Agundua mumewe ana mtoto wa nje baada ya ndoa

Kinachomsumbua Huyu Dada kwa mtazamo wangu ni ubinafsi uliopitiliza anaawaza Mali zaidi kuliko ubinadamu.Sasa kinachomfanya amchukie huyu mtoto wa mumewe ni mambo ya urithi kwa kizazi chake.

Ni kweli, yani hili swala limemvuruga sana,hadi akawa anasema kama anaweza kuweka jina la mwanawe kwenye vitu vyake vyote, ndio maana nimeona niandike hapa naamini ushauri wenu utaenda kumsaidia sana
 
Alimficha kwa sababu alikua akimpenda na aliogopa kumkosa. Mwambie atanuna mpaka lini amkubali tu mtt wa mwanamke mwenzake.
 
Kwan yy ni wakwanza? wanawatoto nje Kwan mtoto huyo anakosa gan kwake? Mtu kaletwa tu aache roho mbaya akae nae vzuri huwez jua kesho kesho kutwa akasaidiwa na huyo mtoto ambaye anamchukia mwenyez mungu huwa na kusudi lake kwa Kila litokealo hapa dunian
 
Sasa analia nn? Mtoto kamkuta. Ingekua mtoto kamkuta yeye ingekua sawa. Aache roho mbayaaa mto hana kosa hapo. Kama mm ningempenda tu cz kila mtoto ana mbaraka wake. Amchukie mumew kwa kutokua open na hiyo chuki asiindeleze muda mrefu isije ika mcost zaid
 
Ila watu mnamsema tu bure dada wa watu. Hivi angekuwa single mother ndo kamficha mumewe kama ana mtoto, mngetetea hivi? Sioni tatizo kama dada from mwanzoni alishasema hataki kuolewa na single daddy. Possibly anajijua mapungufu yake ndo maana hakutaka kuja kumlea mtoto wa mtu. Mumewe amemkosea na hatuwezi kulipinga hilo afu tuseme dada wa watu mchoyo sijui ana roho mbaya. Hivi mnadhani ni rahisi hivyo kumkubali na kumpenda mtoto wa mtu mwingine kama mtoto wako mwenyewe wa kumzaa? Wengine hapa mnakaa tu na ndugu zenu wa damu ila mnawatesaaa. Mume awe tu mpole, aongee na mkewe kwa upole amshirikishe na mama mkwe wake, then ikiwezekana maisha yaendelee tu, gradually atazoea tu hiyo hali. Usimfiche mtu kitu kikubwa kama hicho, mbona watu kibao wanakubali kuolewa na single daddies, kuwa tu muwazi.
 
Jamaa kweli ana makosa lakini hatujajua kwanini hakumweleza toka mwanzo au mke alimsimulia kwamba hataki kuolewa na mwanaume mwenye mtoto naye alimpenda na alitaka awe mkewe amesubiri wakati ulipofika amemweleza inauma sana lakini hakuna analoweza kufanya mtoto yupo na hawezi kubadilisha ukweli huo kilichopo ajipe muda wa kukubali kilichotokea maisha yaendelee
 
ila mmoja sio mbaya ,mimi nilikua na bf wangu alinificha badae akaja kuniambia ana watoto wa 2 ,sikua na hamu nae tena tuliachana
 
Huyo mwanaune mpuuzi sana....
Alipaswa amueleze mwanamke mapema kabla ya ndoa ili aamue mwenyewe...kama yupo tayari kuwa mama wa kambo.

Sitashangaa kuna mijanaune itatetea......wakati ingekuwa mwanamke kafanya hivyo ingekuja na matusi yote na laana zote za dunia hii

Sio kila.mtu anataka kuwa mama wa kambo. Aeleze hisia zake kwa mumewe na aweke misimamo yake. Ingawa mtoto hana kosa ila aishi anavyojisikia asijilazimie kulea wakati moyo wake umekunja. (Amuulize kabisa wako wangapi maana kama kaweza kuficha labda wapo zaidi ya mmoja)

Halafu ujinga kama huu ndio hupelekea watoto wasio hatia kupata taabu. Kwa nini usinueleze mwenzio akaamua kama aolewe/aoe au asepe? Au ajiandae kisaikolojia pia?
 
Habari zenu wapendwa,

Rafiki yangu yuko matatizoni, aliolewa mwaka juzi na kubahatika kupata mtoto mmoja, kipindi chote cha uchumba wao mwanaume alimwambie (rafiki yangu) kuwa hana mtoto wa nje, sasa wiki iliyopita mume wake ndio akamkalisha chini na kumwambia kuwa ana mtoto ambae yuko kidato cha tatu.

Rafiki yangu alilia sana, na toka siku hiyo hadi sasa hivi, ametokea kumchukia mume wake coz anasema hakuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari, ana chuki kwa huyo mtoto maana hataki hata kukutanishwa nae, alijaribu kumwambia mama yake lakini anasema she is not on her side.

