LGE2024 ACT Wazalendo: Wagombea wetu wote warejeshwe, tuendeshe mambo kwa misingi ya haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,616
13,301
STATEMENT - Wagombea wetu warejeshwe Uchaguzi Serikali za Mitaa_page-0001.jpg

STATEMENT - Wagombea wetu warejeshwe Uchaguzi Serikali za Mitaa_page-0002.jpg

Tumepokea taarifa ya Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuongeza muda wa rufani za wagombea na kuelekeza wagombea wetu walioondolewa kwa sababu ya ngazi ya udhamini warejeshwe.
Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 09 Novemba, 2024 Kiongozi wa Chama chetu alitoa rai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia kuhakikisha kuwa wagombea wa vyama vya upinzani walioenguliwa wanarejeshwa.

Rai hii ilitokana na ukweli kuwa wagombea wetu walienguliwa kwa sababu za kisiasa na siyo sababu za kikanuni. Changamoto za kisiasa dawa yake ni siasa na siyo kutusukuma kwenye hatua za kikanuni ambazo wasimamizi wa uchaguzi walizikanyaga tangu mwanzo wa mchakato.

Tunaamini kuwa Waziri ametoa maelekezo aliyotoa kufuatia rai yetu hii pamoja na maoni ya wadau wengine wa uchaguzi huu. Maelekezo hayo ya Waziri yanafuatia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM na waandishi wa habari ambapo Katibu mkuu huyo aliomba TAMISEMI kurejesha wagombea walioenguliwa.
Kufuatia hatua hiyo tunatoa kauli ifuatayo;-

Hatua ya kuwarejesha wagombea wetu wote walioenguliwa bila sababu ni hatua muhimu. Tunaitaka TAMISEMI isimamie maelekezo yake kikamilifu kwani katika mchakato huu tumeshuhudia Wasimamizi wa Uchaguzi wakidharau maelekezo mahsusi ya kikanuni. Tutafuatilia kwa karibu mpaka kila mgombea wetu arejeshwe.

Tunataka kuona hatua za kinidhamu zikichukuliwa kwa watendaji wote wa TAMISEMI waliowaengua wagombea wetu kwa uonevu na ubaguzi. Haitoshi tu wagombea kurejeshwa bali lazima kuwepo na uwajibikaji.

Tunawakumbusha Chama tawala na Serikali inayoiongoza ni lazima kuhakikisha hatua muhimu tunazoziendea za Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, hatua za kampeni, uapishaji mawakala, upigaji kura na kutangazwa washindi zinafuata sheria na kweli zinaheshimu haki ya maamuzi ya wananchi ya kuchagua viongozi wao.

Pamoja na nia njema ya kuhakikisha demokrasia inastawi kufuatia maelekezo yaliyotololewa, haturidhiki na mtindo huu wa kufanya kazi kwenye mambo ya msingi kwa kusubiri utashi wa maelekezo. Uchaguzi ni mchakato wa kisheria na kikanuni na siyo hisani. Tanzania lazima itoke sasa kwenye demokrasia ya kupewa na badala yake tujenge demokrasia iliyosimikwa kwenye misingi ya kikatiba, sheria na kanuni. Demokrasia ya maelekezo ndiyo imetufikisha hapa tulipo na lazima tutoke hapa, miaka zaidi ya thelathini tangu mfumo wa vyama vingi kuanza.

Imetolewa na;

Ado Shaibu Katibu Mkuu ACT Wazalendo​

13 Novemba, 2024. Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom