Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
30,643
33,995
Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?

N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.

Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.

Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.

DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.

Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.

Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.

Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.

Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.

Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.

Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.

Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.

Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.

TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

Ni kumbukumbu nzuri sana kuhusu Uhuru wetu lakini nadhani wengi wetu kama hatupendi hivi kuisikia na wakati mwingine tunawaona au tunamuona mwandishi kama muongo.
👇👇👇👇
Makosa yalifanyika wapi kiasi watu kutokupenda historia kusikia historia yao ya uhuru?
Shida nadhani ni kuweka mambo ya dini yaonekane iiishu kumbe hata hayana ishu yoyote
 
Ni kweli mambo ya dini hayana inshu?
Maana uhuru ulipiganiwa na watu na watu hao walikuwa na dini. Je ni kosa kusema watu wa dini fulani walipigania uhuru? Au itumike misamiati gani ili walau kuepuka kutaja dini?
Naomba tujadili hili.
Shida nadhani ni kuweka mambo ya dini yaonekane iiishu kumbe hata hayana ishu yoyot
 
Safari hii pissa anatrendi, kumbe lindi nayo ipo? Kina pengo na kilaini zama zao zimepita. Mwanahistoria anatanabaisha lindi ilikuwa ni ya kiislam na ndivyo tunavyojua ukanda huo ni islam tu, kumbe ukristo nao upo kitambo tu japo walikuwa wanaupotezea hawaendi kanisani kusali ungekuta lindi ipo mbali sana kimaendeleo ikaishia kuathiriwa na uislam. Kanisa lina shughuli pevu kueneza injili iletayo nuru gizani huko. Awali nilidhani lindi haina jimbo katoliki imeunganishwa na jimbo la jirani. Ni habari njema kumbe injili inasonga mbele huko
 
Hii historia ya kijinga itasaidia nini Kwa kizazi cha Leo?
kwa kweli kwa kizazi cha sasa hakivutiwi sana na mambo hayo. Mwanahistoria huyo ana akili mgando ya nyakati hizo, hataki kupata mtazamo mpya. Mzee bado anaishi anaishi nyakati zile za harakati za kudai uhuru toka kwa mkoloni. Sasa hivi wananchi bila kujali dini zao wanataka mabadiliko mapya katika zama mpya
 
Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?

N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.

Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.

Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.

DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.

Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.

Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.

Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.

Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.

Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.

Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.

Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.

Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.

TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

Mjahidina ameandika takataka (rubbish)...Sio kila jambo ni lakuandikia/kuzungumzia, mengine aache yajipitie.
 
Safari hii pissa anatrendi, kumbe lindi nayo ipo? Kina pengo na kilaini zama zao zimepita. Mwanahistoria anatanabaisha lindi ilikuwa ni ya kiislam na ndivyo tunavyojua ukanda huo ni islam tu, kumbe ukristo nao upo kitambo tu japo walikuwa wanaupotezea hawaendi kanisani kusali ungekuta lindi ipo mbali sana kimaendeleo ikaishia kuathiriwa na uislam. Kanisa lina shughuli pevu kueneza injili iletayo nuru gizani huko. Awali nilidhani lindi haina jimbo katoliki imeunganishwa na jimbo la jirani. Ni habari njema kumbe injili inasonga mbele huko
Kama hujui leo hii hao Viongozi walioko madarakani ndiyo wamegeuka kama wazungu wa kipindi hicho
,hawapendi kuona wapinzani wanaongea ukweli kila siku kujaza mapolisi kwenye mikutano ya wapinzani
Kuwa na macho matatu ili uelewe jambo
 
Kwa maoni yangu naona Mzee Saidi anaongelea mchango wa dini hasa viongozi wa dini ya kiislamu katika kupigania uhuru wa nchi yetu dhidi ya ukoloni, hivo anatukumbusha kuwa wanachokifanya Maaskofu kutetea Haki za wananchi ni sawa na kilichofanywa na waislamu kwa wakati huo.
Hivyo mchango wa viongozi wa dini si wa kupuuzwa. Kama sipo sawa mnaweza kunisahihisha au hata yeye mwenyewe Mzee Saidi anaweza kuendelea kutuelewesha zaidi ili tuelewe maantiki yake, badala ya kumshambulia kuwa ni mdini.
 
Back
Top Bottom