The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,096
- 4,490
Ni yule mwanachama toka Kilimanjaro ambaye mara baada ya kuhoji na kupinga utaratibu uliowapitisha Bi Samia Suluhu Hassan na Dr Emmanuel Nchimbi kuwa wagombea u - Rais, haraka katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro naye bila hata kufuata utaratibu akapokea "maagizo toka juu" atangaze kuwa mzee huyu kafukuzwa uanachama...!!!
Soma: Pre GE2025 - Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama
Pia soma: Pre GE2025 - Aliyefukuzwa CCM baada ya kupinga Rais Samia kupitishwa mgombea pekee urais agoma kuondoka CCM
Maswali anayouliza hapa:
1. Ni kina nani waliufadhiri na kuudhamini mkutano mkuu ule wa Dodoma wa tarehe 19/01/2024 uliowapitisha hawa kuwa wagombea Urais wa CCM...?
2. Ni kwanini jina Makamu Mwenyekiti ambalo tayari lilishapitia kwenye mchakato wote ghafla liliondolewa na kupitishwa Steven Wassira...?
3. Kama mamlaka na maamuzi ya kuteua mgombea u - Rais na mgombea mwenza wake yako mikononi mwa wanachama kupitia vikao vya chama, ni kwanini aliyependekezwa kuwa mgombea u - Rais (Bi. Samia Suluhu Hassan) ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama taifa alikataa kutoka na kuwapisha wajumbe kumjadili pale alipotakiwa afanye hivyo sawasawa na utaratibu unavyotaka..?
4. Anamalizia maswali yake kwa kuuliza: Kama hiki chama hakijatekwa na watu wachache ambao huamua nani awe nani, ni kwanini kuna ukiukwaji wa taratibu kwa kiwango hiki..?
Pia soma: Pre GE2025 - Aliyekosoa uteuzi wa Samia kuwa mgombea Urais ahofia maisha yake