Ama kweli Duniani kuna magumu ya kuamua

2008 umemaliza la saba na una demu, na uandishi wako huu!!!mbona kama mzee zaidi ya hapo???

Sasa nawe kwa akili yako ukamning'iniza faza ako???.pale ungeweka mpira kati,bila kufungamana na upande wowote.maana mpaka sasa sjui nani alikusomesha.
Mimi naona alijibu vyema kwani hakumnyooshea kidole yeyote
 
Internal nimesoma story vizuri,kwanza pole sana katika maisha kuna milima na mabonde,kuna nyakati za Giza na nyakati za mwanga na matumaini,hoja hapo niliyoielewa ni wewe kuwa na mahusiano hafifu au kutengwa na wazazi wako ndicho kitu ninachokuumiza na ambacho unataka Ku kisahihisha yaani kurudisha mahusiano vizuri na wazazi wako nadhani ni hilo,niweke sawa kama nitakuwa nimekosea.Kama ni hivyo kuna Dawa moja tu ambayo unaweza kuitumia haijawahi kushindwa kutibu kurejesha mahusiano yaliyoharibika.Dawa hiyo ni kuwa penda na kuwajali sana wazazi wako kuliko Jana na juzi,Upendo una nguvu kuliko kifo,wapende wazazi wako na usionyeshe kuwa wawo wanakuchukia au kukutenga,sijui una hali gani gani sasa lakini unaweza kutenga muda na pesa na kuaandaa matukio yatakayo onesha kuwa unawazajali,wasaalimu,watumie SMS za kuwapongeza kwa mambo mazuri waliyo Fanya,wanunulie zawadi,suti au vitenge,chukula,wakaribishe kwako,watembelee,huuu ni mfano tu vifunze kuwapenda kwa dhati na endelevu,kamwe usionyeshw hisia za kupambana nao,sahau yaliyotokea anza ukurasa mpya,hao ni wazazi wako wamebeba Baraka zako kutoka kwa Mungu,hamna namna wewe ni Mtoto na haukusababisha huo ugomvi,usifanye jambo la kumpendelea mama au baba kwa namna yoyote ile.kwa kusamalizi ni same wapende na wajali sana wazazi wako Upendo huo utaondoa hisia na mawazo yao mabaya kwako na mahusiano yatarudi tena mazuri kuliko mwanzo na kuhakikishia hili ndugu yangu,pole sana,Mungu atakusaidia.
 
Raimundo wewe nadhani ulishapitia life fln identity na mm la kijijini
 
Aysee mtazamo wako ni kama wangu yan.


Namm naisi kuna makubwa nyuma ya pazia kuhusu wawili hao ila mimi sipaswi kufuatilia zaid.

Kusoma nilipata msaada mkubwa kwa mama mzazi na babu mzaa baba.

Japo huko katikat baba aliingiza mkono wake kwa asilimia ndogo simhukumu ila nazungumza uhalisia wa mambo.

Kwa sasa nashukuru Mungu nimemaliza chuo sasa nipo kibaruani napambana na life kimtindo.

Mkuu kweli nawaza hata siku zingerudi nyuma uamuz tofaut na huo naukosa kabsa nabaki kichwa kinauma tu.
 
Raimundo wewe nadhani ulishapitia life fln identity na mm la kijijini

Sana I thank God kwamba tukio la namna hiyo kwangu lilikuwa la kupatanisha siyo kugombanisha, nakumbuka nilikuwa Form 3 that time wazee wakazinguana, mzee fasta kaja kunichukua ili twende naye ukweni ili niongeze nguvu kwa yeye kusamehewa.

Na walisameheana maisha yakaendelea, hizi changamoto zipo sana.
 

Hongera mkuu kwa kumaliza shule, kitu cha kufanya endelea kuwa karibu na kila mmoja kwa kadri unavyoweza hata kama anakukwepa, tuma tu hata salamu, kuna muda ukifika zitapokelewa.

Kuwa karibu na wadogo zako wote, waambie kilichotokea kati ya wazazi wenu hakitakiwi kuwatenga ninyi kama ndugu, jinsi mtakavyokuwa karibu ndivyo hata wazazi wanaweza kuja kuona kwamba wana deni la kusameheana na kusonga mbele, hata kama hawarudiani.
 
Dah kweli umu Elimu nje nje mkuu sasa ungekuepo enzi izo si ningekuwa niko salama kuliko ninavyojishusha sasa.

Kweli watu wajifunze umu watapata fundisho amazing umeliminimize tatzo kubwa limeonekana kama punje ya haradali mkuu.

Asante sana

Kuna leo na kesho hatujui tutakutana na lipi kesho kujifunza ni muhimu zaid.
 
Sawa sawa mkuu. ..

Kuhusu wadgo zangu mm kwao nikama simba ila tuna cheka na kupeana pongezi panapostahili ila kwenye kosa wananijua maana sitamani hata mmoja aonyeshe tofaut kwa mzazi yeyote yule
 
Sawa sawa mkuu. ..

Kuhusu wadgo zangu mm kwao nikama simba ila tuna cheka na kupeana pongezi panapostahili ila kwenye kosa wananijua maana sitamani hata mmoja aonyeshe tofaut kwa mzazi yeyote yule

Pendaneni tu na wadogo zako, endelea kuwaelekeza umuhimu wa kuto-take sides kwenye ugomvi wa wazazi. Ili wakirudiana kusiwe na aibu ya huyu nilimtenga nk.
 
Wewe uliwapelekea jambo lako la kheri la shule... Wao kwenye majadiliano wakapishana kauli kwa matatizo yao wenyewe...

Alafu hapo hapo kwenye kesi, wote wanataka ukadanganye kwa namna ambayo mmoja wao ahukumiwe kwa chuki zao wenyewe binafsi...

Ulichofanya ni sahihi kabisa kutokuwa upande wa yoyote yule.. Pinga moyo konde na maisha yaendelee...



Cc: mahondaw
 
Livescore nimekuelewa mara mbili kwa ushauri wako naahid kutoupuuza nauweka mezani kama sio leo bas kesho panapomajaliwa ya mwenyezi Mungu nauuingiza kwenye vitendo.

Naamini nitafikia hatua kufua moyo wangu uwe mweupe kama ilivyo theluji.

Thans moreeee mkuu
 
Nimekupata mkuu wangu

Thanx
 
Darasa la saba kua na demu hiyo kwa sie tuliosomea vijijini ni kawaida sn mwenyewe nilianza darasa la tano. Sijui nyie wa mjini. Pili kutegemewa kuna namna nyingi, kwani wewe apo ulipo km unae mtoto humtegei?
 
Kwakua ulikua Mdogo ndio maana ikawa ngumu. Ungesema hivi. Nawapenda wazazi wangu kwa hio mh.hakimu suluhisha ili niende shule. Walipoanza ugomvi nilikimbia
 
Darasa la saba kua na demu hiyo kwa sie tuliosomea vijijini ni kawaida sn mwenyewe nilianza darasa la tano. Sijui nyie wa mjini. Pili kutegemewa kuna namna nyingi, kwani wewe apo ulipo km unae mtoto humtegei?
Vizur maana umeelewa uhalisia wa neno kutegemewa
 
Kwakua ulikua Mdogo ndio maana ikawa ngumu. Ungesema hivi. Nawapenda wazazi wangu kwa hio mh.hakimu suluhisha ili niende shule. Walipoanza ugomvi nilikimbia
Dah kweli wajuzi wa mambo bado mpo.

Na utoto ule ningesema nlikimbia ningeeleweka piah.

Asante mkuu wangu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…