Afrika na ukoloni mamboleo

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,207
69,306
jf habari zenu..?

Leo nataka tuzungumzie hili swala la ukoloni mambo leo na Afrika yetu.
kama tujuavyo bara letu lilitawaliwa na wakoloni,wazee wetu walipigana mpk leo tumefika hapa naweza sema asante kwao. kama historia yetu tunaijua na adui yetu tunamjua, kwanini tusiungane kwa pamoja tukamshinda adui kama wazee wetu walivyofanya.

Nimekuwa nikisikia watanzania wenzangu wakijadili kuhusu hili swala la ukoloni mambo leo pia hata mashuleni limekuwa likifundishwa endapo si kiundani zaidi. swali la kujiuliza je sisi ambao ni wahanga tumechukua hatua gani ili kukomesha jambo hili..? je, na viongozi wetu wanalichukuliaje swala hili..? Maana waswahili husema "usipoziba ufa utajenga ukuta"

Hawa jamaa hawana masihara wao wapo macho ili watimize malengo yao,
sisi ndo tumekuwa wa kila majanga umaskini na magonjwa mwendo mdundo,
Ubinafsi na vita ni kama ulimbo na ulimbombo. Nazani sasa fikra zetu zipambane na hili,viongozi na waafrika wote sizani kama tutashindwa.

THE POWER OF IDEA IS FROM ACTION....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…