Kapyungu A
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 3,499
- 3,161
Baba angu toka 2013 mwishoni mpaka leo. Sina hamu na serikali na hawa watu. Ka mshahara kenyewe kalukuwa ka mkia ka mbuzi
Asante kwa taarifa.. Ila sasa kama hawana pesa mbona pale M city wanaporomosha ghorofa la zaidi ya bilioni sitini? Pesa inaoka wapii?Nachojua hawa PSPF hua wanalipa pale wanapopata pesa kutoka serikalini, yaani hawana Reserve ya hela ambazo zipo zinasubiri kulipa. Hii ni kwa sababu hawa PSPF hua wanapokea kutoka serikalini na infact serikali haipeleki hela ipasavyo kwenye huu mfuko (refer hotuba ya Rais May Mosi). Kawaida serikali kwa mwezi inatakiwa kupeleka kwenye huu mfuko takribani Tshs 40Billion, hela zinazotokana na Wafanyakazi kukatwa kutoka kwenye mishahara yao, lakini hilo limekua halifanyiki. Hii inapelekea hawa PSPF kutolipa kwa wakati muafaka, na kwa sasa wameshalipa mpaka wastaafu wa December 2015 na January 2016. Katika deni hili la serikali kuchelewesha makato wanadaiwa zaidi ya 250Billion na huu mfuko
Pili inawezekana kabisa huyo rafiki yako alikua muajiriwa wa serikali hata kabla ya mwaka 1999. kama jibu ni ndio basi huu mwaka wa 1999 serikali iliwahamishia wafanyakazi wake akiwemo huyo rafiki yako kutoka Hazina na kuwaleta kwenye huu mfuko. Sasa basi hapo kabla ya 1999 huyo rafiki yako makato yake yalikua yanaenda hazina lakini kuanzia huu mwaka yalikoma kwenda kwenye hazina na kuanza kwenda kwenye huu mfuko. Uhuni uliofanyika ni kua majina tu ndio yaliyohamishwa kwenda PSPF, lakini zile hela walizokua wakichukua hazina za makato hawakuwapa PSPF, na hapohapo serikali wanataka PSPF wakilipa mafao walipe hata na makato ya kabla ya 1999 ambayo hela hao PSPF hawakuzichukua. Kwa taarifa zilizoko ni kua deni hili ambalo serikali inadaiwa kutokana na hao wastaafu wa nyuma ya 1999 (Pre-99) ni zaidi ya 1Trillion.
Tatu ni kua Serikali iliwaahidi wananchi wa Dodoma kua itawaajengea Chuo Kikuu Kikubwa kuliko vyote East Africa kama ahsante kwa wnanchi hao kwa kuendelea kuichagua CCM (Political reason??!!). Sasa basi kama ujuavyo ahadi nyingi za kisiasa hua zinakuaga haziangalii uwezo wa kifedha wa serikali hivyo iliyaamuru mashirika ya mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF, NSSF, LAPF etc kushirikiana na kukijenga hiki chuo (UDOM). Chuo hiki kilijengwa kitambo tu na hadi leo serikali haijalipa huu mkopo kutoka haya mashirika. Kwa hili sina uhakika wa kiasi cha deni linalodaiwa ila nikilipata nitakuja ku-edit hapa
Hivyo namalizia tu kua mchawi wa malipo yako ni serikali na sio huu mfuko. Na kwa taarifa yako tu ni kua pamoja na wastaafu wengi sana kulalamika juu ya huu mfuko kuwacheleweshea malipo yako, lakini hutoona Mtumbua Majipu JPM kuwatumbua viongozi wa huu mfuko sababu hata yeye mwenyewe anajua jinsi serikali yake inavyodaiwa na huu mfuko.
Nimemaliza
wanazngua sana hawajamaaNakumbuka Zitto alikuwa anataka kupeleka bungeni marekebisho ya sheria kuhusu ili fao la kujitoa lifutwe.. Sasa kama hakuna aja ya kurekebisha sheria alitaka kupeleka bungeni ya nini?