Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,870
- 5,047
Kada wa Chama cha Mapinduzi, Mchungaji Godfrey Malisa amesema hatambui uamuzi uliofanywa wa kumfukuza uanachama kwa kile alichodai hakuvunja Katiba ya CCM hivyo maoni aliyoyatoa kuhusu uteuzi wa Rais Samia kuwa mgombea pekee wa Urais yako sahihi.
Soma: Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?
Malisa ambaye anajiita kada mwandamizi wa CCM amesema mpango wake wa kwenda Mahakamani upo palepale na atakwenda kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa Urais katika uchaguzi wa Oktoba 2025.
Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.
Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.
Soma, Pia