SI KWELI Aishi Manula: Siumwi chochote, ila wao ndio wanajua nini kinaendelea

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Baada ya jana Klabu ya Simba kutoa taarifa kuwa mlinda mlango wao, Aishi Manula alishindwa kusafiri kuelekea Algeria baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Haya ndio majibu ya Tanzania One

"Siumwi chochote, ila wao ndio wanajua nini kinaendelea. Siwezi kuzungumza chochote, naacha wasimamizi wangu wazungumze." — Aishi Manula
1733407776761.jpeg
 
Tunachokijua
Aishi Salum Manula, ni mchezaji wa Simba S.C na Timu ya Taifa, Taifa Stars, anacheza kama mlinda mlango. Na pia amewahi kuchezea timu nyingine kadhaa, ikiwemo Azam fc

Mnamo Desemba 3, 2024 Klabu ya Simba ilitangaza idadi ya wachezaji watakaokwenda kucheza mchezo wa Pili wa kimataifa wa kombe la Shirikisho nchini Algeria, ambapo moja wa wachezaji waliotangazwa alikuwa Aishi Manula akiwa moja ya walinda mlango watakaokwenda kwenye mchezo huo.

Gd5Ve6PXMAAffjt

Aidha, Desemba 4, 2024 ilikuwa ni siku ya safari ya Simba SC kuelekea nchi hiyo kwa ajili ya mchezo huo. Ilipofika majira ya saa 8 mchana wa Desemba 4 2024 Simba ilitoa taarifa kupitia akaunti zake za Mitandao ya Kijamii kuwa Mlinda malango Aishi Manula amelazimika kuishia uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kutokana na kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuanza kwa safari.
1733400342673-png.3169550

Mara baada ya taarifa hiyo ya Simba juu ya mchezaji huyo, Chicharito JR Presenter kupitia ukurasa wake wa X alichapisha Nukuu inayodaiwa kusemwa na Aishi Manula, "Siumwi chochote, ila wao ndio wanajua nini kinaendelea. Siwezi kuzungumza chochote, naacha wasimamizi wangu wazungumze." — Aishi Manula

Upi uhalisia wa Nukuu hiyo?
JamiiCheck kupitia ufuatiliaji wa kimtandao imebaini kuwa Nukuu ya maneno hayo haikusemwa mahali popote na Aishi Manula. Aidha kupitia akauti Rasmi ya Aishi Manula ya Instagram hakuna ujumbe huo, na hakuna mahali popote kwenye vyanzo rasmi vya kuaminika ambapo amesikika akifanyiwa mahojiano aidha ya ana kwa ana au kwa njia ya Simu tangu kupata changamoto ya kiafya.

Vilevile, Chicharito JR Presenter alichapisha ujumbe huo hajaweka chanzo chochote cha taarifa ambacho amemsikia Manula akisema maneno hayo.

Pia, taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Simba na vyanzo Rasmi vya taarifa vya kuaminika ni kuwa Aishi alipata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya safari kwenda Algeria kuanza na ndiyo Taarifa pekee iliyoripotiwa
Kwann asiombe kuondoka maana kama Hali ndio imefika hapo unafanya vipi kazi?
 
Utopolo hapo juu kakoment kitopolo mnoo..huyo chicharito sijui alimuhoji wapi na saa ngapi? Yani watu wacancel tiketi iliyokua tayari kwa sbb ya propaganda zenu...
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom