Agness Gerald (Masogange) afikishwa Mahakamani Kisutu, Apata dhamana

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,300
25,920
Mrembo anayepamba video za wanamuziki, Agness Gerald, maarufu kwa jina la Masogange na wafanyakazi 14 wa kampuni ya Quality Group wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka.

Masogange ambaye alikamatwa wiki iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano asubuhi akiambatana na wafanyakazi wa Quality Group.

Wafanyakazi hao wa Quality Group wanadaiwa kufanya kazi nchini bila kuwa na vibali baada ya kukamatwa na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule.

======
Wakati huo huo Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema Sepetu imeahirishwa hadi Machi 15 mwaka huu itakapotajwa tena kutokana na upelelezi kuto kamilika.

Chanzo: Mwananchi.

======
Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
Mbona Makonda na Sirro, hawajaitisha vyombo vya habali watangaze?
 
ndio maana hapa nilipo nimesikia tetemeko la ardhi maana baada ya hiyo dhamana nahisi alijitikisa kama kawaida yake

najua wanaume tunajua Aggy akijitikisa taharuki inayotokea

tuvumiliane hata kama nipo nje ya mada
 
Back
Top Bottom