Alshabab Wavamia Kituo Cha Polisi Wajir Kenya

Dark Angel

JF-Expert Member
Sep 12, 2013
212
220
Wapiganaji takriban 100 wa kundi la kigaidi la Alshabab wamevamia kituo kimoja cha polisi Wajir Kaskazini mwa Kenya.

Hadi kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ama kufa haijajulikana lakini kinachothibitishwa na serikali kuwa walifaulu kuteka gari la serikali aina ya Land Cruiser.

''wavamizi walishambulia kituo cha polisi cha Diff na wakakabiliwa vikali na askari waliokuwepo, wengi wao walijeruhiwa ila walifaulu kuteka nyara gari la serikali la kituo cha Diff ambalo walitumia kuwabeba majeruhi wao'' alisema Inspekta Jenerali wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet.
Maafisa 3 wa polisi wa Kenya walijeruhiwa.

Kundi hilo lilitorokea mpakani.

Kikosi cha jeshi la Kenya limewafuata huko baada yao kuvuka mpaka kati ya Kenya na Somalia.

Chanzo: BBC
 
Keya inabidi iombe msaada kwa majeshi toka nje, hakuna namna. Yaan watu 100 wanateka kituo cha polisi! walipita bara bara gani wakati wa kuingia na kutoroka?
 
Nawachukia magaidi always wanatafuta sifa za bei nafuu. Sasa kituo kimoja cha polisi mnaenda 100. Kwenye kambi si mtaenda milioni.... Pumbavu!
 
Intelligence ya Kenya ina shida. Hapo unaweza kuona hao alshabab wanakuja kuvamia tena na kufanikiwa. Kama ilivyotokea mpeketoni.
 
Keya inabidi iombe msaada kwa majeshi toka nje, hakuna namna. Yaan watu 100 wanateka kituo cha polisi! walipita bara bara gani wakati wa kuingia na kutoroka?

Katika hali ya kawaida, kituo cha polisi hakilindwi na askari mia moja. Mara zote huwa wengi wako aktika shughuli mbali mbail za usalama kiasi kwamba aaskari wachache sana hubaki vituoni kwa michakato na dharura.

Kundi la watu mia moja hata kama lingeingia bila kificho ni dhahiri kwamba askari wanaokuwa katika kituo si rahisi kushinda. Ninaomba niwapongeze askari wa kituo hicho cha kenya kupambana hata kwa kiwango kile.

Wale ni magaidi. Tunahitaji kujua waliingiaje kituion wakiwa mia moja ili kupanua wigo wetu wa uelewa wa mbinu za mashetani haya. Lakini hata yangekuja yakitembea yamevaa kanzu kama ma mwana kijiji yana shida ama yanapeleka mtuhumiwa kituoni, polisi wasingeweza kuanza kuyashambuli kwa sababu wamefundisha kusikiliza malalamiko na kuyachukulia hatua. Hayo majitu kama yanekuja kwa namna hiyo maana yake ilikuwa lazima yafanya mashambulizi ya kushtukiza wakati polisi wakijaribu kusikiliza nini hoja ama kuyachunguza.

Yanaweza kuingia kwa zamu katika makudi madogomadogo kwa visingizio anuai baaadaye katika harakati yanaanza mashambulizi.

Yanaweza hata kuja moja kwa moja yamewasha mioto ya vurugu kwa kasi na polisi wasiweze kuyazuia kwa asilimia mia moja kabla hayajafanya uharibifu. Na hapo polisi utakuta yalikuwa yanakwenda kuongeza silaha.

Ni mawazo yangu. Labda tusubri wenye taarifa kutoka sehemu ya tukio watupe maelezo au magaidi walioko jf watuambie uzoefu wao.
 
Kambi ya Wakimbizi ya Dadaab ndio tatizo kuu kwa Kenya kulinda mpaka wake na Somalia.
Kuna idadi kubwa ya wakimbizi pale yapata laki tano na wanaendelea na maisha yao ya kawaida.
Na wakimbizi wenyewe ni Wasomali, hadi inakuwa ngumu kujua nani ni mkimbizi na nani Al Shabab.
Mbaya zaidi kuna biashara ya kipuuzi inaendelea pale inayofanywa na Wakenya wenye njaa.
Biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu toka Somalia wanaotumia ile kambi kama kituo cha basi.
Wasomali hukaa pale kambini huku wakifanya mipango ya usafiri haramu wa kufikishwa Nairobi.
Nimewahi kuona wengi wakifanikiwa kupita kwa njia hiyo. Hivyo, hii kambi ni tobo la maana kwa Al Shabab.
Na mbaya zaidi hii kambi ni kubwa mno, sijawahi ona kambi kubwa kama ya Dadaab.
Yaani imefanya Garissa kujaa Wasomali utadhani tayari ushafika Somalia.

Ova
 
Waongee nini na magaidi?? Wewe unadhani wakiongea hao magaidi wata demand nini??

WE DONT NEGOTIATE WITH TERRORIST!! hii ni slogan ya wamarekani kwenye swala kama hili naiunga mkono kwa 100%

"NO NEED TO NEGOTIATE WITH TERRORISTS"
 
Hahahahahaaa....eti magaidi walioko jf...duh haya bhana
 
Asee hili jambo
Mkuu, hivi ni lipi sahihi, hujui kuna magaidi JF au huwajui? Pls be serious, haya majitu ni mashetani yanajihudhurisha kila mahala. Hata kwenye vikao vya waendesha bodaboda yapo tu.

Mnatutisha ati...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…