Naombeni ushauri wenu ili niweze kumshauri maana amekuwa mtu wa kulia tu,hadi pressure imekuwa inampanda, kazi anaharibu, ikifika muda wa kutoka kazini, hatamani hata kurudi nyumbani, yani hayuko sawa kabisa.

Asanteni
Huyo rafiki yako Ana roho mbaya sana, Mwambie arudi kwa mola wake aliemuumba kwanza, na hii ndo tabia yetu sisi ndo mana wanaume wanaamua kutudanganya mana tukiambiwa ukweli ni shida, na nadhani mwanaume alishamgundua huyo rafiki yako kuwa hapendi hayo na kwa vile mwanaume alimpenda aliogopa kumpoteza ndo mana aliamua kukaa kimya mpaka amuoe.

Kwanza muulize huyo rafiki yako Kuna tatizo kuwwepo kwa mtoto wa nje ya ndoa ambae umemkuta?? anaathiri vipi ndoa yenu? ameshawaza kuletea mtoto tayari akiwa ndani ya ndoa?? mwambie aache Roho mbaya hata yeye anaweza akatangulia kwa MUNGU na watoto wake wakaja wakalelewa na mwanamke mwenzake au anataka na wake waje wachukiwe? tena mfahamishe kama anataka ndoa yake iwe nzuri, akubali hayo yote aondoe kinyongo amkaribishe mtoto nyumbani na amuonyeshe mapenzi kama mtoto wake, akitaka kuiharibu ndoa kwa mikono yake aendeleze hizo chuki zake na roho mbaya kama mwaka huu kaletewa mtoto, mwambie mwakani ataletewa mchepuko.
 
Ni kweli, yani hili swala limemvuruga sana,hadi akawa anasema kama anaweza kuweka jina la mwanawe kwenye vitu vyake vyote, ndio maana nimeona niandike hapa naamini ushauri wenu utaenda kumsaidia sana
Kumbe shida ni mali? Pumbavu zake.na nusu
 
Jamaa kweli ana makosa lakini hatujajua kwanini hakumweleza toka mwanzo au mke alimsimulia kwamba hataki kuolewa na mwanaume mwenye mtoto naye alimpenda na alitaka awe mkewe amesubiri wakati ulipofika amemweleza inauma sana lakini hakuna analoweza kufanya mtoto yupo na hawezi kubadilisha ukweli huo kilichopo ajipe muda wa kukubali kilichotokea maisha yaendelee
Exactly ndo maana Nikasema tusimlaumu mke na mume awe mpole aongee na mkewe ampe sababu, maybe taratibuuu mke atakubaliana na hali. Kuna vitu unaweza kuvichukulia kawaida but vikabadili kila kitu kabisa hata kama ndoa itaendelea. Hatutakiwi kujenga mahusiano kwenye uongo. Ukute angemueleza dada mapema angekubali tu kuwa mama wa kambo. Mbona mara kibao tunasema sitaki kuolewa na mtu wa aina fulani, lakini ukakutana na hiyo package ukajikuta unacompromise tu.
 
Jamaa nae ana makosa yake kwanini akane damu yake tokea awali? Kua na mtoto nje sio ugonjwa,angemueleza tu mwenzie ukweli aamue kusuka au kunyoa.

Anyway maji yameshamwagika,najua huyo dada ameumia sana mana nitofauti na matarajio yake ila asamehe hilo na ajitahidi kukubaliana na ukweli japo itamchukua muda ila atazoea tu....

Asimchukie mtoto,mtoto hana kosa lolote ajitahidi kumpenda na kumwona kama mwanae,ajenge urafiki nae... Wakuitafuta amani ni yeye na wakuipoteza ni yeye. Achague amani na ataipata
 
Mwambie kuna wengine wanazaa nje ya ndoa wakiwa tayari wapo kwenye ndoa,
Aache mambo yake bhana
Inaonekana huyo mwanamke anapenda kujiweka juu ya mmewe au kujiona wa thamani kuliko mmewe
Ana kipato kikubwa zaidi ya mmewe?
Dah kidato cha tatu. Kama nidume basi jibaba, kama ni binti basi jimama. Yeye amchukulie kama mdogo wake tu maisha yaendelee. Au hapo kwao hakuna ndugu yeyote wanayeishi nae? Kama wapo peke yao basi huyo mwanamke bonge la mchoyo.
 
Kama anachosema ni Mali labda tatizo Ndio liko hapo kwani huyo mtoto anakuathiri Nini labda anakuambia umpatie mahitaji ya shule? Huyo mme wako aligopa kutuambia kuhofia atakukusa, kila mtu anaudhafu kama kwa mengine hana tatizo msamehe maisha yenu yaendelee na hakika mtaiishi vizuri tu
 
Back
Top Bottom