Anayejua kuhusu hili la RITA anisaidie tafadhali

C
Okey,

lakini kwanini asipewe hapa cheti na kiandikwe kuwa amezaliwa kenya na mama mkenya ila baba ni mtanzania?
Na je, nikitaka kumuombea passport book sasa hivi atweza kupewa?
Brother acha kusumbua watu hapa...kwanza kwa akili zako hizo naona hata kisoda hakijai ....samahani lakini...unataka utashi wako uamue sio sheria iliyopo....unataka mapenzi yako yatimizwe kule Rita kama yanavyotimizwa nyumbani kwako...mambo hayapo hivyo ....kama we unasimamia ukweli uchwara.... ukweli wenyewe ndio huu...bila kufuata taratibu zao na kutengeneza mazingira wanayoyataka wao, hicho cheti utaendelea kukisikia tu kikitamkwa....wao wanasheria zao we unazako ....mpaka hapo ushashindwa.
 
Duh! Huyu mtu ameshaambiwa suala Hilo linahusisha mtoto aliyezaliwa/kuishi mataifa mawili tofauti hivyo process zake lazima zianzie Jeshi la Uhamiaji.
Lkn Bado anasumbua tu!

We unatakag kusema hao Rita wataaminije kama huyo mtoto ni wako na amezaliwa Kenya kweli?
 
Tanzania kuna ujinga sana kwenye jambo hilo.

Siku ukienda kumwandikisha shule ndiyo utafahamu ujinga wetu. Mwalimu shule atakwambia huyu siyo Mtanzania nenda wizara ya elimu, wizara ya elimu ukienda hakuna jibu la moja kwa moja, watakwambia nenda mambo ya nje, mambo ya nje watakwambia nenda mambo ya ndani watakwambialeta ushuzi, leta uharo, leta ujinga mpaka aandikishwe shule uko taabani. Ni ujinga ujinga mtupu, kote humo kila mtu anajifanya anajuwa kumbe hajuwi.

Yaani hata ufanye vipi sasa hivi, ikifikia shule na kutaka passport yake mwenyewe ya kusafiri ndiyo utajuwa kuwa hatujuwi.
Jamaaa mama mkenya baba mtanzania Ana miaka 18 kaambiwa alete kadi ya klinik
 
C

Brother acha kusumbua watu hapa...kwanza kwa akili zako hizo naona hata kisoda hakijai ....samahani lakini...unataka utashi wako uamue sio sheria iliyopo....unataka mapenzi yako yatimizwe kule Rita kama yanavyotimizwa nyumbani kwako...mambo hayapo hivyo ....kama we unasimamia ukweli uchwara.... ukweli wenyewe ndio huu...bila kufuata taratibu zao na kutengeneza mazingira wanayoyataka wao, hicho cheti utaendelea kukisikia tu kikitamkwa....wao wanasheria zao we unazako ....mpaka hapo ushashindwa.
Hatushindani mkuu tunaelimishana, sema nadhani tatizo nimekutana na wafanyakazi wa rita humu
 
Duh! Huyu mtu ameshaambiwa suala Hilo linahusisha mtoto aliyezaliwa/kuishi mataifa mawili tofauti hivyo process zake lazima zianzie Jeshi la Uhamiaji.
Lkn Bado anasumbua tu!

We unatakag kusema hao Rita wataaminije kama huyo mtoto ni wako na amezaliwa Kenya kweli?
Ninaloo faili la hospitali aliyozaliwa, passport kuthibitisha safari, cheti cha ndoa na hata temporary passport ya mtoto
 
Ila broo we ulioaje Kenya Kuna utaratibu wowote Wa kufata nina manzi wangu yupo kule nataka nimuoe kama vip
Unaenda tu kule unamuoa, then unakuja na bongo na cheti cha ndoa cha kenya unakipeleka rita then unalipia wanakupa cha hapa, sasa kwa mtoto sijui inashindikanaje
 
Mwanangu amezaliwa Kenya na mama Mkenya ila mie ni Mtanzania alienda tu kwao kujifungua sasa amerudi home leo ni mwaka mmoja tayari,

Nimeenda rita wamesema siku hizi unaomba cheti cha kuzaliwa online, sawa nimeingia account yao sasa wakati najaza maelezo ya mtoto nikakuta hakuna kuchagua inchi bali ni watoto waliozaliwa Tanzania tu, sasa hapa nifanyeje?

Anaejua tafadhali
Natanguliza asante nyingi
Ukitaka mfumo uwe unavyotaka wewe ni kujichosha akili tu, ni sawa na kufunga taili la gari kwenye Baiskeli.

Kama kazaliwa Kenya nenda Kenya ukamtafutie cheti cha kuzaliwa huko.
Kwenye mfumo wa Kenya utakuta option ya nchi ya Tanzania then utaselect Tanzania maana ndicho unachotaka tukushauri.
 
Mwanangu amezaliwa Kenya na mama Mkenya ila mie ni Mtanzania alienda tu kwao kujifungua sasa amerudi home leo ni mwaka mmoja tayari,

Nimeenda RITA wamesema siku hizi unaomba cheti cha kuzaliwa online, sawa nimeingia account yao sasa wakati najaza maelezo ya mtoto nikakuta hakuna kuchagua inchi bali ni watoto waliozaliwa Tanzania tu, sasa hapa nifanyeje?

Anaejua tafadhali

Natanguliza asante nyingi
Jambo hili Ki sheria liko hivi:
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania za sasa mtoto wake anachostahiki ni kupatiwa Tanzanian passport tu (Na sio cheti cha kuzaliwa cha Tanzania). Na wakati wa ku apply hiyo passport wataitisha birth certificate ya Kenya na kumtia kwenye passport faili yako (kama Baba mzazi) ili kumpatia hiyo passport.
Tanzania haitojali kama ana passport nyingine ya Kenya tayari kwa wakati huu. Mtoto atakapofika miaka 18 watataka uthibitisho kuwa mtoto hana passport ya Kenya, vinginevyo wakataa ku renewal/issue passport nyingine kwa wakati huo.

Kwa kawaida cheti cha kuzaliwa ni kimoja tu na duniani kote iko hivyo. Mtu huzaliwa mahali pamoja (au nchi moja) kwa wakati mmoja. Na ndio maana leo hii hata mtoto aliyezaliwa Dar -es-Salaam (TZA), ambaye mzazi au wazazi wake ni raia wa US anakwenda kuandikishwa tu kama raia wa US hapo US embassy Dar kwa kutumia cheti chake cha kuzaliwa kilichotolewa na mamlaka ya Tanzania.
Ushauri na Urahisi wa jambo hili:

Andikisha kuwa mtoto amezaliwa Tanzania na Mama yake Mkenya na wewe mwenyewe ni Mtanzania halisi....PERIOD:)
Note: Kenya watampatia tu passport yake ya huko kwani "Dual Citizenship" is one the constitutionally rights.

My one cent contribution.
 
Vuzuri sana, umenielewesha vizuri sana
Asante sana
 
Back
Top Bottom