Alan Turing: Baba(pioneer) wa computer za kisasa aliyeishi maisha ya utata kama shoga na kufa kifo tata kilichohusisha ushoga wake

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
45,730
64,912
Alan Turing anachukuliwa kama baba(mwanzilishi) wa computer za kisasa, Muingireza aliyezaliwa mwaka 1912 na kufariki mwaka 1954 katika kifo chenye utata mkubwa akiwa na miaka 41 tu.

Huyu ndiye aliyepangilia na kurasimisha nadharia za ufanyaji kazi wa computer za kisasa na pia kutengeneza Turing machine iliyokuwa kipimo rejea kwa computer mbalimbali zilizokuja kutengenezwa baadaye.

Turing alikuwa mwanamahesabu ambaye muda mrefu alifanya kazi za kufungua code(code breaker/cryptologist) katika idara mbalimbali za Uingereza hasa katika idara za ujasusi katika vita vya pili vya dunia alipoweza kutengeneza machine ya kufungua codes za enigma machine ya Nazi wa Ujerumani waliyokuwa wakitumia kuwasiliana vitani.

Baada ya vita vya pili vya dunia kumalizika aliajiriwa National Physcal Laboratory ya Uingereza ambapo alibuni mfumo wa Automatic Computing Engine(ACE) inayochukuliwa kama mojawapo ya computer za kwanza za kielectronics.

Mwaka 1952 Alan Turing alithibitika au alithibitisha mwenyewe kuwa shoga ambalo lilikuwa kosa la jinai Uingereza kipindi hicho akahukumiwa na mahakama kati ya kifungo jela au dozi ya kutibu ushoga(Uingereza walikuwa walikuwa wakiamini ushoga unatibika kwa dawa) ambapo alichagua dozi ya dawa za kutibu ushoga.

Mwaka 1954 Turing alikutwa amekufa nyumbani kwake na mfanyakazi wake katika kile kilichoripotiwa kula sumu ya cyanide, utata uliobaki ni kama alijua mwenyewe baada ya hali yake ya ushoga kuwa public na kupigwa marufuku kabisa kufanya kazi katika serikali ya Uingereza, alikula sumu hiyo bahati mbaya kwa sababu alikuwa akifanyia baadhi ya kazi za maabara nyumbani kwake au aliuliwa. Nadharia nyingine ni matibabu ya homoni kutibu ushoga wake yalimuathiri kupelekea kifo chake.
 
Back
Top Bottom