Albamu ya Young Killer ina shida gani kwenye media?

Kinumbo

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
3,067
5,602
Yapata wiki mbili sasa toka kwa Rapa mkali hapa bongo Young Killer atoe albamu yake ya kwanza toka ameanza kuimba muziki. Nyimbo zote zinazopatikana kwenye albamu yake nimezisikiliza, kiukweli jamaa alitulia sana mpaka kufanikisha hiyo ishu. Nyimbo zote ni kali sana, hakuna wimbo nimeruka kwenye hiyo albamu.

Jambo linalonisikitisha ni kwamba sijawahi sikia stesheni yoyote ya redio ikicheza wimbo wowote unaopatikana kwenye hiyo albamu. Hii albamu ya Young Killer ina shida gani kwenye hizi stesheni za radio, ama ni Killer mwenyewe ndiyo ana shida?

Bonge moja la albamu ila ndiyo hivyo haipewi heshima inayostahili.
 
Unawaza Harusi kabla ya kutongoza.

Young killer ni rapper mkali, napenda sana uandishi wake wa tungo pia zile punch line zake ni habari nyingine. Binafsi Young killer ndio rapper mkali Tanzania.

Ishu ya media kutokucheza nyimbo zake kama ni kweli nadhani shida iko kwake mwenyewe sio kwenye nyimbo zake. Ila inaonekana ata Killer mwenyewe hatambui ni kwanini hawachezi nyimbo zake, ndio maana kwenye wimbo wake wa interview aliwachana. "kama ni ngoma natoaga kali kweli sasa kipi kinafanya wasigonge?"

Ila yote kwa yote huyo dogo hapati ile sapoti inayotakiwa, Killer kinacho mbeba na kumfanya mpaka sasa awe kwenye ramani ya muziki ni kutokana na kutoa mashairi makali sana ata bila sapoti anapeta tu. Bila hivyo angekuwa amepotea muda tu.
 
Mtoa mada ablam aina ubora ndio maana usikii nyimbo zake ingekuwa na ubora ungesika dogo kaimba style moja nyimbo zote tofauti ni maneno tu hata kaka zake kina prof Jay, kina. Juma nature enzi zile walichanganya radha mfano kina inaniuma sana hii hali sasa ngumu nk ila dogo yeye mwanzo mwisho mikato ile ile kujua ni wimbo tofauti tofauti ni kiitikio tu
 
Kwa tuliowahi kufanya rap tunajua. Yule dogo ana kipaji sana, anaandika (kama anaandikiwa kudos kwa mwandishi wake).
Kilichonifanya niache rap ni upumbavu wa kunyenyekea watu ili wacheze ngoma zako. Ndio maana wengine tulifanya ant virus kisha tukaachana na hiyo biashara
 
Exclusive interview bonge moja la ngoma aseee
 
Staili moja haifanyi nyimbo zisiwe nzuri, Young Killer kutumia staili moja ya uimbaji katika albamu hiyo sio sababu ya kufanya kwamba nyimbo zitakuwa sio nzuri.

Nenda kasikilize baadhi ya hizi nyimbo zinazopatikana kwenye hiyo albamu.

Young Killer Ft Watoto. Thank You

Young Killer. Respect

Young Killer. Yeah

Young Killer. Umenipata

Young Killer Ft Mr Blue. Umeniweza

Young Killer. Mrs Me

Young Killer Ft Unju. Dada Jambazi

Young Killer Ft Silabi, Maarifa, Unju na wengine. Harakati

Nenda kasikilize hizo pini kisha uje tena.

Mtoa mada ablam aina ubora ndio maana usikii nyimbo zake ingekuwa na ubora ungesika dogo kaimba style moja nyimbo zote tofauti ni maneno tu hata kaka zake kina prof Jay, kina. Juma nature enzi zile walichanganya radha mfano kina inaniuma sana hii hali sasa ngumu nk ila dogo yeye mwanzo mwisho mikato ile ile kujua ni wimbo tofauti tofauti ni kiitikio tu
 
Killer yuko njema sana na nzuri zaidi mashairi ana andika mwenyewe. Ni vile media zinambania ti bila sababu ya msingi.

Back
Top Bottom