Amelaaniwa na mke wake, ameanza kuwa chizi

Wakuu, ninawaletea taarifa hii nikiwa ni mwingi wa huzuni na majonzi ya hali ya juu.

Hii si hadithi bali ni tukio la kweli kabisa lililomkuta mkuta rafiki yangu na sasa majuto ni mjukuu na sijui tufanyeje,habari yenyewe ipo hivi :
Rafiki yangu Ben (si jina lake halisi) alikuwa akiishi maisha magumu Sana, hana elimu yoyote, alikuwa akiishi Kwa kufanya kazi za ujenzi na vibarua jijini Mwanza, na mimi na wenzangu tulikuwa tukimsaidia matumizi ya hapa na pale Kwa kipato chetu kidogo.

Mungu hamtupi mja wake, Siku moja wakati akiwa anafanya kibarua cha ujenzi maeneo ya nyakato kwenye Nyumba ya mzee mmoja mwenyewe uwezo kimaisha, Ben akawa amebahatika kupendwa na binti Wa Yule mzee, ambaye alikuwa amemaliza kusoma Makerere university Uganda, binti Yule mrembo mwenyewe rangi ya chocolate alimpenda Sana Ben, Naomba nikiri kuwa japokuwa nilikuwa na mke wangu, nilianza kumwonea wivu Sana Ben, nikatamani yule mrembo angenipenda mimi, wakawa wameanza uhusiano wa kimapenzi, yule mzee alipogundua kuwa binti yake kampenda fukara, alimwonyesha haraka Sana avunje hayo mahusiano, binti hakusikia ndo kwanza akazidisha mapenzi Kwa Ben.

Wakuu, ktk hali iliyomshangaza kila mtu na asiamini kilichotendeka, yule mzee alichanachana vyeti vyote vya bintiye kuanzia O level hadi university.
Yule binti alilia Sana, hadi akataka kujiua, Kwa busara ya mama yake mzazi na sisi shemeji zake akawa ametulia na mama yake akawa amempatia pesa za kufuatilia vyeti vingine, badala yake Kwa hasira akawa kamwibia baba yake zaidi ya milioni 20,alizokuwa kaziweka ndani ili akanunue dhahabu porini, alikuwa ni mfanya biashara wa dhahabu.

Binti na mpenzie Ben wakawa wametoroka Mwanza na kwenda kisiwani ambako walianza kufanya biashara ya samaki huku wakiishi Kama mume na mke.

Mafanikio ya kimaisha yakaanza kuwapata, Ben akawa bonge la handsome na pesa kibao, mara akaanza kumbadilikia mkewe, kufumba na kufumbua akamwacha na kuoa mwanamke mwingine huku akimkashfu mkewe, walikuwa na miaka 3 ya kuishi wote na walipata mtoto mmoja Wa kiume.
binti Yule alilia Sana, nakumbuka kauli yake Kwa Ben, ilikuwa "Ukimaliza miaka miwili hapa duniani ukiwa salama, basi hakuna Mungu".

Tulimshauri Sana rafiki yetu hakusikia, baada ya miezi Kama 9 hivi Ben akaanza kufilisika na yule mwanamke mwingine akamkimbia .taratibu akaanza simu, mara viatu, mara nguo, Napoandika hapa sasa hivi analala kwenye mabaraza ya watu na ameanza kuwa chizi, mkewe hata sijui alipo, Ukimwona Ben Kwa wanaomjua inasikitisha japokuwa alijitakia, anatembea huku akiongea peke yake, nimejaribu kumsaidia nimeshindwa, mama yake kashindwa, watu wanasema hadi mkewe aonekane ndo pekee wa kumfungua.

