Alichojibiwa Mkuu wa Wilaya Baada Ya kuomba Mchango wa Mwenge Kwa Mbunge

Sielewi huyu mkuu wa wilaya ilikua ni ombi au amri. Naomba ufafanuzi. Na kabla sijaupata naomba hizo pesa kama profesa anazo azipeleke kwa wananchi wapate maji. Nisamehe mh. DC
 
Kama huduma muhimu tumeambiwa ni bure kwa nini tuchangie mwenge? ina maana mwenge ni bora kuliko elimu?! Halfu wachangie mwenge wakati hawana maji?! Hilo jibu ndio haswa alistahili huyo mkuu wa wilaya ina maana yeye haoni shida ya maji hapo wilayani?
 
Hongera sana chadema kwa kuwapa nafasi vijana walalahoi watoto wa makapuku , ccm nafasi kama hizi hupewa watoto wa viongozi tu .
 
Mwenge kwa kiasi fulani unatokana na pesa za wananchi kuchangia maendeleo yao kwa njia isiyo ya kodi. Kwahiyo ipo miradi isingekuwepo km mwenge ungekufa.
nitajie mradi wowote uliozinduliwa na mbio za mwenge uliodumu hata kwa miezi 6.
 
Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni rapa, Joseph ‘Prof: Jay’ Haule, amedai alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ambayo Mikumi inapatikani kujulishwa kuwa alitumiwa barua kuomba achangie mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya mbio za Mwenge.

Akizungumza na wananchi wa Ruaha Mkoani Morogoro, Prof Jay amesema alimjibu mkuu wa Wilaya hiyo kuwa, kuliko kuchangia Mbio za Mwenge ni bora fedha zake aelekeze kwenye maendeleo ya Wananchi.

“Wakati nakuja njiani Mkuu wa Wilaya alinipigia simu, akanambia Mh tumeleta barua ofisini kwako kuomba mchango wako katika mbio za mwenge, nikamwambia daah hizo hela za kuchangia karibu milioni tano, ni bora nipeleke Ruaha maji yatoke tu” Alisema.
Huyu kijana namtabiria mambo makubwa sana huko mbele ya safari .
 
Attachments

  • IMG-20160419-WA0044.jpg
    IMG-20160419-WA0044.jpg
    19 KB · Views: 19
Naona hata JPM ameshindwa kabisa kuukataa na kuutumbua! Labda anaupa time tu! Tujaribu kuwa tunaweka miaka 3 ndio unakimbizwa hata zile sherehe za kila mwaka zipunguzwe iwe inafanyika miaka 3....
 
Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni rapa, Joseph ‘Prof: Jay’ Haule, amedai alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ambayo Mikumi inapatikani kujulishwa kuwa alitumiwa barua kuomba achangie mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya mbio za Mwenge.

Akizungumza na wananchi wa Ruaha Mkoani Morogoro, Prof Jay amesema alimjibu mkuu wa Wilaya hiyo kuwa, kuliko kuchangia Mbio za Mwenge ni bora fedha zake aelekeze kwenye maendeleo ya Wananchi.

“Wakati nakuja njiani Mkuu wa Wilaya alinipigia simu, akanambia Mh tumeleta barua ofisini kwako kuomba mchango wako katika mbio za mwenge, nikamwambia daah hizo hela za kuchangia karibu milioni tano, ni bora nipeleke Ruaha maji yatoke tu” Alisema.
Kama kweli alipigiwa na akajibu hivyo ni kheri atimize ahadi hiyo kwa wana Ruaha isijekuwa porojo tu akadhani anashuka mistari ya muziki.
 
Mwenge kwa kiasi fulani unatokana na pesa za wananchi kuchangia maendeleo yao kwa njia isiyo ya kodi. Kwahiyo ipo miradi isingekuwepo km mwenge ungekufa.
Kama mrai gani na ulifanikishwa kwa fedha kutoka wapi?
 
Kama mtu ameshashiriki mkesha wa mwenge basi atakubaliana nami kuwa ni sawa na kuhalalisha ulevi na uzinzi kwa siku hiyo!Watu hukesha wakinywa na kuishia kufanya ngono zisizo salama,makahaba wote hujaa kwenye mkesha wa mwenge!Hili dude halina faida zaidi ya kusambaza upendo wa ccm!
 
Back
Top Bottom