AJALI: Daladala yaua wawili na kujeruhi kadhaa Mbezi kwa Msuguri

Nimepita hapo nikitokea maeneo ya Kiluvya,nimekaa kwenye foleni toka saa kumi na mbili na nusu mpaka sasa 2030,ajali ni mbaya sana na damu zimetapakaa mtaroni,maana ilibidi niegeshe gari ili nitembee kuona eneo la tukio nini kimejili.

Ni huzuni sana sana sana!!Inaweza kuwa uzembe wa mtu mmoja anasababisha binti mdogo kupoteza maisha na kuisurubu familia.

NB:Nimeongeza msamiati wa "Kivuko-Milia"...Duuu kweli HKL na KLF wanatutesa sana humu Jf

we jamaa mimi nakukubali sana i wish one day nikutane nawe. unaonekana bonge la mstarabu. Mungu ni fundi kwa kuwaumba watu kama wewe. Big up
 
Asante kwa taarifa ....poleni wafiwa baba yetu aliye juu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi.....swala la afande kupoteza kiatu ni too minor...usingeliandika
 
Weka picha basi TUONE hali ilivo kuwa. Otherwise mimi hata sijaona tija ya habari hii kama kila mmoja anasema tu maneno picha ya eneo la tukio hakuna!!
..usiwe kama sio ms€ng€ maji baridi,
.kwahiyo ulitaka watu wapige picha ya maiti ya mtoto mdogo alipasuka kichwa na ubongo umetapakaa ili wewe msengerema mmoja utoe pole?
...korchiputana!
 
Kuna ajali mbaya sana imetokea maeneo ya Mbezi kwa Msuguli jioni hii mkabala na maegesho ya malori ya kutoka mikoani.Ajali imehusisha gari (daladala) inayofanya safari zake kati ya Mbezi Mwisho na Muhimbili.

Ajali imeuwa watu wawili katika eneo la tukio na kuacha wengine wajeruhi.Waliofariki na mtoto mdogo (wa shule) ambaye amepasuliwa kichwa na ubongo kumwagika chini na mwanaume mmoja wa makamo.

Eneo limejaa damu na kutapakaa ubongo wa binadamu.Ni ajali ambayo huwezi kutamani kutazama picha wala kuziangalia maiti.Ajali imesababisha foleni ya zaidi ya saa moja na nusu.

Chanzo cha ajali ni gari ku-fail kushika breki na kusababisha kupitia waenda kwa miguu waliokuwa wanavuka kwenye kivuko-milia eneo la Msuguri.Waliokuwa kandokando wamekoswakoswa na gari kuangukia mtaroni.

Askari wa Usalama barabarani maarufu kwa jina la Mashaka (wanaopita njia ya Morogoro wanampata) ambaye karibu kutwa ya leo amepita vituo vyote kuwaondoa bodaboda na meza za wauza ndizi na kina mama wauza samaki,amenusurika kugongwa,askari wa kike naye amepoteza kiatu chake baada ya kuruka mtaroni kukwepa kifo.

Isingelikuwa oparesheni iliyoongozwa na askari wa barabarani kuwaondoa bodaboda na wauza baishara kando ya vituo vya daladala,leo Msuguri kungegeuka "machinjio" na msiba mkubwa.

Walio na ndugu maeneo ya Msuguri,au mtoto wa kike ambaye mpaka sasa hajafika nyumbani,wafuatilie polisi kujua maiti zilipopelekwa na kwenda kutambua miili ya marehemu.

Tuombe Mungu kuzikwepa roho za mauti na ajali zenye uzembe,madereva watazame vyombo vya moto kabla ya kuingia barabarani.Waendesha bodaboda waepuke kuegesha kando mwa vituo vya daladala na kuongeza msongamano unaosababisha ufinyu wa maegesho,na wale wauza pweza,karanga,ndizi,mahindi yenye mkolezo wa chumvi,matikiti na machungwa,wasogeze meza zao ili kutanua eneo la maegesho ktk vituo vya daladala
Huyo mwanafunzi alivaa sare za ranging gani kama unakumbuka?
 
Sipendagi mtu anaandika habari kwa mihemko ili kuvutia wasomaji...
Unaposema ajali mbaya sana.
Halafu kumbe imeua watu wawili tuu!!!

Na ajali za Majinja, Simba Mtoto tusemeje!!
Daah we Jamaa Mungu Akubariki Kwa Ulichokiandika ...
 
poleni sana mliopoteza ndugu zenu katika ajali hiyo in sha allah allah (s.w) awape subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Allah azijalie nguvu familia za wahanga na kulaza mahala pema roho za marehemu ... amen
 
Wabongo bwana...
Inasikitisha wapi wakati hata picha hatujaona...
Kwahiyo Namie nikiandika uzi sasa hivi kuwa Taxi imeua watu watatu hapa Kinondoni Biafra napo mtaanza kupayuka "RIP... Inasikitisha sana"

Nachukiaga kishenz habari za kusikia kutoka kwa mtu aliyesikia.

