Anatishia kuninyang'anya mtoto

Mkuu inategemea na majibizano yenu pengine ndo yalimfanya atamke hayo.
Kumbuka huyo ni mzazi mwenzio yapasa mtunziane heshima wote wawili kwa ustawi wa mwanenu.
Nakuomba wewe na huyo jamaa mpunguze jazba za kutarikiana kwenu kimahusiano na muelekeze nguvu zenu zote katika kumlea mwanenu.
Ushamtunza mwanao kwa muda mrefu bila msaada wa baba yake, ni suala la kupongezwa na kumshukuru Mungu hukupandwa na "roho wa kuharibu" ungeweza kumchoropoa angali "kizaigoti" kama kina mama wengine wafanyavyo!

Punguza jazba, report maendeleo ya mtoto kwa babaye kistaarab mwenyewe atajirudi na kukupa heshima kwa kumlelea mwanae na hakika atachangia malezi na matunzo...
Pole sana dada..
 
Pole sana Baby, ila bila yeye usingelimpata huyo mtoto unaye mwita "mwanangu" hawezi kuwa mwanao bali mwanenu daima daawamu. Soma vizuri uzi wangu. Nimekwambia mtoto akija kuwa mtu mzima, atataka kumjua babake, utamnyima?

Sijamnyima kumwona mwanaye,tatizo anataka kumchukua mazima wakati alimsusa toka mimba.ningeitoa mimba je?angeitwa baba leo?
 
Haya mambo magumu sana na hayana jibu moja. Kila jibu linategemea muda, mazingira na jamii husika.

Pajue kwao halafu utapata jibu mujarabu.

Pole!
 
Sijamnyima kumwona mwanaye,tatizo anataka kumchukua mazima wakati alimsusa toka mimba.ningeitoa mimba je?angeitwa baba leo?

Hizo ni hamaki tu Baby, tulizana tu. Hawezi kupenda tunda alichukie ua. Mwambiye mwanzo wa tunda ni ua. Akuliwaze kwanza usahau maumivu ndipo mkae chini na kumzungumzia mwanaye. Akija kimazungumzo, nakushauri usimkatalie hayo mazungumzo yake. Aje na mzee sio peke yake.
 
Inaonekana unampenda sana baba mtoto, ila kwa alichokufanyia unaamua kuvaa ubao usoni, na huyo baba mtoto yaonekana bado anasumbuliwa na utoto na nnahis saikolojia yake imevurugika. Na mbaya zaid pengine kazoea kuish maisha ya ubabe, sasa anashindwa kukuomba radhi na wewe unapenda umlee mwanenu bila kujali kilichotokea. (Nimejaribu kufikiri kwa sauti.)
 
Hata mimi nina ajira yangu,so naweza mlea vizuri tu.nimemnyonyesha bila choxhote kwa miezi 6 ,wadhani bila lishe ya uhakika ni mwanamke gani anaweza nyonyesha mtoto exclusive kwa miezi sita hapa mjini?
Mimi niliweza mbona
 
Mlee mtoto wako kwa upendo na usimjengee mazingira ya kumchukia baba yake.Naamini huyo jamaa anahisi aibu kukuomba msamaha kwa wakati huu ndo akajifanya anamtaka mtoto kwa nguvu ila kadri siku zinavyoenda atakuja kukuomba msamaha na mtashirikiana vizuri kulea mtoto wenu.
na wataongeza na mwingine na mwingine tena.
 
Wanaume ndo zao wanatelekeza watoto makusudi huku wanajipa moyo kwamba watoto wakikua watawatafuta. Ningekuwa mi ndo wewe wala sihangaiki na huyo baba nalea mwanangu vizuri tu ila nahakikisha anajua kwamba babaake alimkana akiwa tumboni. Hata wakija kutafutana huko mbeleni sawa ila lazima mtoto ajue ukweli.
 
