jiwekuu770
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 2,246
- 1,645
- Thread starter
- #21
Upo sawa mkuuTafsiri sahihi kisheria (Nikikosea naruhusu kukosolewa ama kurekebishwa), juu ya neno ama maana ya adhabu ya jela / kifungo ni hii; INFLECTION OF SUFFERING AND PAIN, na mengine kama sijui kujifunza huko yanakuja baadaye sana, na tena yamekaa kisiasa siasa hivi.
Matendo maovu yote, likiwemo la ubakwaji kwa wanyonge (hasa wale wenye tamaa na wanaokubali kwa hiari yao wenyewe), yanafanywa uraiani, huko jela ni alama tu ya yanayotokea uraiani huku.
Siku zote na hadi kufikia mwisho wa dunia, vyombo vya kiserikali (mahakama, magereza, polisi), hawatakaa kuja kukubali ya kuwa hayo hayatendeki, yanatendeka sana, na mfano ni hata hapo juu watu wamelishuhudia hilo.
Hivyo, kwa kuthibiti hilo, kwanza lile neno - tafsiri niliyoiweka hapo juu, ibadilishwe ama kurekebishwa, maana wengi wanaingia jela kwa kusingiziwa, kuonewa, kubambikiwa kesi, na wengine hata kwa makosa ya kweli, ila kama akiingia na kuikuta hiyo tafsiri inafanya kazi midomoni mwa askari jela, pamoja na wafungwa wenzie, atahisi kama siyo kuamini, hata kulawitiwa ama kusagwa (kwa wanawake), ni moja ya ile tafsiri, hivyo kujikuta tu akikubali maana hakuambiwa kabla ya kuwa hilo halimo ndani ya ile tafsiri.
Mkinikosoa ama kunirekebisha, nitafurahi zaidi, maana wengi humu tunajifunza kila siku.
Ahsante!