Ali Kamwe aombe radhi yaishe asilete ujuaji wake

Naye huyo sanda aache ufala... Watu kibao si walikuwa wanasema kaamua kutengeneza sanda (nguo ya maiti), mbona hakumaindi?

Ukiona imemuuma basi jua imemchoma na kumuingia kisawasawa. Kwa yale madekio halali yake amaindi
 
Defamation Haina uzito kwa tz tu kwakua watu wanachukulia poa, lakini kwa nchi za wengine ni bonge la case.

sio kosa kuponda jezi za Simba, kosa ni kutaja jina la mtengenezaji na msambazaji. kataja neno sanda ni kuharibu brand ya watu.

Sanda ni brand ndomana jina la sanda linasoma kwenye jezi za Simba. Kwahy kumtaja sanda Moja kwa moja ni kosa.

Ahmed Ally utamskia akiponda jezi za Yanga lakini huwezi kumskia akisema GSM katoa jezi mbaya, GSM ndo msambazaji wa jezi za yanga, GSM ni brand na yeye kama msemaji wa club kubwa anamamilioni ya watu wanaomfatilia , neno lake linasafiri masafa marefu.

Kumshambulia hadharani ni kuharibu biashara yake.

Hata kama watayamaliza kimya kimya lakini atapata funzo kuto kumshambulia mtu au brand yake Moja kwa moja. Nafikiri hata sanda Hana shida na hizo pesa Bali ni kumpa funzo kijana.
Hakuna kesi hapo, sanda ni sanda. Defamation gani hapo sasa. Sanda kakosa kazi.
 
Na ndo watu walitakalo apate funzo. Msemaji ni muhimu kujua kutenganisha utani wa Simba na yanga na biashara za watu wengine.
Kesi yenu ya yanga kutumia brand ya simba kwenye bango la 5-1 ilifikia wapi? Watu wa mipira mna ujinga mwingi. Hakuna kesi hapo sanda anawafurahisha makolo tu, na wala kamwe haogopi huo ujinga mnaoufanya. Na kesi ya kipanya na mwijaku nayo iko wapi? Hivi mnadhani defamation ni rahisi rahisi tu hivo
 
Kusema katoa jezi MBAYA kuna sababishaje jezi nzuri zilizo tolewa na SANDA ziwe mbaya?

Kama ni nzuri halafu atokee mtu aseme ni mbaya na mazuzu wa simba waache kununua jezi nzuri kwa sababu tu mtu wa yanga amesema ni jezi mbaya.. Tatizo litakuwa kwa nani?
Kwa kuwa weww si JK wala Sunday Manara, huwezi kuona athari ya kauli ya Ally Kamwe
 
sio kosa kuponda jezi za Simba, kosa ni kutaja jina la mtengenezaji na msambazaji. kataja neno sanda ni kuharibu brand ya watu.🔨
me naona hamna haja ya kuwa tunaponda jezi maana hata usimtaje mtengenezaji bado utakuwa umepunguza asilimia kazaa za wateja! tuongelee Mpira tu na ikiwezekana hawa wasemaji wangefutiliwa mbali kwny vilabu vyetu maana wamekuwa wakiharibu timu zetu! Jamani Sisi mbona tunaacha professional tunaendekeza uswahili. Sijawahi kusikia msemaji wa real Madrid, Barcelona, arsenal, na hata timu zingine
 
Kusema katoa jezi MBAYA kuna sababishaje jezi nzuri zilizo tolewa na SANDA ziwe mbaya?

Kama ni nzuri halafu atokee mtu aseme ni mbaya na mazuzu wa simba waache kununua jezi nzuri kwa sababu tu mtu wa yanga amesema ni jezi mbaya.. Tatizo litakuwa kwa nani?
Umeishia darasa la ngapi? Kuiponda jezi siyo inshu ze problemu iz ashura ma yutiai kumtaja sanda as a kit suplaya. Umeelewa dada mwajuma.
 
Yaani sanda asiliache lipite hivi hivi ikiwezekana atafute hata wanasheria 100 wamshikishe adabu huyo mtoto kama ni hela za kuwalipa hao wanasheria wanasimba wa tawi la kishua hungry lion tutachanga hela. Huwezi kuchafua brand ya mtu kirahisi na kipuuzi namna hii.
 
Sanda usikubali kumaliza mambo kimya kimya either mtoto aombe msamaha au u file case mtoto alipe b3 au akashikishwe ukuta segerea na nyapara.
 
