SIPENDI SIASA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 791
- 1,187
1. Nilikuwa maeneo ya parking ya Magari pale kitengo cha mifupa MOI mwaka 2014, nikiwa ninamsubiria mgonjwa ndugu yangu, jamaa alikuwa ofisini kwake, akaja akakagua kama mlango wa gari lake umefungwa vizuri, kisha huyo bila salamu akarudi tena ofisini kuendelea na shughuli zake.
NB: Sio kila kijana anayetokea Mbagala, Temeke, Kivule, Buza, Keko, Tandale, Vingunguti ni mwizi au kibaka. Wengine dressing codes zao ni za hovyo kwa sababu ya umasikini tu lakini hizo tabia za udokozi hawana hata kidogo.
2. Mdogo wangu graduate wa kidato cha 4 alipewa Jukumu la kumsindikiza mgeni (mzungu wa Norway) aende Kariakoo shimoni kushangaa shangaa kidogo, lakini yule aliyempa dili (mtoto wa kishua) akawa ana msisitiza mara kwa mara ya kuwa "hakikisha haukimbii na camera zake, alafu usimuombe ombe hela" sasa dogo akawa ananiuliza "brother hivi huyu jamaa mbona ananiona kama vile mimi ni kibaka?"
Nyie wenye Good life watoto wa kishua, please show us some respect aisee. Sio kila kijana wa uswazi ni mwizi au kibaka, ndio maana wengine ni ndugu zetu lakini tunaogopa hata kuwatembelea huko Ununio na Mbweni kwa maana kwa mavazi yetu tu mtatuona kama vile wezi.
~ SIPENDI SIASA ~