Mjanja M1
JF-Expert Member
- Oct 7, 2018
- 4,023
- 14,187
Wakati kilio cha mgawo wa maji na umeme, na uhaba wa sukari kikiendelea nchini, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa imara anapoendelea kutafuta suluhisho la changamoto hizo kwa kuwa ni mambo ya kawaida kwenye uongozi.
Kikwete amesema anachoonyesha Rais Samia katika kipindi hiki, kinadhihirisha ushupavu wake katika uongozi, akieleza changamoto ni sehemu ya uongozi na utulivu wake unawafanya wananchi pia kuwa watulivu.
Kauli ya Kikwete ameitoa katika kipindi ambacho kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme, maji na sukari, ambayo bei yake imepanda maradufu.
Credit - Mwananchi