Nimejifunza jambo zito Sana.
WHAT GOES AROUND COMES AROUND AKAOMBE MSAMAHA LAANA IPOTEE
 
Da inasikitisha sana tatizo watu husahau walikotoka ukipendwa pendeka ukitendewa mema nawe tenda mema. Bora yupo hai mnamuona kuna mkoa niliwahi kuishi wao ukiwatenda hivyo wanakutanguliza chini haraka kuna mdada alimsaidia mchumba wake kumlipia ada ya chuo ili waje kuish wote na walikuwa wamezaa mtoto mmoja cha ajabu yule kaka alipomaliza chuo alimkataa huyo dada na kuoa mwingine hakucheleweshwa .

Ni habari yakusikitisha sana kwa wote binti na huyo bwana ben. Lakini kwa kupitia mtandao huu huu kuna visa vingi sana vya wanawake wanaowatenda waume/marafiki zao baada ya kusaidiwa kama kusomeshwa, kutafutiwa kazi, nk. Je, kuna yeyote mwenye taarifa ya nini kinawapa wanawake waliowasaliti wapendwa wao baada ya kuwawezesha kimaisha? Itakuwa vizuri na hao tukawajua huenda ikatufundisha kitu kama tunavyojifunza kupitia kwa Ben.
 
Unapaswa kuelewa hakuna atendaye hila awe me au ke akaacha kupata malipo ya hila zake.
 
Da inasikitisha sana tatizo watu husahau walikotoka ukipendwa pendeka ukitendewa mema nawe tenda mema. Bora yupo hai mnamuona kuna mkoa niliwahi kuishi wao ukiwatenda hivyo wanakutanguliza chini haraka kuna mdada alimsaidia mchumba wake kumlipia ada ya chuo ili waje kuish wote na walikuwa wamezaa mtoto mmoja cha ajabu yule kaka alipomaliza chuo alimkataa huyo dada na kuoa mwingine hakucheleweshwa .
Ahahahahahahahahahahahaha!!!

Mkoa gani huo Mkuu!!??

Ahahahahahahahahahahahaha!!!
 
Unapaswa kuelewa hakuna atendaye hila awe me au ke akaacha kupata malipo ya hila zake.

Kueleweka ni sawa kabisa ila unapoweka mifano halisi kama huu wa hii thread inakuwa ni bora zaidi ndio maana nikaomba mwenye mifano kwa upande wa pili aweke hapa. Naamini mafunzo yatazidi kupatikana.
 
Binti alikuwa na upendo wa kweli kwa jamaa upendo usiohoji kwanini...halafu akatendwa pamoja na ku sacrifice na ku risk it all ikiwa ni pamoja na kumwibia mzazi , roho ya maumivu na ile laana ndio vinamtesa jamaa
Hapa kuna mambo mengi sana na kila moja limepata malipo yake sawia
1. Wote Tunaelewa umuhimu wa cheti..baba mtu alifanya vibaya sana kuharibu vyeti vyote vya mtoto
2. Wote tunaijua nguvu ya mapenzi, baba mtu alipinga kwa kila hali hayo mahusiano (malipo ikawa ni kuibiwa pesa)
3. Binti pamoja na kufanyiwa mambo yanayoumiza na mzazi wake lakini hakupaswa kuchukua hatua alizochukua...mzazi ni mzazi tuu (malipo yake ni kukimbiwa na mtu aliyempenda sana)
4. Kijana maskini kapendwa na mtoto wa kishua, akasaidiwa akasaidika halafu akaja kumtenda mkombozi wake (malipo yake ndio hayo)
Ili kuvunja hizi roho za laana visasi na maumivu ni watatu hawa kukutanishwa na kufanya reconciliation.....! Ikitokea mmoja mmoja akatangulia mbele ya haki yajayo mbeleni hayatakuwa na afya sana na ni afadhali atangulie Ben kuliko mojawapo wa hao wawili
Umejibu kitaalamu haswa! Sasa yule mke hapatikani, mleta mada hajatuambia miaka mitatu imemfanya nini bababinti.... labda kashakufa kwa presha ya kuibiwa 20m na bintiye. ili tupate conclusion ya kumshauri mleta mada.
 
Time will tell...God is always gud...! Unless otherwise
 
Back
Top Bottom