Habari za mchana,

Nimezaa na kijana mmoja ambaye alinitelekeza toka niko mjamzito.Nilimove on na maisha yangu nikalea mimba haadi mtoto akazaliwa,hajawahi hudumia huyu mtoto tangu mimba hadi leo ana mwaka sasa.

Siwajui ndugu zake na wala kwao haijulikani kama hata ana mtoto kwani hajawahi hata mpeleka mtoto kwao,mtoto alipozaliwa nilimsihi amtaarifu japo mama yake aje kumwona mjukuu wake akakataa.

Leo nikiwa katika pilika za maisha nimekutana naye,baada ya salamu,akanambia nipe mtoto wangu au kama hutaki endelea kunilelea akikua nitakuja nikulipe gharama zako nimchukue,siko tayari kumpatia mwanangu kwani hakuna gaharama ya kufidia uzazi na malezi ya mwanangu.

Je inawezekana mtu kumnyanganya mtoto ambaye ulimtelekeza toka mimba? Nifanyeje?Nimetumia muda na rasilimali zangu kumlea mwanangu halafu leo mwanaume anakuja na kauli ya vitisho kutaka kuchukua mwanangu.
maneno tu hayo anabwabwaja. Kama angemtaka kweli kwanini asubiri mpaka akue? na kama ana hela za kulipa gharama kwanini asingeanza sasa basi kutoa gharama za matunzo ya kila siku. Mjinga tu huyo kaa nae mbali.
 
Habari za mchana,

Nimezaa na kijana mmoja ambaye alinitelekeza toka niko mjamzito.Nilimove on na maisha yangu nikalea mimba haadi mtoto akazaliwa,hajawahi hudumia huyu mtoto tangu mimba hadi leo ana mwaka sasa.

Siwajui ndugu zake na wala kwao haijulikani kama hata ana mtoto kwani hajawahi hata mpeleka mtoto kwao,mtoto alipozaliwa nilimsihi amtaarifu japo mama yake aje kumwona mjukuu wake akakataa.

Leo nikiwa katika pilika za maisha nimekutana naye,baada ya salamu,akanambia nipe mtoto wangu au kama hutaki endelea kunilelea akikua nitakuja nikulipe gharama zako nimchukue,siko tayari kumpatia mwanangu kwani hakuna gaharama ya kufidia uzazi na malezi ya mwanangu.

Je inawezekana mtu kumnyanganya mtoto ambaye ulimtelekeza toka mimba? Nifanyeje?Nimetumia muda na rasilimali zangu kumlea mwanangu halafu leo mwanaume anakuja na kauli ya vitisho kutaka kuchukua mwanangu.
Nenda ofisi za ustawai wa jamii zilizo karibu yako!
 
Mfyuuuuuuuuuuùu

Anadhani kuna fidia anayoweza toa?

Mfyuuuuuuu zake huyo.mwanaume trna mfyuuu kaniudhi

Upo mpendwa? Uwe na wiki njema

Haha. Huyu mpendwa alivyoelezea, ni kwamba uchungu wake upo zaidi kwenye muda na rasilimali alizopoteza. Hivyo vinaweza kulipwa, hatujui uwezo wa mshkaji.

Nipo mpendwa. Wewe ndio umeadimika kama rais wa Tanzania angani.
 
Sijakataa,wala sijawahi mnyima kumwona mwanae ingawa yeye mwenyewe ndio huwa hajishughulishi kumwona mwanaye.Na sina mpango wa mtoto kutomjua baba yake,tatizo ananitishia kumchukua mwanangu niliyembeba kwa uchungu miezi 9.
Na wewe kwanini umemwambia mtoto ni wake? Mwambie ulikuwa na mpango wa kando na ndo uliokumimbisha
 
HANA HAKI YA KUKUNYANGANYA NA ASITHUBUTU.....WE LEA TU KMA KAWAIDA BILA CHUKI KWAKE....ILA ASILETE UJINGA NA MAJIPU YA KULAZIMISHA
 
Back
Top Bottom