Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 76,271
- 121,362
Sifa ya utulivu inaweza kuwa ni chaka la kujificha viongozi ambao hawana maamuzi, hawajui la kufanya na wanaogopa au hawataki kujieleza.Wakati kilio cha mgawo wa maji na umeme, na uhaba wa sukari kikiendelea nchini, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwa imara anapoendelea kutafuta suluhisho la changamoto hizo kwa kuwa ni mambo ya kawaida kwenye uongozi.
Kikwete amesema anachoonyesha Rais Samia katika kipindi hiki, kinadhihirisha ushupavu wake katika uongozi, akieleza changamoto ni sehemu ya uongozi na utulivu wake unawafanya wananchi pia kuwa watulivu.
Kauli ya Kikwete ameitoa katika kipindi ambacho kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme, maji na sukari, ambayo bei yake imepanda maradufu.
Credit - Mwananchi
Rais ambaye kashatoa hotuba ya kueleza hatua anazochukua kupambana na tatizo la umeme, huyo unaweza kuniambia ni mtulivu.
Lakini, kama rais hajatoa hata hotuba ya kutupa mipango ya serikali, huyo huwezi kumuita mtulivu.
Huyo anaonekana hajui cha kufanya.
Tutajuaje rais ni mtulivu, na hajasema "Huu ni upepo utapita tu" bila kuchukua hatua yoyote?