Ajali mbaya Mbezi Afrikana

Hakuna kilichofichwa, madereva wanaendesha kwa spidi sana bila uangalifu. Usisahau hiyo barabara inapitisha wafanya tafakuri wengi kama mimi.......hasa usiku mkubwa
Kama unatumia hio njia weekend usiku utajua kwa nini ajali haziishi.
 
Hiyo barabara kutoka hapo Afrikana mpaka njia panda ya wazo sijui kuna kiumbe gani kimefichwa kwa chini
Mkuu Hakuna kiumbe! Kuna kosa tu la kiufundi, hii barabara Ni high way lakini Ina ingiza Au kutoa barabara nyingi Za pembeni Na hapo Ndio tatizo huanzia! Yaani wangeitegeneza Na sehem chache sana Za kuingilia Au kutoka! Yaani Kwa Hivi ilivyo Kila wiki hua tunatoa maiti barabarani..!

Kiukweli kama huijui vizuri hii njia hasa hili Eneo ukifika maeneo Haya unaweza kusema Sasa Ndio Muda wa kutest uwezo wa gari langu, Ila wenyeji hapa ukienda sana ni 60kph, Muda wowote unaweza kushangaa kicheche kimekatiza!
 
Watanzania wengi hawafuati taa za kuongoza magari,wana haraka sana.
Taa zitazingua! Waweke round about Africana Na Mbuyuni hii itasaidia sana kupunguza mwendo! Taa USIKU Jamaa wanatembea tu! Ila Hakuna mwenye ubabe kwenye round about!
 
Mleta mada hii taarifa yako na yenyewe ni taarifa mfu.
Lengo la taarifa ni ili wasomaji tupate kujua gari la nani?
Nani aliyehusika?
Je ni ndugu yetu kwa kiasi gani ni ndugu wa nani ni rafiki au la?
Sasa ukitoa taarifa ambayo haionyeshi namba ya gari wala wahusika inakua haina maana.
Jitahidi uwe unazingatia vigezo na masharti ya uandishi.
 
Me ni shuhuda gari ni land cruser v 8 no.DFL 598 mpya kabsa me nimeshudia mwenywe na picha nimepost hapo na cyo x trail kama mleta mada anavyoaminisha watu mwenye kujua muhsika ajitokeze liliteketea lote na yeye akiwemo ndani haijajulikana ni nani gari ilivyogonga truck ilianza kupga alam na mkanda ukajilock chakushangaza tulishndwa kumtoa kwenye gari
 
umakini barabarani unahitajika. hamna uchawi juu ya ajali hizi tusitishana. kuna uzembe au bahati mbaya lakini uchawi hamna!
 
Hata mm ningeshangaa eti wawekewe taa wakat magar yana taa labda angesema madereva wazingatiwe kupimwa macho yao

Hapana,Pamoja na taa za gari lakini barabara inapokuwa na taa zake yenyewe inakua bora zaidi Kiusalama!!! Hilo La kupima macho nalo ni La msingi kama ilivyo muhimu kwa kanuni zingine za Usalama barabarani
 
barabara kati ya mwenge na tegeta usiku inaua sana na hii inatokana na giza kali kwenye njia hiyo taa zinahitajika kumwezesha dereva kuona pande zote za barabara

Mkuu hivi katika barabara zetu kuu kama za Dar - Moro - Iringa - Mby au Dar - Chalinze - Segera - Moshi - Arusha nk, usiku nako kutahitajika taa za barabarani all the way? Umakini wa waendesha vyombo vya moto ni muhimu zaidi.
 
Me ni shuhuda gari ni land cruser v 8 no.DFL 598 mpya kabsa me nimeshudia mwenywe na picha nimepost hapo na cyo x trail kama mleta mada anavyoaminisha watu mwenye kujua muhsika ajitokeze liliteketea lote na yeye akiwemo ndani haijajulikana ni nani gari ilivyogonga truck ilianza kupga alam na mkanda ukajilock chakushangaza tulishndwa kumtoa kwenye gari
mlishindwa hata kupasua vioo hata kwa mawe?nieleweshe mi cjui mengi kuhusu gari!
 
Majira ya saa kumi na moja asubuhi kumetokea ajali mbaya sana eneo la Mbezi Beach Afrikana.

Gari aina ya Nissana xtrail au Honda ikiwa inatokea Mwenge imegonga kwa nyuma truck na kuungua hapohapo.

Kwa mujibu wa mashuhuda watu wawili waliokuwemo ndani ya gari wamefariki kwa moto wakiwa ndani.

Kwa adabu zangu sitoweza kuweka wala sikupiga picha.


View attachment 334553

View attachment 334554

Mmiliki alikuwa ni Dr. Richard Mgaya
 
Back
Top Bottom