Msangi ndugu yangu Msangi weeee ebu jisomee hapa mwenyewe..Bold Nyeusi kwa nyeusi, Blue kwa Blue na Nyekundu kwa Nyekundi.. Shahidi wako akana na pengine kuruka vile vile - msinishirikisheeeee!
Msangi:-
Kwanza ifahamike mimi huyu Dk. Ulimboka na mwenzake Dk. Deo nimewafahamu siku nyingi sana. Kwa maana hiyo ni mtu anayenifahamu vizuri tu. Kuna upotoshaji wa makusudi umefanywa ambao mimi nadhani una msukumo wa kisiasa.
Alichosema Dk. Ulimboka nilipozungumza naye, ni kwamba simu moja ilidondoka, nyingine wale watu waliomteka wameichukua pamoja na wallet yake. Hivyo alikuwa ananitajia vitu vilivyopotea. Nilipomuuliza iwapo anakumbuka namba ya simu, aliniambia nikamuulize Dk. Deo. Sasa nashangaa mtu aliyepenyeza uongo huu kwamba alisema mimi ndiye niliyempora hivyo vitu… sielewi ni nani na ana malengo gani.
Wakati anazungumza maneno haya, alikuwapo Profesa Museru ambaye ni Mkurugenzi wa MOI. Sina cha kuficha kamuulize tu, atakwambia alichosema Dk. Ulimboka. Yupo pia Dk. Deo, huyu ananifahamu na Dk. Ulimboka anasema walikuwa wote wakati anatekwa. Dk. Deo ananifahamu, akaulizwe iwapo mimi ndiye niliyemteka Dk. Ulimboka.
Profesa Museru:-
Mimi ndiye niliyempeleka pale wodini. Ni bwana mzuri tu. Nilimu-introduce (nilimtambulisha), akaanza mahojiano. Mimi hilo sikulisikia kwamba ameambiwa arejeshe simu na wallet, hilo sikulisikia.