Akimtimua mkewe atakuwa na makosa?

Mambo mengine bwana, unaendeleaje sasa hapo kwasababu psychologically ushaharibika, hata ukibaki nae utafanyanae nn sasa?? Huwezi mwingilia kwasababu utahisi unaambukizwa. Na pia ndugu zangu wengine nani anae penda apate ugonjwa wa aina yeyote ile????
 
Kama walifunga kanisani lazima magomvi yao yote yapelekwe huko na sio mahakama za kiraia. mahakamani talaka utapewa ila kumbuka Mungu hataki talaka. suala la kutoachana kwa wanandoa ni suala la Kimungu ktk sheria asili(natural law). kumbe hata kama talaka imetolewa kokote, si halali na ni dhambi mbele ya Mungu.

KANISA HALIKAI NA MKE NA WALA MADHARA YA MKE KWAKO PADRE HAWEZI KUYA FEEL HIVYO VICTIM NI WEWE SUALA LA KUISHI KWA KUMRIDHISHA PADRE NI UJINGA ULIOKITHIRI ISHI VILE NAFSI YAKO INAVYOKUTUMA NA SIYO KANISA LIMEAGIZA NINI HIVI UNAYAJUA WATENDAYO WATAWA? WAO WANAISHI MAISHA YA KUIHADAAA JAMII NI WATAKATIFU WAKATI SIYO KWELI NA WEWE UNATAKA HUYU BWANA AISHI MAISHA YA KUWAFURAHISHA VIONGOZI WA DINI ILI HALI NAFSI YAKE IKIUNGU???
 
Ulivomuelezea mke wa jamaa ka mkeo vile,, yaani umemuelezea vizuuri da!! Any way mpelekee pole mwambie asimwache ila atafte namna ya kuishi nae pasipo kutesa hisia zake hasa ukizingatia ana mimba yake...
NB ufikishe kwa uaminifu kama ulivoleta huku..sasa ukute ni wewe
 
KANISA HALIKAI NA MKE NA WALA MADHARA YA MKE KWAKO PADRE HAWEZI KUYA FEEL HIVYO VICTIM NI WEWE SUALA LA KUISHI KWA KUMRIDHISHA PADRE NI UJINGA ULIOKITHIRI ISHI VILE NAFSI YAKO INAVYOKUTUMA NA SIYO KANISA LIMEAGIZA NINI HIVI UNAYAJUA WATENDAYO WATAWA? WAO WANAISHI MAISHA YA KUIHADAAA JAMII NI WATAKATIFU WAKATI SIYO KWELI NA WEWE UNATAKA HUYU BWANA AISHI MAISHA YA KUWAFURAHISHA VIONGOZI WA DINI ILI HALI NAFSI YAKE IKIUNGU???
kutoachana siyo sheria ya Padri na Kanisa tu bali ni amri ya Mungu. ukiitii unamtii Mungu na Kanisa lake
 
hata uzinzi si sababu ya kuvunja ndoa ya Kikristo. injili ya Mathayo 19 inayosema hivyo ilimaanisha ndoa za watu waliooana wakati ni ndugu ndiyo zaweza kuvunjika. hata hivyo huko si kuvunjika ndoa kwani tangu mwanzo wake muungano huo wa kindugu ulikuwa batili. no talaka kwa Wakristo! waulizeni viongozi wenu wa dini
...asimuache kwani alimtoa bikra?,..huyo pekee huwezi muacha!
 
Biblia inesema usiishi na mwanamke kahaba uyo kama kachepuka muache MUNGU kakulinda umepona hakuna sababu ya kuendelea kuishi nae.
 
Mh jamani hizi ndoa hizi
Kama ndio mimi, kama tunaishi nyumba ya kupanga, ningechukua nyaraka zangu muhimu tu ( Vyeti, passport nk) ningehamia sehemu nyingine kimya kimya kupona ukimwi sio masihara
Ninwachia kuanzia soksi hadi simu mashati na vyote
 
naona watu wanatetea vitu visivyowezekana. nani ameumbiwa kuishi kwa shida ya gubu, ujeuri nk kisa ndoa???
tuacheni fantasies!! kuishi na mtu mliyekulia mazingira tofauti aaafu akawa na tabia msizoweza kuvumiliana hakuna anayeweza. ni bora mkatengana kila mmoja akaenda kutubu kwa Mungu wake na kuendelea kuishi kwa amani. maana utajifanya unakwepa dhambi ya kutalikiana na ukaja kuua kabisa.
bora uishi mwenyewe tu
 
Mume angebahatika kuwa na hili tatizo, angeambiwa mke amvumilie mkewe na hayo ndio katika raha na shida lkn kwakuwa ni mke aachwe anakiburi, ndio maana napenda sana mitazamo ya watanzania.
 
Kwasababu wana matatizo ndani na mikwaruzano, basi hapo kuna zaidi ya hili la mwanamke kua na maambukizi aiseeee...,
It's too complicated sasa
 
Jamaa amefunga ndoa,ndoa ina miezi kadhaa hata mwaka bado ikafika kipindi wife akapata ujauzito.
Alipoenda kuanza clinic,vipimo vikaonesha ana maambukizi. Clinic wakamuambia aje na mumewe wapime wote, mume akapima hana hayo matatizo yupo salama.

Je jamaa afanyeje, ndoa na iwe basi au? Na pia mke ndo jeuri, kiburi, dharau na kejeli zimezidi mno mpaka nyumba inakuwa siyo sehemu ya kuishi mshikaji tena.

Je mshikaji akimtimua huyo wife atakuwa kakosea?

walifunga ndoa ya namna gani? kama ni Wakristo hamna talaka!
Kiapo cha ndoa: ....nitakupenda katika SHIDA na raha katika hali ya UGONJWA na uzima , nitakuwa na WEWE tuu mpaka KIFO kitakapotutenganisha
 
Apime tena after 3 months ajihakikishie kama kweli yupo salama.
 
Mwanamke anapokuwa mjamzito unahitaji hekima busara na uvumilivu kwakuwa atafanya mambo ambayo kwa kawaida asingeweza kuyafanya hasa kiburi hasira dharau na kususa
Lakini vile vile nani ana guarantee na maisha? Unamtimua leo mkewako wa ndoa au vinginevyo kwakuwa ana maambukizi kesho unapata ajali mbaya inayokuacha na kilema kibaya kabisa
Maisha hayana formula na upendo wa kweli huonekana wakati wa matatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom