa vile mkataba huo wa mauzo ungeokoa
ajira ya Waingereza 250 katika kisiwa cha Wight. Kwamba muhimu kwa
Uingereza ilikuwa ni ajira za watu wao kwa gharama za walalahoi wa
Tanzania!
Ndani na nje ya nchi yetu, tuliokuwa tukipinga manunuzi ya
rada hii ya gharama kubwa tulielewa umuhimu wa Tanzania kuwa na rada
bora ya kudhibiti safari za anga, lakini, tulichohoji ni umuhimu wa
kununua rada ya thamani kubwa ilhali kulikuwa na uwezekano wa
serikali kununua rada bora kwa thamani isiyozidi dola za Kimarekani
milioni kumi kwa wakati huo. Kumbe, leo tunafahamu, kuwa kung'ang'ania
kule kuinunua rada ile kulikuwa ni kwa maslahi ya baadhi ndani ya nchi
yetu! Kulikuwa na " Sete Pasenti! Ama kweli; Mvunja nchi ni mwananchi.

Muhimu lingine kulifahamu hapa ni ukweli, kuwa kiwanda kile cha BAE
kilichotuuzia rada ile, kimo katika rekodi ya kuhusishwa na kashfa ya
rushwa ya kimataifa. Vielelezo vya kuthibitisha kiwanda hiki na rushwa
vipo kupitia kumbukumbu za Shirika la Habari la Uingereza , BBC
hususan kwa kutafuta habari kuhusiana na kashfa ya mauzo ya silaha
nchini Afrika Kusini( www.bbc.co.uk)
Kule Afrika ya Kusini, BAE inatuhumiwa kuhusika na kutoa rushwa
kwa mwanachama mashuhuri wa chama cha ANC Bw. Toni Yengeni akiwa kama
mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge la Afrika ya
Kusini. Ilidaiwa Toni Yengeni alifanikisha kiwanda cha BAE ambacho
ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kutengeneza zana za kijeshi nchini
Sweden, SAAB kupata tenda ya mauzo ya silaha za angani. Kufuatia
kashfa hiyo, Bw. Toni Yengeni mwezi Oktoba mwaka 2001, alikamatwa na
kulazimika kujiuzulu nyazifa zake ndani ya ANC. Yengeni alihukumiwa
kifungo cha miaka minne jela.

Kwa taarifa hizo, tunaona wazi, kuwa hawa watu wa kiwanda cha
BAE wananuka rushwa katika kuendesha biashara zao. Kwanini basi
tusiwe na mashaka kuwa wametumia rushwa katika kufanikisha tenda ya
mauzo ya rada yao Tanzania kama sasa tunavyothibitishwa na Kitengo cha
Makosa Makubwa ya Jinai cha Uingereza?

Naam. Waingereza wamefanya uchunguzi wao,wamekuja na taarifa
ya kisayansi. Lakini, kama nchi, ingekuwa vema na sisi kama tukafanya
uchunguzi wetu kuwatafuta wengine zaidi waliohusika na uhalifu huo.
Maana,haiyumkini kiongozi mmoja tu mwandamizi akahusika peke yake na
wizi huo mkubwa. Tufanye hivyo kwa maslahi ya nchi yetu. Tufanye hivyo
ili kurudisha imani ya wananchi.

Na kama watapatikana wahusika zaidi, basi, kama walivyofanya Afrika
ya Kusini, nasi tuwafungulie mashtaka mahakamani. Ni kwa namna hii
tutarudisha heshima yetu kama nchi, na vile vile kutoa fundisho kwa
wengine."

Maggid Mjengwa.
 
Haya Ya Akina Chenge Tumeyapigia Kelele Imepita Miaka 16 Sasa...!
- Mfupa huu ukimshinda na Magufuli, basi, hicho Chama Tawala kitakuwa kweli kimeoza, na nchi itakuwa kweli imelaaniwa.

Msiwe mnajitahidi kucheza na maneno na kujifanya mnaipenda nchi hii ilihali ninyi CCM na marafiki zenu ndio mmekuwa mstari wa mbele kuiteketeza nchi hii.

Na hata sasa hamna nia yoyote ya kuisaidia nch hii

Kuna njia moja tu...Tubadili katiba tuondoe kinga ya Rais ili awajibishwe kwa matendo anayoyafanya akiwa madarakani....Haya mambo ya kudeal na chenge as inividual tukiwaacha waliomtuma chenge..Kina Mkapa na Kikwete wala hayatatusaidia.

Huyo magufuli unayemsema ni sehemu ya uozo huo...Yeye hadi sasa kwenye hiki kipindi chake ameshafanya madudu makubwa tu ambayo anapaswa kuwajibishwa
 
Back
Top Bottom