Airtel "Imeolewa" na Diamond - lakini Je, huduma zimeboreshwa?

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,133
Nimeamka asubuhi nikakutana na ujumbe kutoka kwa rafiki yangu ambae ni mfanyakazi wa Airtel (TSM), akiwa amenitumia Tangazo jipya la Joti.

Nikatabasamu kwa kuwaza kwamba Airtel wamefanikiwa kumnyofoa Joti kutoka Tigo; nikawaza au labda huyu muwekezaji mpya alieingia Tigo amechagiza jamaa kuondoka?

Sikuishia hapo, nikaona ngoja niende kwenye ukurasa wa Instagram wa Airtel ili nione wana kipi cha kusema baada ya kumpata Joti kama balozi wao. Heh, si ndo' nikamuona Diamond!

Nilichokutana nacho kwenye maoni (comments) ni msiba; kwanza sikujua kabla kuwa kulikuwa na 'kiki' inaendelea ya kuwa Diamond anaoa! Kiki ambayo mpaka Mama yake mzazi aliishadadia (Tusisahau huu ni mwezi mtukufu).

Bado najiuliza aliyebuni hii kiki ya Airtel kuolewa na Diamond ni wa kike au wa kiume? Japo si mara ya kwanza kwa makampuni kutumia matangazo yenye ukakasi (Tigo ikiwa inaongoza kwa maoni yangu) lakini hili la Airtel naona kama lime-backfire kwa kiasi fulani.

Ukipitia sehemu kubwa ya maoni ya watumiaji katika ukurasa wa Instagram wa Airtel, inaonekana kuna shida upande wa huduma za Airtel - hazikidhi mahitaji ya wateja.

Airtel AD 1.png


Airtel AD 2.png


Naamini wamewalipa pesa nyingi sana Diamond na Joti ili kutengeneza "image" ya kampuni. Lakini sasa, naamini humu kuna watumiaji wa Airtel - pengine wale wa Instagram ni mamluki; vipi jamani - hali ya mtandao wa Airtel kihuduma ukoje? Ni kweli wana kasi ya Supa 4G? Kama ni kweli nataka ninunue ile Mi-Fi yao.... japo sijapenda suala la kuolewa na Diamond!
 
Kwenye maeneo kadhaa niliyotembelea vijijini ambako kuna minara ya airtel, kwa kweli kwenye supa 4G iko vizuri sana. Changamoto ni calls hupoteza utulivu kwa kiasi fulani.

Nina kile kifaa chao cha wi fi. Kiko vizuri kiasi fulani japo kuunganisha watu kumi at a time sina uhakika. Lakini nimetest hadi watu 6 kimeweza vizuri.

Kile kifaa kikisoma bar moja tu, ni mwendo mdundo.
 
Kwenye maeneo kadhaa niliyotembelea vijijini ambako kuna minara ya airtel, kwa kweli kwenye supa 4G iko vizuri sana. Changamoto ni calls hupoteza utulivu kwa kiasi fulani.

Nina kile kifaa chao cha wi fi. Kiko vizuri kiasi fulani japo kuunganisha watu kumi at a time sina uhakika. Lakini nimetest hadi watu 6 kimeweza vizuri.

Kile kifaa kikisoma bar moja tu, ni mwendo mdundo.
Safi, angalau umenipa matumaini.... kama hutojali, unaweza kutujuza maeneo ambako uli-test?
 
Back
Top Bottom