Yaani sanda asiliache lipite hivi hivi ikiwezekana atafute hata wanasheria 100 wamshikishe adabu huyo mtoto kama ni hela za kuwalipa hao wanasheria wanasimba wa tawi la kishua hungry lion tutachanga hela. Huwezi kuchafua brand ya mtu kirahisi na kipuuzi namna hii.
Hata ukodi bar mzima, kama hakuna hoja kesi yako hushindi
 
Kusema katoa jezi MBAYA kuna sababishaje jezi nzuri zilizo tolewa na SANDA ziwe mbaya?

Kama ni nzuri halafu atokee mtu aseme ni mbaya na mazuzu wa simba waache kununua jezi nzuri kwa sababu tu mtu wa yanga amesema ni jezi mbaya.. Tatizo litakuwa kwa nani?
Kama ni utani angesema tu..makolo wametoa jezi mbaya baasi..lakini kasema bwana SANDA katoa jezi mbaya ndio maana viongozi wa Simba wamegoma kuzizindua ...huu ni ugonvi wake na SANDA.. Kamwe kakosea
 
Sasa nani ana kipimo cha jezi nzuri ama mbaya? Mahakama? Sanda kachanganyikiwa. Mie simba ila huu upuuzi wa drama hazina msingi ni wa kuachana nazo
 
Defamation Haina uzito kwa tz tu kwakua watu wanachukulia poa, lakini kwa nchi za wengine ni bonge la case.

sio kosa kuponda jezi za Simba, kosa ni kutaja jina la mtengenezaji na msambazaji. kataja neno sanda ni kuharibu brand ya watu.

Sanda ni brand ndomana jina la sanda linasoma kwenye jezi za Simba. Kwahy kumtaja sanda Moja kwa moja ni kosa.

Ahmed Ally utamskia akiponda jezi za Yanga lakini huwezi kumskia akisema GSM katoa jezi mbaya, GSM ndo msambazaji wa jezi za yanga, GSM ni brand na yeye kama msemaji wa club kubwa anamamilioni ya watu wanaomfatilia , neno lake linasafiri masafa marefu.

Kumshambulia hadharani ni kuharibu biashara yake.

Hata kama watayamaliza kimya kimya lakini atapata funzo kuto kumshambulia mtu au brand yake Moja kwa moja. Nafikiri hata sanda Hana shida na hizo pesa Bali ni kumpa funzo kijana.

View: https://m.youtube.com/watch?v=zeKNTddZVyI&pp=ygUaYWxpIGthbXdlIHV6aW5kdXppIHdhIGplemk%3D
Ukishaingia kwenye kitu chochote kwa timu hizi za Kkoo (iwe kibiashara au benchi la ufundi au chochote) utataniwa hata iweje, labda kama huu utani ufute jambo ambalo haiwezekani. Kamwe hatoomba msamaha wala kutoa hiyo hizo bil.
 
Naye huyo sanda aache ufala... Watu kibao si walikuwa wanasema kaamua kutengeneza sanda (nguo ya maiti), mbona hakumaindi?

Ukiona imemuuma basi jua imemchoma na kumuingia kisawasawa. Kwa yale madekio halali yake amaindi
Kutaja kila mtu anaweza kutaja lkn ni ktk nafasi gani aliyopo?

Kama ni mwenyeji hapa jf kuna user washatafutwa sana na Melo akasota sana mahakamani ku kutakiwa kutoa taarifa za wateja wake ili wakamatwe.
 
Nafikiri Kabla ya Kuzungumza nyakati zote twapaswa kufikiria kuhusu madhara ya tuyasemayo...
Kijana kwa bahati mbaya hakufanya hivyo...lakini kwa kuwa bado ni kijana mdogo...atiwe misukosuko kidogo kama funzo lakini maisha yake yasiharibiwe.
Lazima afundishwe funzo zito ili elimu isambae, Kwa umaarufu wake watu wengi watajifunza. Adhabu inayofuata ikibidi auze Mali zake zote Kisha arudi kijijini akalime.

Ikibidi mashabiki wamchangie tu. Hivi Mwijaku na KP waliishi wapi?
 
Ni mtazamo wako
Sasa kama anaona jezi mbaya unalazimisha aseme ni nzuri.

Kwa mfano nikisema soda ya Pepsi ni mbaya ni kosa?
 
Mbona huna msimamo we jamaa? We si ulisema unahama jf sports forum? Jitambue bhasi
 
Back
Top Bottom