Sitoi pole wala cha nini, mpaka nione picha eneo la tukio.
Kichwa chako kipo sawa au una stress?!!

Unabwata as if mwili wako wa chuma ajali haiwezi kukuua..

Sometimes its very wise to stay silent, those words can get back to you at any time.
 
Hii tabia ya kuruhusu biashara kwenye kingo za barabara itadhibitiwa lini? Video vingine vya kusababishwa na mamlaka husika
 
Hawa madereva wamezidi sasa, inabidi kama makosa ni yao basi wao na wanaowaajiri waanze kuwajibishwa hapo ndipo heshima ya usalama barabarani itarudishwa kwa upande wao.

RIP
Ivi ww una matope kichwan? Umeshaambiwa gari ilifeli breki sasa ulitaka dereva aburuze miguu chini..? Anyway Mungu awape uvumilivu wafiwa wote
 
Kichwa chako kipo sawa au una stress?!!

Unabwata as if mwili wako wa chuma ajali haiwezi kukuua..

Sometimes its very wise to stay silent, those words can get back to you at any time.
Huyo jamaa ni kumwacha tu nadhani yuko na msongo wa mawazo
 
Kuna ajali mbaya sana imetokea maeneo ya Mbezi kwa Msuguli jioni hii mkabala na maegesho ya malori ya kutoka mikoani.Ajali imehusisha gari (daladala) inayofanya safari zake kati ya Mbezi Mwisho na Muhimbili.

Ajali imeuwa watu wawili katika eneo la tukio na kuacha wengine wajeruhi.Waliofariki na mtoto mdogo (wa shule) ambaye amepasuliwa kichwa na ubongo kumwagika chini na mwanaume mmoja wa makamo.

Eneo limejaa damu na kutapakaa ubongo wa binadamu.Ni ajali ambayo huwezi kutamani kutazama picha wala kuziangalia maiti.Ajali imesababisha foleni ya zaidi ya saa moja na nusu.

Chanzo cha ajali ni gari ku-fail kushika breki na kusababisha kupitia waenda kwa miguu waliokuwa wanavuka kwenye kivuko-milia eneo la Msuguri.Waliokuwa kandokando wamekoswakoswa na gari kuangukia mtaroni.

Askari wa Usalama barabarani maarufu kwa jina la Mashaka (wanaopita njia ya Morogoro wanampata) ambaye karibu kutwa ya leo amepita vituo vyote kuwaondoa bodaboda na meza za wauza ndizi na kina mama wauza samaki,amenusurika kugongwa,askari wa kike naye amepoteza kiatu chake baada ya kuruka mtaroni kukwepa kifo.

Isingelikuwa oparesheni iliyoongozwa na askari wa barabarani kuwaondoa bodaboda na wauza baishara kando ya vituo vya daladala,leo Msuguri kungegeuka "machinjio" na msiba mkubwa.

Walio na ndugu maeneo ya Msuguri,au mtoto wa kike ambaye mpaka sasa hajafika nyumbani,wafuatilie polisi kujua maiti zilipopelekwa na kwenda kutambua miili ya marehemu.

Tuombe Mungu kuzikwepa roho za mauti na ajali zenye uzembe,madereva watazame vyombo vya moto kabla ya kuingia barabarani.Waendesha bodaboda waepuke kuegesha kando mwa vituo vya daladala na kuongeza msongamano unaosababisha ufinyu wa maegesho,na wale wauza pweza,karanga,ndizi,mahindi yenye mkolezo wa chumvi,matikiti na machungwa,wasogeze meza zao ili kutanua eneo la maegesho ktk vituo vya daladala
Jiji la dar biashara zinafanyika barabarani na kwenye kingo za barabara sasa huwa najiuliza kwa nini tulienda mbele na kurudi nyuma kwa kasi hii yote? Viongozi wanafikiri kuruhusu biashara holela ndio kuwasaidia WA kipato cha chini lol! Lakini usalama WA watembea kwa miguu nao uzingatiwe Kwani ni aibu! Pita mtaa WA uhuru! Nje ya office ya mkuu WA mkoa na jiji lote kwa ujumla ni aibu Sana
 
Umaarufu wapi wewe....
Nyie mtashobokaje na habari ambayo haina reliable source..
Mtu kajiunga bando la chuo, anaandika uzi.. Nyie matumbo mbele kushoboka!!

Habari ya ajali halafu haina picha ni sawa na uozo wa utumbo wa nguruwe
Hujalazimishwa kuishobokea ss kimbelembele chako tu
 
Back
Top Bottom